Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,655
- 729,714
Ndugu zangu hamkani si shwari tena...you are being watched n monitored!take care
Uhuru wa kupashana habari umeingia kitanzini... mitandao ya kijamii imebanwa mbavu.... mada nyingi zenye kukosoa utendaji hazidumu tena popote
Kamatakamata ya kimyakimya inaendelea....kama wewe ni mpenzi na mkereketwa wa siasa za upinzani..badili mtazamo wako sasa...kimenuka na kumenuka
Tunarudi kwenye zama za kuongelea chini ya zulia kunong'ona na kunong'onezana utafikiri mahaba ya wizi
Tunarudi kwenye zama za kuangalia kushoto na kulia mbele na nyuma juu na chini kabla hatujaongea dukuduku
Ni kama maji yenye kina kirefu sana..yametulia tuli lakini Usijaribu kuingia....!tutakupoteza mara
Kuna jicho kali katili kizani LIOGOPE...! Tena liogope hasa..koleo na bisibisi vipo tena vipo sana na vimekolezwa makali...! Lala ukijua hilo amka ukitafakari
Nilisema na naomba niseme tena wakimaliza juu wakimaliza katikati watakuja chini....hawako mbali sasa...hawaonekani kwa macho lakini mvumo wao unasikika...JIHADHARI
Where we dare to talk openly inaelekea kubaki story zinaumiza sana hizi hisia... tunaupa mwanga kisogo na kulikabili giza linaloogofya...! Giza lenye macho makali na masikio marefu
Wakati utaamua...! Wakati utasema...! Lakini kwasasa vuta handbrake...! You are being watched n monitored