Tafakuri kuhusu Mikopo ya Elimu ya Juu

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
Isangula KG

Imekuwa kawaida yangu nipatapo fursa kidogo najaribu kutafakari mambo kadhaa yanayogusa Nchi yetu ama dunia kwa ujumla. Japo wasomaji wanaweza kujikuta wananufaika kwa busara hizi, kimsingi lengo kuu huwa ni *kutafakari kwa njia ya kujisemea mwenyewe* ama *talking to myself* kama sijakosea.Mara nyingi naandika mambo haya ninapokuwa safarini kukabili majukumu yangu ya kimaisha ama kwa kutembea ama katika vyombo vya usafiri. Leo pia najiongelesha habari za mikopo ya vyuo.

Nimeona taarifa kuwa sasa Bodi imefungua dirisha kwa wakopaji lakini jambo la kusikitisha ni kuona kwamba kigezo cha kutokupata mkopo ni mzazi kumiliki leseni ya biashara. Kwanza niseme wazi kuwa sina uhakika wa habari na mimi pia ni mnufaika wa mikopo hii. Hivyo bado nina maswali kama vile leseni ya Biashara ya gani?kwa maana ya aina ya biashara, thamani ya mtaji, uhai wa Biashara na kiwango cha faida n.k. Kwa hiyo tafakuli yangu imejengeka ndani ya uhaba huu wa majibu.

1. Kumiliki biashara vs ada za vyuo
Kwa uelewa wangu Ada na mahitaji ya mwanafunzi Chuoni kwa mwaka havipungui Mil 3 kwa kiwango cha chini. Hii kwa mzazi hajatimiza vizuri wito wa mkuu wa "fyatueni sasa elimu ni bure" labda inaweza isiwe shida. Kuna suala la kumiliki leseni ambako hakumaanishi biashara inazalisha faida. Ukitembelea ofisi za biashara za wilaya ni watu wengi sana wamekata leseni za biashara lakini ni wachache sana ambao biashara zao zina tija. Sote twajua kuwa mazingira ya kibiashara ya sasa nchini ni magumu sana na nyingi zinachechemea (hapa sitaenda ndani sana nisifanye uchochezi).

Nchi yoyote kuendelea inahitaji kukua kwa biashara. Ni Biashara ndizo zinazozalisha kodi ya serikali, kutoa huduma na mahitaji kwa wananchi , ajira n.k. Nchi ambayo haina wafanyabiashara wadogo na wakubwa ni nchi iliyopoteza dira ya kiuchumi. Risk ya kutumia umiliki wa leseni ya Biashara kama kigezo cha wanetu kukopa ni kwamba (kwa jinsi mazingira ya biashara yalivyo magumu sasa) wengine wanaweza kuogopa kabisa kukata leseni meaning wataacha kujaribu kufanya biashara. Hata kama mpango huu unawalenga akina Mangi ambao wana maduka nchi nzima na watoto wa upande wao wamesoma sana kama njia ya kuleta usawa wa watoto wa pande za wafugaji, bado inaweza kuwaathiri hao wa pande hizo kwa kuwa kuna biashara ya mifugo, maziwa na nyama pia.

2. Tafsiri ya mkopo

Kwa uelewa wangu mdogo, kutoa mkopo si msaada bali ni biashara pia. Bodi ya Mikopo ni kama Benki kubwa ya mikopo kwa wanachuo ambayo inapata mtaji wake kutokana na kodi za wazazi wao (wenye biashara na wananunuzi wa huduma) na inatakiwa ikusanye mikopo hiyo kwa wadeni wake ili kutoa kwa wanafunzi wengine wengi zaidi siku za usoni.

Imani yangu ni kuwa mkopo wa chuo ni deni kwa dhamana ya elimu ya mnufaika ili arejeshe apatapo kazi kutokana na elimu yake. Hapa bodi inatumia "elimu kama mwezeshi wa ajira kwa mkopaji" kama dhamana kwa ajili ya mkopo. Kimsingi Bodi inaingia "mkataba" na mwanachuo kama mlipaji na si mzazi. Katika "ideal situation" kila mwanachuo alitakiwa apewe fursa ya kukopa isipokuwa wale ambao watachagua kwa hiari kwamba hawataki shida za kudaiwa mkopo baada ya elimu na wakaweza kuangalia sources nyingine za malipo ya masomo yao kama wazazi, wafadhiri ama juhudi zao binafsi (hasa kama mazingira yangekuwapo kuwezesha vijana wadogo kuanzisha bishara zao). Msingi wa hoja hii ni kwamba mkopo ni mkataba kati ya mkopaji na mkopeshaji na dhamana ya mwanachuo ni elimu yake.

Kwa kutambua kuwa uchumi wetu hauruhusu "ideal situation" hii japo tuna uwezo huu, vimewekwa vigezo vya mchujo wa wapata mkopo. Bahati mbaya baadhi ya vigezo vina hatari ya kudidimisha urejeshwaji wa mikopo yenyewe mfano:kama mzazi kajinyima sana kulipa mamilioni (kwa wenye uchumi wa kati watakaoweza) ina maana anawekeza kwa mwanae na si kwake. Ipo risk kuwa mpaka kijana anamaliza chuo anapata kazi, mzazi atakuwa amezeeka, fukara na hana nyumba (kwa mfano) na sasa atakuwa mtegemezi wa mwane (kama malipo ya fadhira za uwekezaji wake) na pia atakuwa mzigo kwa taifa. Kijana atawajibika kupata fedha ya kulipa fadhira kwa mzazi na kijiletea maendeleo binafsi. Hizi "demand" ni lazima zitajenga roho ya tamaa na rushwa ili kutimiza majukumu. Hapa kwa uwezekanifu mkubwa tunazalisha taifa la wala rushwa na mafisadi japo inaweza isiwe hivyo.

Kama lengo ni kuwawezesha watoto wa masikini wengi kupata mkopo kwa kuwa filter wenye ahueni nje (maisha ya kati, sina tatizo na matajiri) , nia hii njema ina risk zake. Wataalamu wa mikopo wataniambia ni mtu yupi ni rahisi kurejesha mkopo kati ya masikini na mwenye ahueni. Mkopo kama biashara inapaswa iwe na mchanganyiko wa wenye ahueni ya kurejesha na wenye risk ya kutoweza ili angalau kutoa fursa ya uendelevu wake.Vinginevyo bodi italazimika kuendelea kutegemea mtaji wa kodi ambazo nazo zitapungua kwa sababu watu wenye ahueni ambao sasa nao wanaweza kuogopa kumiliki leseni za biashara. Madhara yake yanaweza yasionekane leo ama kesho lakini yataonekana tu mwisho wa siku.

Hii nimefanya kuwazawaza tu na inawezekana sana tafakuli yangu isiwe sahihi.

Nimefika safari yangu.

IsangulaKG

Facebook:
 
Back
Top Bottom