Tahadhari kwa namba hizi

Tahadhari kwa namba hizi

Ukiwa na tamaa ya kupata hela nyingi kwa ghafla au kuamini mambo ya ushirikina lazima utatapeliwa.

Jana nilipokea sms ifuatayo kutoka kwa namba ya mtu nisiyemjua:
"Kaka ahsante sana kwa mganga uliyetuletea. Kwa sasa hivi baba hali yake inaendelea vizuri kabisa hadi tunashindwa kuamini kama baba ndiye yule aliyekuwa ameugua kiasi kile. Hata vile vifaa vyetu vilivyokuwa vimeibiwa nyumbani tumeshangaa tulipoamka asubuhi ya leo tumevikuta vimerudishwa mlangoni kwetu na wezi na vyote vikiwa vimetimia. Hakika duniani kuwa watu wana madawa....". Nikajua anakotaka kunipeleka. Niliyomwandikia siwezi kuyaandika hapa lakini hakurudia tena kuniandikia.
Aisee wewe mzee Sure Boy nini?? maana juzi nilikuwa nae akanionesha sms kama hiyo nikamwambia usipoteze ata mda kumjibu huyo ni TAPELI.
 
Pia kuna utapeli kupitia minada ya vitu vya electronics
Watu wanauziwa vitu kwa bei rahisi lakini huwa ni vibovu,na unapewa risiti ikiwa na jina feki la Auction Mart fulani,risiti haina contacts za hiyo kampuni wala chochote pia nahc TIN no huwa ni za kubuni pia.
Mimi nilitapelewa kama 160k kama pesa ya manunuzi ya PC but nilipoenda Police kutoa taarifa wakanipotezea tyu.Nahic kuna mkono wao labda!
"!!Tuweni Makini!!"
 
Na wewe una moyo! Muda wote unahangaika nao badala uwapotezee pale walipotaka pesa?
 
Mimi nimeshawwhi pigiwa mara 5 lakini zote nilizipuuza..
1. Nilishawahi kufanya PT pale K1 kilombero sugar... baada ya kupita miaka kadha mtu ananipigia kwamba yupo huko na kuna sukari ya deal ailete Dar mimi niipokee. Eti nitume nauli ya mzigo... NIKAMWAMBIA HUJANIPATA BADO
2. Nilipigiwa na namba kwamba mwenyewe yupo mtwara. Kuna biashara ya spea za matrekta ya kubota. Kataja baa ninayokataga kiu yangu kwamba ananifahamia hapo. Akataja na watoto wangu.a ninapoishi... Nikapuuza
3. Ninapokunywaga supu jamaa wa supu akaibiwa simu. Wezi walichofanya ni kuandika sms ya kuomba hela kwenye namba zote zilizopo kwenye phonebook. Nikawaambia kama wewe ni yule ninayemfahamu, mwambie mwenzio mnayekuwa naye pamoja anipigie. La sivyo mambo ya mjini hayo.. nikaapuuzia
4. Jamaa nilikuwa nafanya naye kazi Celtel enzi hizo, akaibiwa simu then mwizi akaandika sms moja kwa wote walioko kwenye phonebook. Tuliohamia sehemu moja tukapata sms hiyo. TUKAPUUZIA
5. Niliandikiwa sms eti niende Muhimbili kwenye interview.... cha ajabu
- Sikuwahi omba kazi huko
- Kazi niliyoitiwa haikuwa ya profesional yangu
- Kazi niliyoitwa kuifanyia interview ilikuwa chini ya education level yangu
- Siku ya interview ilikuwa Jumapili wakati ni ofisi za serikali
 
Haya matukio yanaonekana kushamiri mwezi uliopita nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha anafanyia kazi kampuni moja ya simu makao makuu akinieleza namba yangu imeshinda zawadi ..... alipoona sielekei mwelekeo wa kutapeliwa alikata simu.
 
Walishanipigia na mimi na huwa na enjoy to play along, na mode yao ni hiyo hiyo mkurugenzi, dokta, mzungu, madawa kind of these settings. Ila mimi nilibahatika kupata elfu kumi ya bando.., niliambiwa nitume laki tatu au nne kama sikosei, like three years ago, nikajidai kumwambia nimehamisha hela zote bank na imepungua elfu kumi, jamaa akanirushia elfu kumi ili nitume, nikanunua bando, nikamtext text ya bando na kumwambia nitamreport police kwa kutaka kutapeli.
 
