Tahadhari kwa namba hizi

Tahadhari kwa namba hizi

Wakuu heshima zenu

Tahadhari kwa hizi namba tajwa hapo juu.

Siku ya Jumatano tarehe 19/10/2016 saa 3 asubuhi alinipigia bwana mmoja anajiita Samweli (0787-332977) akanitaja kwa jina nilosajili kwenye line yangu ya airtel na kuniuliza leo hujaenda kazini? Nikajibu ndiyo nipo home, akasema mimi naitwa Samweli(Mkurungezi wa kampuni nipo Dodoma) naomba uende AICC Hospital utamkuta Dr Shabani(0689-694153) mwambie Samweli ameniomba nisimamie mzigo wake wa dawa boxes 40 akataja jina gumu la dawa silikumbuki vizuri kila box shilingi 400,000 x 40 = 16,000,000.

Kuna mzungu anatokea KIA nakutumia no yake mara moja atakupigia mwambie wewe ni mwakilishi wa Kampuni na atakukabidhi million 24 cash, million 16 utalipa AICC na million 8 ni faida tutagawana mimi, mhasibu wangu na wewe, nikamjibu sawa. Baada ya muda mfupi akanipigia huyo Shabani A.K.A dr akaniuliza wewe ndiyo mwakilishi wa Samweli? Nikamjibu ndiyo. Mwambie wakaguzi wa TRA wanataka 480,000 cash bila mhuri wa TRA mzungu atakataa, nikamjibu kuwa ongea naye mimi nimeambiwa kusimamia kupaki mzigo (alipotaja hiyo hela nikaanza kushituka kuwa hapa kuna jambo). Baada ya muda Samweli akapiga cm akaniambia nimeongea na dr anataka 480,000 cash, akajifanya analalamika vibaya sana nikamwambia million 8 kutoa lakini 480,000 baki 7,520,000 mbona ni faida kubwa sana? Akasema isiwe tabu hapa mfukoni nina 280,000 naomba uniongezee laki 2 nikamwambia isiwe tatizo tuma hiyo 280,000 kwenye airtel money yangu nitaongezea hiyo laki 2 akasema sawa.

Baada ya kama dak 5 Shaban (dr) akapiga akasema Samweli amenitumia 280,000 amesema laki 2 unatoa wewe nikamjibu ni kweli natoa mimi lakini nipe dak 20 tu, baada ya dak 15 nikampigia nikamwambia nipo hapa getini japo sikuwa getini njoo unipokee au nielekeze ofisini kwako nipo na hela. Akasema ukiingia mlinzi atashituka nikamjibu mbona watu wengi wanaingia hashituki kwani anajua nakuja kufanya nini na wakati mimi nakuja kuonana na dr wangu? Wewe tuma kwenye simu nikamwambia poa ngoja niende airtel money town, Arusha airtel money ni za shida nyingi ni m-pesa akaniambia fanya haraka naandaa mzigo nije nao hotelini atapofikia mzungu na mhasibu wenu. Baada ya dak kama 5 mzungu feki(0787-407501) akapiga akaniambia anapata supu karibu na Golden Rose wapo na mhasibu wa kampuni lakini anavyoongea kimombo nikajua huyu ni tapeli, nikamwambia nakuja hapo nikufuate akakataa akasema anatafuta hoteli ya kulala na kupokelea mzigo.

Baada ya muda kidogo akanipigia Samweli (mkurugenzi feki) akaniuliza unafanya kazi gani? Nikamwambia nipo Monduli kambini akakata simu nikapiga hakupokea tena mpaka leo.

Hawajamaa ni matapeli wazoefu ukikurupuka unaenda na maji, maswali nilijiuliza inakuwaje mtu ambaye unamjua umuulize unafanya kazi gani? Kama wewe ni mkurugenzi wa kampuni dr anashindwaje kukuamini 480,000 wakati mnafanya biashara ya mamilioni? Maswali ni mengi sana siwezi kuandika yote.

Hawajamaa wamesajili majina yale ambayo wanayatumia kutapeli lakini ukituma pesa hutakaa uwapate na wanaomba hela kidogo iliusishituke. Tuwe makini jamani nimeona ni wafahamishe msije mkatapeliwa na sijui na wanazitoa wapi no za simu za watu pamoja na kutaja eneo ulipo, kama hawashirikiani na watu wa customer care basi wanashirikiana na watu wa karibu yako.

Tusikimbilie hela za haraka unaweza kutapeliwa kirahisi sana.

Nilichelewa kuirusha/post kutokana kuwa na majukumu mengine nilikuwa sijapata muda wa kuichapa.

Jamani mimi siyo mwandishi wa habari kwa hiyo mapungufu mtanisamehe japo lengo langu ni tahadhari kwa wadau wasijitapeliwa.

