Tahadhari kwa namba hizi

Tahadhari kwa namba hizi

Hongera mkuu kwa kuruka nami washanipigiaga kutaka kufanya biashara ya vinyago na utalii pia, nilijiuliza sana wamejuaje najishughulisha na utalii kiujumla waknitajia hadi ninapoishi nikajua ni ishu ya maana ilikuwa kama ya milioni8 hivi ya fasta ila waliponiambia niwatumie hela ya Malipo ya dhl kwanza ili nikifika ishu iwe tayari hapo nikaanza kuwa na wasiwasi na nikajua ni matapeli nikaachana nao wakapiga simu had wakatulia wenyewe
Maswali niliyojiuliza
1.wamenijuaje majina yangu yote matatu?
2.plate no ya gari zangu mbili?
3.mahali ninapoishi
4.muonekano wangu
5.sehemu ninazopendelea
Kwa sababu vitu vyote hivo tapeli hilo lilinitajia ingiwa lenyewe linasema lipo serengeti na watalii nilijua ni mtu tunayefahamina nae ila kila nikiviluta picha simpati tuweni makini sana ndugu zangu

Ila hivi kweli serikali haiwezi kuwabaini mijitu haua au tcra washirikiane na matandao ya simu.
 
Wakuu heshima zenu

Tahadhari kwa hizi namba tajwa hapo juu.

Siku ya Jumatano tarehe 19/10/2016 saa 3 asubuhi alinipigia bwana mmoja anajiita Samweli (0787-332977) akanitaja kwa jina nilosajili kwenye line yangu ya airtel na kuniuliza leo hujaenda kazini? Nikajibu ndiyo nipo home, akasema mimi naitwa Samweli(Mkurungezi wa kampuni nipo Dodoma) naomba uende AICC Hospital utamkuta Dr Shabani(0689-694153) mwambie Samweli ameniomba nisimamie mzigo wake wa dawa boxes 40 akataja jina gumu la dawa silikumbuki vizuri kila box shilingi 400,000 x 40 = 16,000,000.

Kuna mzungu anatokea KIA nakutumia no yake mara moja atakupigia mwambie wewe ni mwakilishi wa Kampuni na atakukabidhi million 24 cash, million 16 utalipa AICC na million 8 ni faida tutagawana mimi, mhasibu wangu na wewe, nikamjibu sawa. Baada ya muda mfupi akanipigia huyo Shabani A.K.A dr akaniuliza wewe ndiyo mwakilishi wa Samweli? Nikamjibu ndiyo. Mwambie wakaguzi wa TRA wanataka 480,000 cash bila mhuri wa TRA mzungu atakataa, nikamjibu kuwa ongea naye mimi nimeambiwa kusimamia kupaki mzigo (alipotaja hiyo hela nikaanza kushituka kuwa hapa kuna jambo). Baada ya muda Samweli akapiga cm akaniambia nimeongea na dr anataka 480,000 cash, akajifanya analalamika vibaya sana nikamwambia million 8 kutoa lakini 480,000 baki 7,520,000 mbona ni faida kubwa sana? Akasema isiwe tabu hapa mfukoni nina 280,000 naomba uniongezee laki 2 nikamwambia isiwe tatizo tuma hiyo 280,000 kwenye airtel money yangu nitaongezea hiyo laki 2 akasema sawa.

Baada ya kama dak 5 Shaban (dr) akapiga akasema Samweli amenitumia 280,000 amesema laki 2 unatoa wewe nikamjibu ni kweli natoa mimi lakini nipe dak 20 tu, baada ya dak 15 nikampigia nikamwambia nipo hapa getini japo sikuwa getini njoo unipokee au nielekeze ofisini kwako nipo na hela. Akasema ukiingia mlinzi atashituka nikamjibu mbona watu wengi wanaingia hashituki kwani anajua nakuja kufanya nini na wakati mimi nakuja kuonana na dr wangu? Wewe tuma kwenye simu nikamwambia poa ngoja niende airtel money town, Arusha airtel money ni za shida nyingi ni m-pesa akaniambia fanya haraka naandaa mzigo nije nao hotelini atapofikia mzungu na mhasibu wenu. Baada ya dak kama 5 mzungu feki(0787-407501) akapiga akaniambia anapata supu karibu na Golden Rose wapo na mhasibu wa kampuni lakini anavyoongea kimombo nikajua huyu ni tapeli, nikamwambia nakuja hapo nikufuate akakataa akasema anatafuta hoteli ya kulala na kupokelea mzigo.

