Tafakuri: Janga la kuibuka panyaroad wasomi, wizara ya Elimu imejipangaje!?

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,538
17,473
Kama Taifa tumeshindwa kabisa kuwahodhi nguvukazi ya vijana WETU Hadi WAMEKUWA panyaroad wakikimbizana na polisi!huku ni kufeli kwa sera zetu za ajira japo tuna wabobezi katika uchumi pia ni wanasiasa wakubwa.

Wimbi la vijana waliokosa ajira litaongezeka KILA mwaka na kuzalisha wahalifu wengi,kuna kundi la wasomi waliohitimu mafunzo nao watakuja na u panyaroad wakisomi kama Taifa tumejiandaaje!!?tumekubali wasomi wetu kuwa panyaroad wajao wakitumia maarifa ya shule kuwa matapeli,majizi,wahuni na nk!?

Itafikia kipindi idadi ya panyaroad itazidi idadi ya polisi je serikali imejiandaaje!!?Jaribu kufikiria kama Watoto wa mtaani wameleta taharuki hivi karibuni mitaani Hadi polisi wakijinasibu kuwapiga Risasi je kundi la vijana wasio na ajira Baada ya kuhitimu masomo yao hilo tumejiandaaje kama hilo lililopo limetushinda Hadi tunatumia silaha za moto kupambana nalo linalokuja tutaliweza kweli!!?

Matumizi ya nguvu dhidi ya vijana Hawa ni kufeli KWA sera za uchumi na elimu kiasi kwamba tumeshindwa kuhodhi nguvu zao Hadi tunataka kuziua Sasa tujiandae na panyaroad wasomi wakabaji wasiotumia mabavu kama Hawa na kuleta sintofahamu nchini!

Wizara ya Elimu harakisheni mitaala ya elimu hasa ile ya kujiajiri Ili kuhodhi vijana na NGUVU zao kabla hatujatumbukia kwenye janga kuu kama Taifa!
 
Wimbi la vijana waliokosa ajira litaongezeka KILA mwaka na kuzalisha wahalifu wengi,kuna kundi la wasomi waliohitimu mafunzo nao watakuja na u panyaroad wakisomi kama Taifa tumejiandaaje!!?tumekubali wasomi wetu kuwa panyaroad wajao wakitumia maarifa ya shule kuwa matapeli,majini,wahuni na nk!?
Halafu wanasambaa kwa kasi sana nasikia wameshafika Karagwe
 
Kama Taifa tumeshindwa kabisa kuwahodhi nguvukazi ya vijana WETU Hadi WAMEKUWA panyaroad wakikimbizana na polisi!huku ni kufeli kwa sera zetu za ajira japo tuna wabobezi katika uchumi pia ni wanasiasa wakubwa.

Wimbi la vijana waliokosa ajira litaongezeka KILA mwaka na kuzalisha wahalifu wengi,kuna kundi la wasomi waliohitimu mafunzo nao watakuja na u panyaroad wakisomi kama Taifa tumejiandaaje!!?tumekubali wasomi wetu kuwa panyaroad wajao wakitumia maarifa ya shule kuwa matapeli,majizi,wahuni na nk!?

Itafikia kipindi idadi ya panyaroad itazidi idadi ya polisi je serikali imejiandaaje!!?Jaribu kufikiria kama Watoto wa mtaani wameleta taharuki hivi karibuni mitaani Hadi polisi wakijinasibu kuwapiga Risasi je kundi la vijana wasio na ajira Baada ya kuhitimu masomo yao hilo tumejiandaaje kama hilo lililopo limetushinda Hadi tunatumia silaha za moto kupambana nalo linalokuja tutaliweza kweli!!?

Matumizi ya nguvu dhidi ya vijana Hawa ni kufeli KWA sera za uchumi na elimu kiasi kwamba tumeshindwa kuhodhi nguvu zao Hadi tunataka kuziua Sasa tujiandae na panyaroad wasomi wakabaji wasiotumia mabavu kama Hawa na kuleta sintofahamu nchini!

Wizara ya Elimu harakisheni mitaala ya elimu hasa ile ya kujiajiri Ili kuhodhi vijana na NGUVU zao kabla hatujatumbukia kwenye janga kuu kama Taifa!
Ni vigumu ukiwa kwenye airconditioned V8 kumkumbuka aliyekosa kiamsha kinywa.
 
Wizara ya Elimu harakisheni mitaala ya elimu hasa ile ya kujiajiri Ili kuhodhi vijana na NGUVU zao kabla hatujatumbukia kwenye janga kuu kama Taifa!
Suala la vijana kujiajiri mimi huwa silikubali. Je, waliosomea ualimu lbda wako laki mbili, Kila mmoja atafungua shule yake? Waliosomea udaktari/kada zingine za afya, Kila mmoja aanzishe hospitali? Mainjinia Kila mmoja kiwanda chake?

Wanasiasa wamekuwa wakihubiri vijana wajiajiri, wakati wao watoto wao na ndugu zao wanawapa Kwa upendeleo zile nafasi za ajira ktk mashirika, majeshi na idara za serikali.

Suluhisho sio kuwaimbia vijana wajiajiri, bali kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuhamasisha/kuwezesha matajiri wa ndani na nje waanzishe viwanda na shughili za kiuchumi tuweze kuwa na nafasi nyingi za ajira. Ikumbukwe suala la kodi ni mwiba mkali kwa wawekezaji.

Hawa vijana wanaoimbiwa wajiajiri, mtaji walionao ni elimu na nguvu zao. Hawana fedha, hawana ufafhili na hawakopesheki sababu hawana mali ya kuweka dhamana.

Serikali iwe na sera nzuri zitakazozalisha ajira. Sera mbovu, eg ktk awamu Tano ziliuwa ajira badala ya kuongeza ajira. Tulishihudia mabenki yakifungwa, biashara kufilisika, mahoteli yakifungwa, Arusha na Kilimanjaro mashamba mengi ya maua yaliyoajiri maelfu ya watu yalifungwa, nk.

Haina maana kuwekeza kwenye kusomesha vijana wapate vyeti na shahada, halafu waje wawe wamachinga na bodaboda (au panyaroad).
 
Back
Top Bottom