Asanteni.
huu wizi wa kizamani walikuwepo hawa watu wa jambo hilihili
 
Unasema wanaomba hela kidogo...laki 2 ndogo usawa huu??
 
Tufanyaje ilikuondoa huu utapeli? tuliambia tusajili line lakini naona tatizo ndiyo linazidi kuwa kubwa sana.
Ngumu sana ...nyingine winitext eti ww uko wapi bro mkeo anapointment na mshikaji wangu mmjoa hiv asikudanganye yuko kazin kumbe mm n mwanamke dahhh niliinjoy kuchat nae sana mana nilikuwa bored .....nilipimwambia nakuja ulipo nije kukupa hyo hela ya asante n atuende sehem ya kumfumania hapo akasema endelea na shuhul zako kwan alikuwa anataka nimtumie hela buku 20 ya kunywa bia akiwangoja mke wangu na shoga akke ambaye wangekuja kumfata mshikaj wake......
 
wengi wa wanaoingizwa mkeknge ni wale wanaotaka faida bila ya kuingia gharama za faida.....kazi kweli kweli.......!!!!
 
Usitume Pesa yeyote kwenye cm kutokana na ujumbe wa meseji hata kama ni ndugu,rafiki au MTU yeyote unayetaka kumtumia hela mpigie kwanza usikie sauti yake ndo yeye ndo utume Pesa sababu wakishapora simu haraka usambaza meseji za kuomba hela haraka kutumia simu hizo Kwa kukuelekeza utume kwenye namba wanayokupa ukibugi tu kutuma dakika washatoa Kwa Wakala hela.
 
Wanapataje no za watu kama wahashirikiani na watu wa customer care? ndiyo swali langu.
Huenda wanabuni namba yoyote kisha wanaangalia imesajiliwa kwa jina gani. Sina hakika kama wana-target specific number, nahisi ni random selection
 
Lakini mimi nilishaapa siku moja nitakuja kula hela ya tapeli.
Sababu wana-formula ya kutapelia kwa muda flani. Ikibuma wote kwa pamoja wanahamia formula nyingine!
Hii ya mzungu kuendelea kutapelia, haijakaa vizuri, kwa mjanja yeyote ni rahisi sana kuigundua.
Kuna hizi hela za chambo kwa ajili ya kuopolea mzigo ndohizo huwa nasema maranyingi kwamba ole wao!
Ingawa ni maranyingi sana nimewakosakosa, wakapitia tundu la sindano kusevia.
Siku1 waliingiza kiasi cha sh.4,000,000/= cash kwenye account yangu na wakanipigia cm kuniulizia kama hiyo cash nimeipata.
Nilivyo na kawaida kabla ya mjadala wowote lazima nihamishe salio lote kwenda account nyingine na kuitoa muda huohuo. Kama mtu katuma kimakosa hulazimu kumrejeshea baadae baada ya kujiridhisha.
Ss waliponiuliza nikwaambia subiri kdogo ntakujibu.
Nikaingia kwenye acct kuuliza salio nikaona cash mil.4. Nikaicommand ihamie kwenye acct nyingine ikagoma, ikidai salio halitoshelezi.
Tayari nikajua kwamba nipo kwenye ligi, mchezo wa kutafuta ubingwa!
Nikawapigia nikawaeleza kuwa nimekiona hicho kiasi nani kanitumia? Wakanitajia jamaa nisiye mfahamu na kunielekeza nimpigie kupata maelekezo. Lakini kabla ya kumpigia wakanitahadharisha, nimwamkie kwa lugha ya kinyenyekevu nikianza na shikamoo, maana ni mtu mzito na wa makamo.
Mtu huyo nilipompigia akanieleza fedhahizo zimeingizwa na boss wangu wangu ambae zamani tulikuwanae kazini. Na kwamba hizo pesa nisizichukue hadi Kwamba kanitumia hizo hela ili nimkopeshe kwa kumuongezea milioni2 kwa ajili ya kununulia uwanja maeneo ya mjini. Na kwakuwa mimi ni mwenyeji nimsaidie, kwenda hilo eneo na mil.6.
Nikawauliza kwa kutumia authentication kila swali. Nikagundua hawana lolote wanalolielewa kwangu ama kwa huyo boss wangu.
Nikawaambia kuwa tuonane popote wanapotaka wao ama waje nyumbani "kupopoa" hizo hela ambazo boss wangu kahitaji.
Ni hadithi ndefu. Lakini mara nyingi wanaoliwa huwa wanaaminishwa kupata faida maradufu ya fedha watakazotoa wao. Ni mbinu za kizamani. Ukiingiwa tamaa, lazima uliwe.
Mkuu na mwisho wao hela zao wakazichukua kwenye account yako!
 
