Tahadhari kwa namba hizi

Tahadhari kwa namba hizi

Ukiwa na tamaa ya kupata hela nyingi kwa ghafla au kuamini mambo ya ushirikina lazima utatapeliwa.

Jana nilipokea sms ifuatayo kutoka kwa namba ya mtu nisiyemjua:
"Kaka ahsante sana kwa mganga uliyetuletea. Kwa sasa hivi baba hali yake inaendelea vizuri kabisa hadi tunashindwa kuamini kama baba ndiye yule aliyekuwa ameugua kiasi kile. Hata vile vifaa vyetu vilivyokuwa vimeibiwa nyumbani tumeshangaa tulipoamka asubuhi ya leo tumevikuta vimerudishwa mlangoni kwetu na wezi na vyote vikiwa vimetimia. Hakika duniani kuwa watu wana madawa....". Nikajua anakotaka kunipeleka. Niliyomwandikia siwezi kuyaandika hapa lakini hakurudia tena kuniandikia.
Hiyo text nishatumiwa nami siku moja nikaaipuuza na kumwandikia wrong number, nikaidelete,
 
Hawa hata mimi walinikosakosa pale kkoo ghorofa la swahili, kaniambia ana mzigo wa ml 6 na ni kati ya bidhaa nnazouza dukani kwangu, wakati tunaondoka kufata mzigo kaniachia ctn 1 sample dukani, akataka nichukue na gari ya kubebea mzigo, na hela km laki 8 ya kumlipa mhifadhi mzigo, nikamwambia mi nnayo cash hapa nikiona mzigo na kuuhakiki nakupa hela yako yote,
Tumefika pale swahili nkapaki gari tukaanza kupanda juu ya ghorofa, (ikumbukwe mpaka mda huo cjashtuka kama natapeliwa)
Tumepanda ghorofa ya kwanza tunaelekea ya 2 ananizuia nisipande juu nimpe ela yeye laki 8 ampe mlinzi ili tupakie mzigo, ananiambia huku juu haruhusiwi kupanda mtu wakati mi naona kuna maduka, nkamshtukia nkasepa zangu na ile katon moja kaifata sikumpa nkamwonyesha rb nkamwambia ukiendelea kunisumbua ntakuitia mwizi, na ctn 1 ni sh 216000,
Hii imetulia. Pambav zao kabisa!
 
1477295335172154669259.jpg 14772954370231018740114.jpg

Wengine hawa hapa
 
Hii tz ni full mausanii.siujui kwa nn vitu vya kipumbavu kama hivi mamlaka husika zinashindwa kutokomeza huu upuuzi.au sijui wana mkono wao.

Hizi namba huwa hazibadiliki na kuna wengi washatapeliwa watu wa usalama mpo wapi na mnafanya nn??
Kama jeshi la polisi halina wataalam wa IT wakufanya shuguli hizi kuna vijana wengi tuu mtaani wana taaluma na elimu za kutosha waajilini basi.sasa kama hawa wapuuzi wakitapeli kijinga hivi mnawashindwa je wakija wale matapeli wa kimataifa toka nigeria itakuwaje??

mitandao ya simu nayo sijui inafanya kazi gani mitandao ya simu nayo hovyo kabisaa yaani ni full upuuzi na sijui suala la kusajiri line lina maana gani.
 
Wakuu heshima zenu

Tahadhari kwa hizi namba tajwa hapo juu.

Siku ya Jumatano tarehe 19/10/2016 saa 3 asubuhi alinipigia bwana mmoja anajiita Samweli (0787-332977) akanitaja kwa jina nilosajili kwenye line yangu ya airtel na kuniuliza leo hujaenda kazini? Nikajibu ndiyo nipo home, akasema mimi naitwa Samweli(Mkurungezi wa kampuni nipo Dodoma) naomba uende AICC Hospital utamkuta Dr Shabani(0689-694153) mwambie Samweli ameniomba nisimamie mzigo wake wa dawa boxes 40 akataja jina gumu la dawa silikumbuki vizuri kila box shilingi 400,000 x 40 = 16,000,000.

Kuna mzungu anatokea KIA nakutumia no yake mara moja atakupigia mwambie wewe ni mwakilishi wa Kampuni na atakukabidhi million 24 cash, million 16 utalipa AICC na million 8 ni faida tutagawana mimi, mhasibu wangu na wewe, nikamjibu sawa. Baada ya muda mfupi akanipigia huyo Shabani A.K.A dr akaniuliza wewe ndiyo mwakilishi wa Samweli? Nikamjibu ndiyo. Mwambie wakaguzi wa TRA wanataka 480,000 cash bila mhuri wa TRA mzungu atakataa, nikamjibu kuwa ongea naye mimi nimeambiwa kusimamia kupaki mzigo (alipotaja hiyo hela nikaanza kushituka kuwa hapa kuna jambo). Baada ya muda Samweli akapiga cm akaniambia nimeongea na dr anataka 480,000 cash, akajifanya analalamika vibaya sana nikamwambia million 8 kutoa lakini 480,000 baki 7,520,000 mbona ni faida kubwa sana? Akasema isiwe tabu hapa mfukoni nina 280,000 naomba uniongezee laki 2 nikamwambia isiwe tatizo tuma hiyo 280,000 kwenye airtel money yangu nitaongezea hiyo laki 2 akasema sawa.

