Tafakuri ya Kikwete

Tafakuri ya Kikwete

Nchi ya kinafiki: zile kelele za jana kuhusu kuachiwa kwa Babu Seya na mwanae Papi Kocha zimefia wapi? What to expect from watu ambao umeme unakatika usiku, ukirejeshwa asubuhi wanashangilia na kusahau kabisa kuhusu tatizo hilo lililodumu zaidi ya miaka 10?
Katika kila jamii ulimwenguni hapakosekani kundi la bendera fuata upepo.. Wao si moto wala si baridi, ni vigeugeu na wana rangi za kinyonga hawana tofauti na popo
 
Katika kila jamii ulimwenguni hapakosekani kundi la bendera fuata upepo.. Wao si moto wala si baridi, ni vigeugeu na wana rangi za kinyonga hawana tofauti na popo
Aliyenisikitisha zaidi ni mwanasheria msomi Msando. Hivi haiwezekani kuhama chama bila kutoa maneno yasiyopendeza?
 
Mwenyekiti wenu ndio ana hali mbaya kupita maelezo kachanganyikiwa mpaka anajihusisha hadharani na walawiti.

Angejihifadhia utu kidogo.
hizi mboko anazowapiga Magu si za nji hii!

Mkuu usiumie sana, hata hivyo wewe endelea kusheherekea ujio wa kamanda mpya bwana nyalandu
 
Kikwete alikuwa na busara,mstahimilivu na muungwana. Ni wangapi wamepotea awamu hii bila miili yao kuonekana? Ni wangapi wamepigwa risasi kwa kuonesha udhaifu kwenye taasisi za serikali!? Ni wangapi wameuawa kwa kujeruhiwa na risasi za polisi kabla hawafikishwa mahakamani kutekeleza agizo lakunyang'anya silaha? Ni wangapi wako magerezani kwa kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa,kutoa maoni na kukutana?

Mdhaifu ni yule anayetumia nguvu pasipo busara na akili huku yeye akiwa baba wa familia. Akigawa familia kwa misingi ya kikanda, kidini,kisiasa na kiitikadi. Asiyejua nafasi yake kwa familia kwa kuficha ukweli na kutokuwa na uhakika na ukigeu geu kwa kile anachosema na kutenda. Wapi wenye vyeti feki!?Wakati Bashite analindwa huku kukiwa na tuhuma za wazi za kutumia cheti kisicho chake.
Wataje ukifikisha 10 waliopigwa risasi na kuuwawa na waliojeruhiwa na waliopotea ukijumlisha na waliotekwa awamu hii nakupa Jero ya vocha usitukane we shusha tu majina alafu reply me ntajua kweli upo serious acheni mambo ya kihuni fanyeni maisha mambo tafuteni maisha acheni siasa za vijiweni
 
hizi mboko anazowapiga Magu si za nji hii!

Mkuu usiumie sana, hata hivyo wewe endelea kusheherekea ujio wa kamanda mpya bwana nyalandu
Tumia akili kidogo utuambie babu seya anatakiwa na jamii ili aje kufanya nini hata apewe msamaha?

Anawachapa fimbo nyie mnaoenda kama kuku kakatwa kichwa.
 
