Mshobaa
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 1,716
- 680
Heshima na utii zije kwenu wanajf wote: Kuna huyu dada alini inbox kwenye facebook na kunipa Email yake kisha akaniomba nimpatie mail yangu na bila hiana nikampatia baada ya hapo akaanza kunitumia jumbe mbalimbali akisema yupo Dakar Senegal nikawa naendelea kufuatilia ili nijue dhumuni lake,alinipa historia ya maisha yake ambayo ni ya kusikitisha flani hivi ili aniteke ki saikolojia kiukweli alinitumia ujumbe mrefu sana ambao kwa kuuangalia unaonekana kabisa umeandaliwa maalumu kwa kazi hiyo ya ki haini uliojaa kila aina ya stori na mwishowe ndipo nilipostukia ukiwa na nafasi za kujaza kwa ajili ya kutransfer money akidai nimtajie bank ninayotumia, jina kamili na mengineyo mengi kwa kweli huyu tapeli anayejiita kwa jina la Elizabeth Elizabeth kajipanga. Naomba nitoe rai kwenu ndugu zangu na watanzania kwa ujumla muwe makini sana na huyu tapeli hafai hata kidogo.Nawasilisha wakuu