Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,230
Shirika la Vijana na Wanawake Tanzania (TAFEYOCO) limewataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu na kwa manufaa, ili kudumisha amani na utulivu kuelekea Uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais, huku likikemea vikali watu wote wanaojihusisha na vitendo au kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kusababisha machafuko na hata vita nchini.