Bulaya001
JF-Expert Member
- Dec 21, 2018
- 5,868
- 6,480
Michael Jackson alikuwa ni binadamu mwenye ndoto nyingi lakini Ndoto zake 2 kuu maishani zilikuwa ni:-
*1.* Kwanza ni kuwa mwanamziki mkubwa zaidi duniani wa Pop.
*2.* Kuishi miaka 150.
Baada ya kuifanikisha ndoto yake ya kwanza kwa ufanisi mkubwa aliamua kuanza kuwekeza kwenye ndoto yake ya pili ambayo kwa wakati huo ilikuwa ndiyo takwa lake kubwa
Ili aweze kuishi miaka 150 (Karne moja na nusu) aliamua kufanya mambo yafuatayo:-
*1* . Aliajiri madaktari binafsi 12 wa kumchunguza mwili wake wote hadi nywele na kucha kila siku.
*2.* Ilikuwa ni lazima chakula chake kipitie maabala kupimwa kabla hajala.
*3* . Wataalamu 15 aliwaajiri kufuatilia mazoezi,kazi na kila jambo alilofanya kila siku
*3* . Alitengeneza kitanda maalumu kilichokuwa na uwezo wa kufanya regulation ya hewa (oxygen)
*4.* Watu 50 waliwekwa tayari kujitolea viungo vyao kama angepata dharula yoyote. Aliwalisha, aliwatunza na kuwalipa mshahara kila siku kwa kazi hiyo.
Sasa alikuwa na uhakika wa kuishi karne moja na nusu bila mashaka yoyote lakini June 25, 2009 akiwa na miaka 50 moyo wake ulizima na ndoto yake ikawa imefika mwisho.Timu ya madaktari wake bingwa 12 haikuweza kuzuia pumzi yake isiondoke.
Pamoja na juhudi za madaktari wengine kutoka Calfornia na Los Angeles hawakuweza pia kuokoa maisha yake. Mtu ambaye kwa miaka 25 alikuwa hawezi kunyanyua unyayo wake bila ushauri na ruhusa ya daktari wake akawa kafika mwisho bila kutimiza ndoto yake ya kuishi miaka 150.
*Wewe na mimi tusio na uhakika wa kuhimili hata milo mitatu mwisho wetu ni upi?*
Safari ya mwisho ya Michael Jackson ilishuhudiwa moja kwa moja na zaidi ya watu milioni 3, Rekodi ambayo haijavunjwa hadi sasa. Siku aliyofariki mitandao mikubwa ya *wikipedia, twitter, AOL's instant messenger* ilielemewa na mzigo wa watumiaji waliokuwa wakisaka taarifa za kifo hiki hadi ikaacha kufanya kazi. *Google* pia ilivunja historia ya matumizi yake kwa siku ile.
Michael Jackson alitaka kupambana na kifo lakini hakuweza hata kufikia nusu ya umri aliopenda kuuishi.Uhai wetu upo mikononi mwa Mola Mlezi, yeye ndiye huutoa na ndiye auchukuaye milele.
Twamuomba Mungu wetu Mtukufu atujalie mwisho MWEMA, atuepushe na KIBURI na atujaze UPENDO kwa kila Binadamu.
Sent using Jamii Forums mobile app