Kwani kucomment bila kureply original thread hatusomi au maana unafcomplicate vitu watu hadi tuangaike kusoma upya ulichoreply... jiongeze
Be a real g8t thinker
inaboa hiyo kitu...
 
walinitapeli Kwa mara ya kwanza 1998 nikiwa moshi bado niko sec. walipojaribu tena 2002 nikiwa dar haikuwwzekana. walikuja na kichupa eti kina dhahabu thamani yake mil 11, eti gari waliokua wanasafiria limepata ajali. Halafu kapona peke yake.
 
Hawa matapeli ni hatari sana 2010 alikuja tapeli mmoja pale CBE Dsm akatulipia mpaka nauli kwenda Bandarini, kweli tukaenda wawili nikashituka anataka hela kwanza mwenzagu akaniambia huyu jamaa anatokea Shinyanga hawezi kututapeli ilikuwa mzigo wa 800,000 na kweli nilikuwa nazo hizo hela ila jamaa ambaye nilikuwa nasomanaye hakuwa na kitu, nikampa 260,000 wakaingia ndani nikawa nampigia cm namwambia usimkabidhi hela mpaka uchukue mzigo baada ya dak kama 10 akatoka analia amevua shati nikamuuliza vipi akasema tayari jamaa amenipiga, nikamwambia anilipe hiyo hela baada ya shimo la HESLB kutema akalipa kama 150,000 zingine nikasamehe. Ndiyo maana huwa nipo makini sana na huu utajiri wa haraka.
Hawa hata mimi walinikosakosa pale kkoo ghorofa la swahili, kaniambia ana mzigo wa ml 6 na ni kati ya bidhaa nnazouza dukani kwangu, wakati tunaondoka kufata mzigo kaniachia ctn 1 sample dukani, akataka nichukue na gari ya kubebea mzigo, na hela km laki 8 ya kumlipa mhifadhi mzigo, nikamwambia mi nnayo cash hapa nikiona mzigo na kuuhakiki nakupa hela yako yote,
Tumefika pale swahili nkapaki gari tukaanza kupanda juu ya ghorofa, (ikumbukwe mpaka mda huo cjashtuka kama natapeliwa)
Tumepanda ghorofa ya kwanza tunaelekea ya 2 ananizuia nisipande juu nimpe ela yeye laki 8 ampe mlinzi ili tupakie mzigo, ananiambia huku juu haruhusiwi kupanda mtu wakati mi naona kuna maduka, nkamshtukia nkasepa zangu na ile katon moja kaifata sikumpa nkamwonyesha rb nkamwambia ukiendelea kunisumbua ntakuitia mwizi, na ctn 1 ni sh 216000,
 
Laki mbili kwenye faida ya milioni nane siyo hela nyingi sana unaweza hata kukopa iliupate faida kubwa.
 
Laki mbili kwenye faida ya milioni nane siyo hela nyingi sana unaweza hata kukopa iliupate faida kubwa.
 
Wakuu heshima zenu

Tahadhari kwa hizi namba tajwa hapo juu.

Siku ya Jumatano tarehe 19/10/2016 saa 3 asubuhi alinipigia bwana mmoja anajiita Samweli (0787-332977) akanitaja kwa jina nilosajili kwenye line yangu ya airtel na kuniuliza leo hujaenda kazini? Nikajibu ndiyo nipo home, akasema mimi naitwa Samweli(Mkurungezi wa kampuni nipo Dodoma) naomba uende AICC Hospital utamkuta Dr Shabani(0689-694153) mwambie Samweli ameniomba nisimamie mzigo wake wa dawa boxes 40 akataja jina gumu la dawa silikumbuki vizuri kila box shilingi 400,000 x 40 = 16,000,000.

Kuna mzungu anatokea KIA nakutumia no yake mara moja atakupigia mwambie wewe ni mwakilishi wa Kampuni na atakukabidhi million 24 cash, million 16 utalipa AICC na million 8 ni faida tutagawana mimi, mhasibu wangu na wewe, nikamjibu sawa. Baada ya muda mfupi akanipigia huyo Shabani A.K.A dr akaniuliza wewe ndiyo mwakilishi wa Samweli? Nikamjibu ndiyo. Mwambie wakaguzi wa TRA wanataka 480,000 cash bila mhuri wa TRA mzungu atakataa, nikamjibu kuwa ongea naye mimi nimeambiwa kusimamia kupaki mzigo (alipotaja hiyo hela nikaanza kushituka kuwa hapa kuna jambo). Baada ya muda Samweli akapiga cm akaniambia nimeongea na dr anataka 480,000 cash, akajifanya analalamika vibaya sana nikamwambia million 8 kutoa lakini 480,000 baki 7,520,000 mbona ni faida kubwa sana? Akasema isiwe tabu hapa mfukoni nina 280,000 naomba uniongezee laki 2 nikamwambia isiwe tatizo tuma hiyo 280,000 kwenye airtel money yangu nitaongezea hiyo laki 2 akasema sawa.

