Tafsiri ya kauli za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa; Tanzania kama nuru ya amani, umoja na usalama duniani

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
894
Reaction score
994
TAFSIRI YA KAULI ZA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA: TANZANIA KAMA NURU YA AMANI, UMOJA NA USALAMA DUNIANI

Na GULATONE MASIGA

Kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. António Guterres, wakati akipokea ujumbe maalum wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan uliowasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje Mhe Mahamud Thabit Kombo amesema kwamba Tanzania imekuwa rejea muhimu ya amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani, si kauli ya kawaida wala ya kiitikadi.

Ni tathmini ya kina kutoka kwa taasisi ya juu zaidi ya kimataifa inayohusika na amani, usalama na mahusiano ya kimataifa. Kwa Mtanzania wa kawaida, kauli hii inabeba ujumbe mzito kuhusu hadhi ya Taifa letu mbele ya dunia.

Kwa miongo kadhaa, Tanzania imejijengea sifa ya kipekee kama nchi yenye umoja wa kitaifa, amani ya kudumu na mshikamano wa kijamii unaovuka mipaka ya dini, kabila, itikadi za kisiasa na tofauti za kiuchumi.

Hii ndiyo misingi iliyowezesha Tanzania kuepuka migogoro ya ndani iliyozikumba nchi nyingi katika kanda na barani Afrika kwa ujumla. Kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inathibitisha kuwa dunia inaitambua na kuithamini Tanzania kama nguzo ya utulivu wa kikanda na kimataifa.

Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025, kama alivyoainisha Bw. Guterres, ulikuwa jaribio kubwa kwa hadhi hiyo ya amani. Katika mazingira ambayo siasa za dunia zimejaa migawanyiko, misuguano na wakati mwingine vurugu, Tanzania ilipitia kipindi hicho nyeti bila kuyumbisha misingi ya Taifa.

Uwezo wa nchi “kuvuka salama jaribio hilo” unaonesha uimara wa taasisi zake, busara ya uongozi wake na ukomavu wa wananchi wake katika kulinda amani yao.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutamani kuona Tanzania ikiendelea kubaki na umoja huo na kuwa mfano bora kwa mataifa mengine una maana pana zaidi. Kimsingi, Umoja wa Mataifa unaitazama Tanzania si kama mnufaika tu wa amani, bali kama mwalimu wa amani kwa dunia.

Hii inaweka wajibu mkubwa kwa viongozi, vyama vya siasa, asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kuwa tofauti za kisiasa au kijamii hazigeuki kuwa tishio kwa mshikamano wa Taifa, amani na utulivu.

Ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kutoa msaada kamili katika mchakato wa Tume ya Uchunguzi ni ishara ya imani kwa utawala wa sheria na uwajibikaji nchini Tanzania.

Inadhihirisha kuwa amani ya kweli haijengwi kwa kuficha changamoto, bali kwa kuzitambua, kuzichambua na kuzitatua kwa uwazi na haki. Huu ni ujumbe muhimu kwa Watanzania kwamba kulinda amani kunakwenda sambamba na kujenga mifumo imara ya haki, maridhiano na mazungumzo ya kitaifa jumuishi kama anavyohimiza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Kwa tafsiri pana, kauli za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa zinawaambia Watanzania jambo moja la msingi kuwa dunia inaangalia Tanzania kama hazina ya amani.

Hadhi hii si ya kupewa kwa maneno tu, bali ni dhamana inayopaswa kulindwa kila siku kwa vitendo. Amani, umoja, utulivu na usalama wa Taifa si mali ya serikali pekee, bali ni jukumu la kila Mtanzania kuanzia kiongozi wa juu hadi mwananchi wa kawaida.

Kwa kuendelea kudumisha utamaduni wa mazungumzo, kuheshimiana na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele ya tofauti binafsi au za kisiasa, Tanzania itaendelea kuwa kile ambacho Umoja wa Mataifa inakitamani: Mfano hai wa nchi inayothibitisha kuwa amani inawezekana, umoja unawezekana, na usalama wa Taifa unaweza kujengwa kwa hekima na mshikamano wa watu wake.

Kwa Maoni Na Ushauri
0768497974

Pia soma > António Guterres: Tanzania imekuwa rejea na mfano wa kuigwa katika masuala ya amani na mshikamano wa kijamii Afrika na duniani
 
Attachments

  • IMG_4618.jpeg
    IMG_4618.jpeg
    607 KB · Views: 10
Una taarifa yeyote ya Trump aliyoitoa jana kama huna ngoja nikusogezee
 
..tatizo ni kwamba Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN hajatoa taarifa kuhusu mkutano wa Katibu Mkuu na Waziri Thabit Kombo.

..kilichoripotiwa mpaka sasa hivi ni taarifa ya Wizara yetu ya Mambo ya nje. Na upo uwezekano kwamba taarifa hiyo imetiwa chumvi. Ili tuweze kutoa tafsiri yenye uwiano kuhusu nini kimetokea tunapaswa kusubiri tupate na taarifa ya Msemaji wa Katibu Mkuu UN.
 
Back
Top Bottom