Baada ya muda kidogo akanipigia Samweli (mkurugenzi feki) akaniuliza unafanya kazi gani? Nikamwambia nipo Monduli kambini akakata simu nikapiga hakupokea tena mpaka leo.

Hawajamaa ni matapeli wazoefu ukikurupuka unaenda na maji, maswali nilijiuliza inakuwaje mtu ambaye unamjua umuulize unafanya kazi gani? Kama wewe ni mkurugenzi wa kampuni dr anashindwaje kukuamini 480,000 wakati mnafanya biashara ya mamilioni? Maswali ni mengi sana siwezi kuandika yote.

Hawajamaa wamesajili majina yale ambayo wanayatumia kutapeli lakini ukituma pesa hutakaa uwapate na wanaomba hela kidogo iliusishituke. Tuwe makini jamani nimeona ni wafahamishe msije mkatapeliwa na sijui na wanazitoa wapi no za simu za watu pamoja na kutaja eneo ulipo, kama hawashirikiani na watu wa customer care basi wanashirikiana na watu wa karibu yako.

Tusikimbilie hela za haraka unaweza kutapeliwa kirahisi sana.

Nilichelewa kuirusha/post kutokana kuwa na majukumu mengine nilikuwa sijapata muda wa kuichapa.

Jamani mimi siyo mwandishi wa habari kwa hiyo mapungufu mtanisamehe japo lengo langu ni tahadhari kwa wadau wasijitapeliwa.

Asanteni.
dah hiyo kitu hata Mimi ilinipata sema Mimi nilikwambia live kuwa ww ni tapel wanajifanya ni wataalamu wa dawa za maji na mambo ya visima .
 
betting za vo*a nao ni utapeli! kila siku sms...!eti milion 5.Nasikia watu wanaliwa sana 300 zao kila siku!!!
 
Ukiwa na tamaa ya kupata hela nyingi kwa ghafla au kuamini mambo ya ushirikina lazima utatapeliwa.

Jana nilipokea sms ifuatayo kutoka kwa namba ya mtu nisiyemjua:
"Kaka ahsante sana kwa mganga uliyetuletea. Kwa sasa hivi baba hali yake inaendelea vizuri kabisa hadi tunashindwa kuamini kama baba ndiye yule aliyekuwa ameugua kiasi kile. Hata vile vifaa vyetu vilivyokuwa vimeibiwa nyumbani tumeshangaa tulipoamka asubuhi ya leo tumevikuta vimerudishwa mlangoni kwetu na wezi na vyote vikiwa vimetimia. Hakika duniani kuwa watu wana madawa....". Nikajua anakotaka kunipeleka. Niliyomwandikia siwezi kuyaandika hapa lakini hakurudia tena kuniandikia.
Mkuu umenichekesha sana, hiyo message hata mimi nilitumiwa
 
Mi nlipokea meseji hii KAKA NASHUKURU SANA TENA SANA BABA KAPONA KABISA. KWA MTAALUMU WAKO ULIYENILETEA. WALE WEZI TUMEWAKUTA GETINI.

Nikamwambia acha ufala
Mimi nilipata hiyo sms, then nikaipuuza nikidhani ni mtu amekosea pa kuituma
 
Hawa matapeli ni hatari sana 2010 alikuja tapeli mmoja pale CBE Dsm akatulipia mpaka nauli kwenda Bandarini, kweli tukaenda wawili nikashituka anataka hela kwanza mwenzagu akaniambia huyu jamaa anatokea Shinyanga hawezi kututapeli ilikuwa mzigo wa 800,000 na kweli nilikuwa nazo hizo hela ila jamaa ambaye nilikuwa nasomanaye hakuwa na kitu, nikampa 260,000 wakaingia ndani nikawa nampigia cm namwambia usimkabidhi hela mpaka uchukue mzigo baada ya dak kama 10 akatoka analia amevua shati nikamuuliza vipi akasema tayari jamaa amenipiga, nikamwambia anilipe hiyo hela baada ya shimo la HESLB kutema akalipa kama 150,000 zingine nikasamehe. Ndiyo maana huwa nipo makini sana na huu utajiri wa haraka.
 
Tatizo watanzania tunapenda utajiri wa haraka sana ndiyo maana hawa jamaa wanatumia hiyo weakness kututapeli kirahi, siku hiyo nilitaka nione mwisho wake nini ndiyo maana nilikuwa natoa ushirikiano ili hata ndugu yangu asikuingizwa chaka.
 
Ukiwa na tamaa ya kupata hela nyingi kwa ghafla au kuamini mambo ya ushirikina lazima utatapeliwa.