Baada ya kama dak 5 Shaban (dr) akapiga akasema Samweli amenitumia 280,000 amesema laki 2 unatoa wewe nikamjibu ni kweli natoa mimi lakini nipe dak 20 tu, baada ya dak 15 nikampigia nikamwambia nipo hapa getini japo sikuwa getini njoo unipokee au nielekeze ofisini kwako nipo na hela. Akasema ukiingia mlinzi atashituka nikamjibu mbona watu wengi wanaingia hashituki kwani anajua nakuja kufanya nini na wakati mimi nakuja kuonana na dr wangu? Wewe tuma kwenye simu nikamwambia poa ngoja niende airtel money town, Arusha airtel money ni za shida nyingi ni m-pesa akaniambia fanya haraka naandaa mzigo nije nao hotelini atapofikia mzungu na mhasibu wenu. Baada ya dak kama 5 mzungu feki(0787-407501) akapiga akaniambia anapata supu karibu na Golden Rose wapo na mhasibu wa kampuni lakini anavyoongea kimombo nikajua huyu ni tapeli, nikamwambia nakuja hapo nikufuate akakataa akasema anatafuta hoteli ya kulala na kupokelea mzigo.

Baada ya muda kidogo akanipigia Samweli (mkurugenzi feki) akaniuliza unafanya kazi gani? Nikamwambia nipo Monduli kambini akakata simu nikapiga hakupokea tena mpaka leo.

Hawajamaa ni matapeli wazoefu ukikurupuka unaenda na maji, maswali nilijiuliza inakuwaje mtu ambaye unamjua umuulize unafanya kazi gani? Kama wewe ni mkurugenzi wa kampuni dr anashindwaje kukuamini 480,000 wakati mnafanya biashara ya mamilioni? Maswali ni mengi sana siwezi kuandika yote.

Hawajamaa wamesajili majina yale ambayo wanayatumia kutapeli lakini ukituma pesa hutakaa uwapate na wanaomba hela kidogo iliusishituke. Tuwe makini jamani nimeona ni wafahamishe msije mkatapeliwa na sijui na wanazitoa wapi no za simu za watu pamoja na kutaja eneo ulipo, kama hawashirikiani na watu wa customer care basi wanashirikiana na watu wa karibu yako.

Tusikimbilie hela za haraka unaweza kutapeliwa kirahisi sana.

Nilichelewa kuirusha/post kutokana kuwa na majukumu mengine nilikuwa sijapata muda wa kuichapa.

Jamani mimi siyo mwandishi wa habari kwa hiyo mapungufu mtanisamehe japo lengo langu ni tahadhari kwa wadau wasijitapeliwa.

Asanteni.
Hongera kunusurika kutapeliwa. Siku hizi matapeli ni wengi hali ya fedha ni ngumu, kuna wengine wanajidai ni FREEMASON wanatoa mamilioni, jihadharini nao pia
 
Hawa matapeli ni hatari sana 2010 alikuja tapeli mmoja pale CBE Dsm akatulipia mpaka nauli kwenda Bandarini, kweli tukaenda wawili nikashituka anataka hela kwanza mwenzagu akaniambia huyu jamaa anatokea Shinyanga hawezi kututapeli ilikuwa mzigo wa 800,000 na kweli nilikuwa nazo hizo hela ila jamaa ambaye nilikuwa nasomanaye hakuwa na kitu, nikampa 260,000 wakaingia ndani nikawa nampigia cm namwambia usimkabidhi hela mpaka uchukue mzigo baada ya dak kama 10 akatoka analia amevua shati nikamuuliza vipi akasema tayari jamaa amenipiga, nikamwambia anilipe hiyo hela baada ya shimo la HESLB kutema akalipa kama 150,000 zingine nikasamehe. Ndiyo maana huwa nipo makini sana na huu utajiri wa haraka.
Mkuu utakua na nyota ya kutapeliwa, mbona kila siku wewe tu.!
 
Wakikupigia jifanye lofa fulani jaribu kufuata maelezo yao na check mianya, unaweza kuishia kuwapiga wao, japo kiasi cha vocha, elfu tano, kumi, trust me guys its funny, the game worth to be played.
I do exactly that, I just play along and learn some of their new tricks or refinements . Huwa wanachoka,maana wakipiga unapokea,wakiongea ujinga unawakubalia tu,wakikupimia unaonekana fala tu ila hela haitoki hata kwa tindo.
 
Back
Top Bottom