Tafuta hela uoe mke mzuri

Webb

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
425
883
Wakuu hii kauli nilikua nikiambiwa na marehem baba. Hivi ina maana gani, kwa sababu alikua akinambia kipindi nasoma na mimi nilikua nachukulia kawaida sana

Na hata mtaani uwa naiskia sana.Hivi ela na mke mzuri vinaendana vipi?
 
r.i.p baba yako! kuna mke mzuri kwa tabia huyu yeye na pesa sio sababu ya mapenzi yake kwako,yeye yupo kwa sababu wewe upo.( huyu anaweza kuwa mzuri pia kwa muonekano au asiwe) Hapa baba ako alimaanisha utafute Pesa ili umtimizie mahitaji huyu bibiena familia yako kwa ujumla maana ndio WAJIBI.

Kuna huyu mwingine ni mzuri wa KIMUONEKANO ( hapa nazungumzia yale mambo yako unayoyapenda kwa mwanamke achilia mbali tabia zake,hapa nazungumzia chura,modo,white au black)Hapa baba ako alimaanisha utafute pesa ili uweze kumiliki wanawake kama hao,na ukifahamu fika siku utayakosa pesa basi utapigiwa ,na inawezekana kupigiwa ata ukiwa na izo pesa,maana mara nyingi nao hupenda vifua,anayejua kuvaa na swaga kwa ujumla,vitu ambavyo wewe hutakuwa na muda navyo maana wewe ni busy kutafuta pesa.
 
Swala la mapenzi wakati mwingine halina kabisa uhusiano na pesa japo ni kweli pesa urahisisha mambo mengi na kufanya mapenzi yazidi kuwa mazuri hasa kwa wanawake wa material things.. Hela hizo hizo ukiwa nazo badala ya kumtuliza mkeo ndo zitatumika kuwahonga Vijana (serengeti boys) kwa jina maarufu.
 
Ni kwa kuwa ukikosa hela utatorokwa
Katorokwa Marehemu Ivan The Don na hela zake.

Katorokwa Bilionea wa dola Ted Turner.

Kuna bendi 9Nafikiri Sikinde ya Chidumule ile) iliimba wimbo

"Usitumie peesa, kama fimbo baba, mambo ya pesa hutakamakubaliano, hapo ndipo pesa huwa na thamani ee".

Mnapoweka pesa mbele mkumbuke ushauri maridhawa wa wimbo huu.
 
Mbona havina uhusiano?
Au unamaaniza uzuri gani?
Kuna uzuri wa tabia, uzuri wa muonekano (kuna uzuri asili na wa kununua)
 
Aliona mwanae anapote, anapenda wanawake wazuri ila hapigi kaz , akacheza na saikolojia. Shida yake ufanikiwe sio wanawake km unavyofikiria Fungua akili mkuu. alaaaaaa........
 
Back
Top Bottom