Baada ya kama dak 5 Shaban (dr) akapiga akasema Samweli amenitumia 280,000 amesema laki 2 unatoa wewe nikamjibu ni kweli natoa mimi lakini nipe dak 20 tu, baada ya dak 15 nikampigia nikamwambia nipo hapa getini japo sikuwa getini njoo unipokee au nielekeze ofisini kwako nipo na hela. Akasema ukiingia mlinzi atashituka nikamjibu mbona watu wengi wanaingia hashituki kwani anajua nakuja kufanya nini na wakati mimi nakuja kuonana na dr wangu? Wewe tuma kwenye simu nikamwambia poa ngoja niende airtel money town, Arusha airtel money ni za shida nyingi ni m-pesa akaniambia fanya haraka naandaa mzigo nije nao hotelini atapofikia mzungu na mhasibu wenu. Baada ya dak kama 5 mzungu feki(0787-407501) akapiga akaniambia anapata supu karibu na Golden Rose wapo na mhasibu wa kampuni lakini anavyoongea kimombo nikajua huyu ni tapeli, nikamwambia nakuja hapo nikufuate akakataa akasema anatafuta hoteli ya kulala na kupokelea mzigo.

Baada ya muda kidogo akanipigia Samweli (mkurugenzi feki) akaniuliza unafanya kazi gani? Nikamwambia nipo Monduli kambini akakata simu nikapiga hakupokea tena mpaka leo.

Hawajamaa ni matapeli wazoefu ukikurupuka unaenda na maji, maswali nilijiuliza inakuwaje mtu ambaye unamjua umuulize unafanya kazi gani? Kama wewe ni mkurugenzi wa kampuni dr anashindwaje kukuamini 480,000 wakati mnafanya biashara ya mamilioni? Maswali ni mengi sana siwezi kuandika yote.

Hawajamaa wamesajili majina yale ambayo wanayatumia kutapeli lakini ukituma pesa hutakaa uwapate na wanaomba hela kidogo iliusishituke. Tuwe makini jamani nimeona ni wafahamishe msije mkatapeliwa na sijui na wanazitoa wapi no za simu za watu pamoja na kutaja eneo ulipo, kama hawashirikiani na watu wa customer care basi wanashirikiana na watu wa karibu yako.

Tusikimbilie hela za haraka unaweza kutapeliwa kirahisi sana.

Nilichelewa kuirusha/post kutokana kuwa na majukumu mengine nilikuwa sijapata muda wa kuichapa.

Jamani mimi siyo mwandishi wa habari kwa hiyo mapungufu mtanisamehe japo lengo langu ni tahadhari kwa wadau wasijitapeliwa.

Asanteni.
Asante mkuu na pole sana

Mimi binafsi wameshanipigia mara 2, mwaka ,moja nikiwa mkoani morogoro , Mara ya pili nikiwa mkoani kagera

Wa morogoro
Alinipigia akataja jina langu na fani yangu , akaongea kuwa anafanya Kazi ofisi ya waziri mkuu kitengo cha kilimo kwanza na yuko iringa ,

Maelezo yalifanana kama yako ila alitlhitaji msaada wa bailing za tractor na alitaka mimsaidie akaniunganisha na dealer ambaye alikuwa mwanamke ambaye alimtambulisha kama kanali wa jeshi ( mzinga), na mhasibu aliyefikia Mildland hotel , yaani walizunguka mwisho yule kanali akadai mzigo upo tayari na inatakiwa laki 4 , ndio mzigo utoke jeshini maana mhasibu wa jeshi katia ngumu , aisee dau nililokuwa nimetangaziwa lilikuwa kubwa yaani kila bailing moja laki 6 na bailing 10 hvyo mil 6, na nikipewa hizo pesa ni dipost mil 4 kwenye akaunti yake na Mimi nichukue 2 , aisee lilikuwa dili la fasta kidogo nichanganyikiwe


Nilichofanya nikamwambia yule kanali wa uongo tukutane gate la chuo kikuu cha SUA , sababu alinambia yuko mzinga , basi nikasubiri kama dk 5, ikapigwa simu aisee mzigo upo tayari , hivyo nimekwama laki 2 , maana nimeambiwa nitoe laki 4, risit itoke sababu mzigo ni wa magendo , duuh nikashituka

Ikabidi nimpigie , jamaa aliyenipigia mwanzo yule wa ofisi ya waziri mkuu
Akadai yuko porini hana access na Mpesa hvyo nitoe then watarudisha pesa yule mhasibu wa kilimo kwanza akitoa , hapo nikashtuka


Nikamwambia nipe muda , kama dk 30 nikapiga , jibu namba unayopiga haipatikani ,nikajaribu ya kanali haipatikani , hapo nikagundua kweli walikuwa matapeli ,