Jana nilipokea sms ifuatayo kutoka kwa namba ya mtu nisiyemjua:
"Kaka ahsante sana kwa mganga uliyetuletea. Kwa sasa hivi baba hali yake inaendelea vizuri kabisa hadi tunashindwa kuamini kama baba ndiye yule aliyekuwa ameugua kiasi kile. Hata vile vifaa vyetu vilivyokuwa vimeibiwa nyumbani tumeshangaa tulipoamka asubuhi ya leo tumevikuta vimerudishwa mlangoni kwetu na wezi na vyote vikiwa vimetimia. Hakika duniani kuwa watu wana madawa....". Nikajua anakotaka kunipeleka. Niliyomwandikia siwezi kuyaandika hapa lakini hakurudia tena kuniandikia.
Hahaaaaaaaaa niliwah tumiwa hyo ....yan jibu moja tu nahis aliniblock kabisa
 
Hawa jamaa ni hatari.Mimi walinipigia nikabaki nacheka.Eti mtu anakwambia anamjua muuza viatu vya shanga na batiki.Halafu ya hivyo vitu bei yake anajua.Anataka umpigie muuzaji ubargain bei aliyokupangia.Kuna mzungu anatoka ngorongoro atavichukua Kia kwenda navyo ng'ambo.Yaani ni full comedy.Usipokuwa mjanja unaliwa.
Daaah kama mm ilinitokea story kama hii ya viatu vya shanga mchina anavitaka wapo kiwanda cha dangote ile yy kanipa nipa namba ya muuzaji viatu anakaa kigamboni nipange nae bei yaan sie tuzidishe hela ss hiyo hela tuliozidisha unanunua gari na nyumba
 
Hao wameshanipigia sana cha ajabu wakakutana na sensor. Utapeli wao ni wamiaka ileeeeee 1800's. We wajibu nakuja mlipo tuongee vzr. Ukiwa na tamaa watakukula
 
Mkuu kassimneema siyo wote wanaweza kuruka mtego unashangaa umempa mdogo wako karo anapiga hesabu ya kupata fedha nyingi.
 
Tufanyaje ilikuondoa huu utapeli? tuliambia tusajili line lakini naona tatizo ndiyo linazidi kuwa kubwa sana.
 
Wangempigia Scorpion kabla hajaenda rumande waone kazi yake shenzi kabisa hao!
 
Kweli utapeli sijui wanatumia akili za kijinga kiasi gani.
Mimi niliamka siku moja nikakuta msg.
"Shost mambo, asante shogayangu kwa yule mtaalamu maana mambo yangu yameninyookea kila kitu nikiiambia hii pete napata, account zangu zinasoma hela ndefu hivi najiandaa kwenda dubai kufuata mzigo. Kumbe yule mganga hawamsifii bure eh?"
Nilichomjibu ni "nakutakia utajiri mwema, nyau wewe "
Kwani alijibu tena.
 
Mkuu kassimneema siyo wote wanaweza kuruka mtego unashangaa umempa mdogo wako karo anapiga hesabu ya kupata fedha nyingi.
Nyingine ...nilipigiwa kwel nina kampun ya usafi wakanipa dil la kufanya fumigation ktk kituo cha watt yatima kiko kigambon na bagamoyo malipo mazur tu ,,, tender ya miaka miwili nikamwambia tukutane tukakutana holiday inn alisema wanamkutana pale ....hakuniomba hela ila aninitengeneza poa sana basi nikarud ofusin baadae anasema kampun yako imepitishwa so umefanikiwa kupata tenda mana najua mm nitapata chochote kitu kutoka kwako...so tuma laki moja ya kuandaa tender document kabla ya saa kum jion tuipitishe fasta jumatatu kazi ianze nikamjibu poa ... Sasa nilikuwa sijafika mbal ngoja nikuletee hapo toka nje basi ....kumbe niko zangu na mishe nyingine dk.kum nikapiga simu niko nje akajib nakuja ..lisaaa nikampigia mbona hautok kaka njoo basi ohh nimebanwa na kikao tuma tu hapo nje si kuna tgo pesa?? Nikamwambia nakungoja mana alisema n kama nusu saa atamaliza kikao ...mpka saa kum na mbil napiga simu akasema WEWE DADA UMETUMWA NN ENDELEA NA SHUHUL ZAKO ....UNABAHATI ....AKAKATA SIMU ,,MSG NILOMTUMIA ZILE NO MPKA LEO HAZIPATIKAN ZOTE
.
 
Back
Top Bottom