Mi nshamdharau tangia kipindi kile alivyovunja ndoa ya mbasha.
Ni upuuzi na ulofa mkubwa sana kwa kiongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa
Gwajima aliwarekodi watu aliokuwa anaenda kuwapa ushauri wa kiroho.
Halafu anatangaza ushauri huo na matatizo yao hadharani.
Ole wako...ukimwambia siri zako utajuta.
Naona ccm sindano imewwingia haswa
Teh teh teh jamani laha sana ebu waacheni hawa watumishi wa bwana watupe raha .padri vs.askofu inanogaje?
Mkuki kwa nguruwe. ....aliyeanza kumchafua mwenzake nani?
Sio kosa lako, jina lako linatosha kufafanua who you are
Ukitaka kufaidi thread Kama hii, tafuta computer yenye screen kubwa yenye mwanga usioumiza macho pamoja na kopo kuubwa la bisi na bilauli moja ya juisi ya pensheni. Hapo ndio utajua utamu wa JF !🙂🙂
Ni muda mrefu jamii yetu imekuwa ikiwaheshimu na kuwaamini viongozi wa dini katika masuala mbalimbali ya kiroho na ustawi wa familia.
Ni jambo la kawaida sana kwa waumini wa dini zote kupeleka matatizo yao mbalimbali ya kifamilia kwa viongozi wa dini.
Ni dhahiri kwamba wengi wetu hupeleka masuala mbalimbali hata yale ya unyumba na siri nzito nzito za chumbani na familia kwa ujumla kwa kuwa tuna imani viongozi wa dini wana hulka ya kutunza siri na kusaidia kutatua matatizo yetu ya kiroho au kifamilia.
Hii ni tofauti kwa Gwajima ambaye ni mtomvu wa heshima ya kiongozi wa dini kwa kueleza siri za familia aliyoipa huduma za kiroho kisa tu kachokozwa kisiasa na yeye kajibu kwa kutoa siri za familia ya Slaa.
Angekuwa daktari angeweza kufutiwa cheti na kudaiwa fidia.
Lakini tukumbuke ni Gwajima huyu huyu aliyeshutumiwa kuvuruga ndoa ya Mbasha badala ya kutatua mgogoro wa familia hiyo.
Hii ni trend ya Gwajima anayejiita Bishop ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la Tahadhari hasa hasa na waumini wake wanaompelekea siri za ndani.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANI!!