Hahahaa custrine food product. Inahitajika kuhifadhia chakula cha wakimbizi kigoma mzungu yuko zamani kempnsk hotel kila chupa ni dolar 1500 zinatakiwa chupa 1000 kwa kuanzia.!!!
Dadeeki. Hawa wajinga wanawapiga sana watu wanaopenda issue za udalali..
Mpya nimeisikia juzi wanajifanya ni watumishi wa serikali walio katika kitengo cha kuhakiki vyeti. Na wanahitaji pesa ili wakusaidie kwenye kuokoa ajira yako. Wanawapiga sana walimu sasa hivi.
 
0656364789 Kwenye hiyo orodha ongeza na hii. Jamaa anajiita Komba ni hatari kwa utapeli kama ukoma. Anatumia gia ya kusambaza dawa
 
Hawa jamaa ni hatari.Mimi walinipigia nikabaki nacheka.Eti mtu anakwambia anamjua muuza viatu vya shanga na batiki.Halafu ya hivyo vitu bei yake anajua.Anataka umpigie muuzaji ubargain bei aliyokupangia.Kuna mzungu anatoka ngorongoro atavichukua Kia kwenda navyo ng'ambo.Yaani ni full comedy.Usipokuwa mjanja unaliwa.
Lakini mimi nilishaapa siku moja nitakuja kula hela ya tapeli.
Sababu wana-formula ya kutapelia kwa muda flani. Ikibuma wote kwa pamoja wanahamia formula nyingine!
Hii ya mzungu kuendelea kutapelia, haijakaa vizuri, kwa mjanja yeyote ni rahisi sana kuigundua.
Kuna hizi hela za chambo kwa ajili ya kuopolea mzigo ndohizo huwa nasema maranyingi kwamba ole wao!
Ingawa ni maranyingi sana nimewakosakosa, wakapitia tundu la sindano kusevia.
Siku1 waliingiza kiasi cha sh.4,000,000/= cash kwenye account yangu na wakanipigia cm kuniulizia kama hiyo cash nimeipata.
Nilivyo na kawaida kabla ya mjadala wowote lazima nihamishe salio lote kwenda account nyingine na kuitoa muda huohuo. Kama mtu katuma kimakosa hulazimu kumrejeshea baadae baada ya kujiridhisha.
Ss waliponiuliza nikwaambia subiri kdogo ntakujibu.
Nikaingia kwenye acct kuuliza salio nikaona cash mil.4. Nikaicommand ihamie kwenye acct nyingine ikagoma, ikidai salio halitoshelezi.
Tayari nikajua kwamba nipo kwenye ligi, mchezo wa kutafuta ubingwa!
Nikawapigia nikawaeleza kuwa nimekiona hicho kiasi nani kanitumia? Wakanitajia jamaa nisiye mfahamu na kunielekeza nimpigie kupata maelekezo. Lakini kabla ya kumpigia wakanitahadharisha, nimwamkie kwa lugha ya kinyenyekevu nikianza na shikamoo, maana ni mtu mzito na wa makamo.
Mtu huyo nilipompigia akanieleza fedhahizo zimeingizwa na boss wangu wangu ambae zamani tulikuwanae kazini. Na kwamba hizo pesa nisizichukue hadi Kwamba kanitumia hizo hela ili nimkopeshe kwa kumuongezea milioni2 kwa ajili ya kununulia uwanja maeneo ya mjini. Na kwakuwa mimi ni mwenyeji nimsaidie, kwenda hilo eneo na mil.6.
Nikawauliza kwa kutumia authentication kila swali. Nikagundua hawana lolote wanalolielewa kwangu ama kwa huyo boss wangu.
Nikawaambia kuwa tuonane popote wanapotaka wao ama waje nyumbani "kupopoa" hizo hela ambazo boss wangu kahitaji.
Ni hadithi ndefu. Lakini mara nyingi wanaoliwa huwa wanaaminishwa kupata faida maradufu ya fedha watakazotoa wao. Ni mbinu za kizamani. Ukiingiwa tamaa, lazima uliwe.
 
Story nzima nimepapenda hapo alipokuuliza unafanya kazi wapi ukamjibu uko Monduli kambini naamini atakuwa amechanganya akili zake akapata majibu ya kifuatacho ndiomaana hajakutafuta tena....Monduli si mchezo
 
Back
Top Bottom