Jina la tapeli huyo alijitambulisha kama MAPUNDA



Kagera
Kagera ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu ,jamaa akawa ananijua japo simjui akajitambulisha kuwa yuko bunda walihitaji msaada wa madawa flani yako biharamulo na MZEE flani yuko pale , aliongea mengi na kumiunganisha na mzungu anayetokea SA , nilichomjibu ni simple tu , OK Niko tayari ila Mimi Niko bukoba mjini sina nauli ya kwenda biharamulo nitumie nauli nikufanyie Kazi yako na sihitaji commission yoyote

Jamaa akasema tumia pesa yako , nikamjibu hiyo sio plan wala dili langu ni lako ,

Jamaa alikata simu , ila lafudhi ilikuwa ya kichaga
 
Huo mchezo upo sana hata huku Zenj wanaokea sana.
Tatizo hata ukienda TCRA hakuna msaada wowote ndio maana wanaendelea.
 
Ukilegea wanakupiga jamaa ni wabaya sana, hata ukionana naye unatakiwa uwe na bastola akileta shita unamshoot hapo hapo.
 
Hivi mtu hueezo ku comment mpk u quote uzi mrefu hivi!?
Mnatuchosha
 
Ukiwa na tamaa ya kupata hela nyingi kwa ghafla au kuamini mambo ya ushirikina lazima utatapeliwa.

Jana nilipokea sms ifuatayo kutoka kwa namba ya mtu nisiyemjua:
"Kaka ahsante sana kwa mganga uliyetuletea. Kwa sasa hivi baba hali yake inaendelea vizuri kabisa hadi tunashindwa kuamini kama baba ndiye yule aliyekuwa ameugua kiasi kile. Hata vile vifaa vyetu vilivyokuwa vimeibiwa nyumbani tumeshangaa tulipoamka asubuhi ya leo tumevikuta vimerudishwa mlangoni kwetu na wezi na vyote vikiwa vimetimia. Hakika duniani kuwa watu wana madawa....". Nikajua anakotaka kunipeleka. Niliyomwandikia siwezi kuyaandika hapa lakini hakurudia tena kuniandikia.
Haaahaaaa

Nimepata msj km hii hii!

Niliwaambia nina damu ya Yesu!
Kimya hawakuendelea!
 
Nimewahi kutapeliwa laki 3 mwaka 2010 hivyo huwa nipo macho sana.
Baba angu alitapeliwa 1mil kwa styl km hii kuna deal alifanya kimyakima bila kumshirikisha mama! Ilipobuma ndo kajieleza kwa mkewe!

Alijuta!
 
Mimi aliwahi kuniambia anaitwa Mr. Mkwawa. aliniambia kuna mzigo wa dawa za mifugo nikauchukue kwa Dr yuko wizara ya mifugo alinitajia hela ndefu kama m48 hivi. Wakati ananipa maelezo nilishahisi huo mchezo. Nikamwambia kuna kaka yangu pale Wizarani ngoja nimwambie afanye hilo deal. Soon akakata simu. Nilipompigia tena alijifanya hakumbuki lolote
Hii ndo baba angu aliingia mkenge coz yy ni dr pia,akaona bonge la dili!
 
Hawa jamaa nahisi ni wasomi wasio na ajira. Wanazotumia very psychological techniques ambazo kwa mtu wa kawaida hawezi apply! Mi waliniingia na dili la vinyago arusha nikachomoa!!
 
Hii ndo baba angu aliingia mkenge coz yy ni dr pia,akaona bonge la dili!
Pole yake kwa kweli. Mimi namba zangu najua walizipata magazetini kwenye columns zangu ninazochangia so haikuniwia ngumu kutambua mchezo wake. And besides mimi si muumini wa shortcuts kwenye utafutaji wa kipato
 
Kuna jamaa yangu yeye katumiwa meseji kama hiyo leo. Akampigia jamaa anataka atumiwe laki 3 na 50 ili amfanyie mpango wa kupata hiyo kazi.
 
Hawa jamaa ni hatari.Mimi walinipigia nikabaki nacheka.Eti mtu anakwambia anamjua muuza viatu vya shanga na batiki.Halafu ya hivyo vitu bei yake anajua.Anataka umpigie muuzaji ubargain bei aliyokupangia.Kuna mzungu anatoka ngorongoro atavichukua Kia kwenda navyo ng'ambo.Yaani ni full comedy.Usipokuwa mjanja unaliwa.
Yaani nilifanyiwa hivihivi Mara mashuka ya Masai Mara watalii sina hamu nashukuru mungu nilishtuka.
 
Yaani nilifanyiwa hivihivi Mara mashuka ya Masai Mara watalii sina hamu nashukuru mungu nilishtuka.
Sasa hivi wamekuja na mpya dawa za mifugo kupeleka loliondo.Watanzania tuwe makini no free lunch.
 
TCRA nayo ni bure kabisa
Wala siyo TCRA wa kulaumiwa mkuu, sasa hivi mtu anaweza kubuni namba yoyote akajaribu kutuma pesa anapata jina lako. Anaweza kwenda kwenye mitandao ya kijamii kama facebook akapata detail zako. Au anaweza hata kutumia True Caller kukutambua na hata kujua sehemu uliyopo.
 
Back
Top Bottom