Namnukuu Paskali.... "Kikwete alikuwa dhaifu sana ndio maana hakutaka wanyongwe.... " Sikubaliani kwa asilimia zote na Paskali.... Ni kweli JK alikuwa dhaifu!? Lenient! Lakini kwa ishu ya kunyongwa aliongozwa na tafakuri na mtazamo binafsi wenye kuacha maswali yenye majibu ya wazi kabisa...
Kikwete hakutokea porini mpaka kuupata urais hata Mkapa Mwinyi .... Ni watu waliokulia kwenye system, kwenye chama... Maisha yao kwa sehemu kubwa yalikuwa siasa... Walifanya siasa tangu wakiwa vijana.. Hawa hawakusukumiziwa urais, hawakuwa wanajaribu bali walikuwa ni wanasiasa walioiva...
Sipingani na hoja ya kuwanyonga waliokamatwa na madawa ya kulevya... Napingana na Paskali kwa kumuita JK dhaifu kwenye hili.... Mnyonge mnyongenj lakini haki yake mpeni....
Tafakuri ya kikwete kwa mtazamo wangu ni hii.... Hakutaka kutoa idhini ya kunyonga... Hii ni official hata kama PENGINE kwenye shughuli za kisiasa na uongozi wa nchi kuna watu walikufa kupitia yeye, lakini akikiangalia chama akiiangalia serikali aliona wazi kabisa kuna watu wabaya zaidi waliojificha kwenye koti la ngozi ya kondoo waliofanya mabaya zaidi kuliko hao vijana waliokamatwa ambao hata hivyo hawajui zaidi ya kutumika kama punda huku wazungu wa unga wenyewe wakiachwa salama salimini....
Tafakuri ya kikwete ni hii... Tazama kama yule kiongozi mkubwa kabisa ndani ya jumuiya ya chama aliyeaminiwa kutengeneza dawa za kupunguza makali ya ukimwi., lakini ndugu yule kwa kukosa UTU, kwa kukosa UZALENDO kwa kukosa HEKIMA, AKILI na WELEDI na ukizingatia analipwa pesa nzuri tu kwa kazi ile akaamua kutengeneza dawa bandia.. Huu ni zaidi ya uuaji, huu ni zaidi ya uhujumu uchumi.. Huu ni sawa na uhaini... Dawa zile zingeuzwa nje ya nchi na zikakamatwa tungeweka wapi nyuso zetu kama TAIFA? lakini Je dawa zile bandia zimeteketeza roho ngapi zilizokuwa na matumaini makubwa ya kupata nafuu huku wakiamini wanakunywa dawa sahihi?
Uuaji na ukatili huu mkubwa haujaonekana wameonekana vijana wetu, jiulize ndani ya chama na serikali kuna wenye madaraka wangapi wamefanya madudu ya kutisha yaliyoangamiza roho nyingi? Kikwete aliyafahamu yote haya... Kuacha kusaini hati ile ya kifo ilikuwa na maana yake kubwa sana nyuma ya pazia....!!!! Nampongeza Kikwete kwenye hili pamoja na udhaifu wake wote....
Miezi michache iliyopita kukawa na amsha amsha kubwa sana ya vita dhidi ya madawa ya kulevya... Vita ikaishia njiani kwa aibu kubwa baada ya kubainika kinara wa mapambano hayo alikuwa na agenda zake binafsi na alifaidika kwa hali na mali... Kama ni kitanzi kilipaswa kianzie kwa huyu bwana... Ile haikuwa vita bali geresha....!!!!
Paskali Kikwete hakutaka kunuka damu... Hakutaka kumwaga damu isiyo ha hatia.. Huku damu yenye hatia ikiendelea kutamba na kutamalaki....
Walioidhinishwa kunyongwa ni wa wa awamu zilizopita! Je awamu hii sisi hatuna????
Mkuu.. Well said.
 
Kwa kweli JK, ukimlinganisha na huyu was sasa, kwa hekima na busara, ni opposites! Mbali mbali kama mashariki na magharibi!

Acheni kupiga ramli. Mnahangaika kuwafananisha wakati wenyewe wanajua kila kitu kinachoendelea. Fanyeni kazi mpate pesa.
 
Wataje ukifikisha 10 waliopigwa risasi na kuuwawa na waliojeruhiwa na waliopotea ukijumlisha na waliotekwa awamu hii nakupa Jero ya vocha usitukane we shusha tu majina alafu reply me ntajua kweli upo serious acheni mambo ya kihuni fanyeni maisha mambo tafuteni maisha acheni siasa za vijiweni
Kwani mmekubaliana idadi ya mwisho iwe watu10..??? Hudhani kwamba HATA AKIWA MTU MMOJA, na upelelezi haufanyiki tayari ni tatizo..???
 
Back
Top Bottom