Tafakuri chokonozi: Ni dengu, dengi, au ni propaganda?!

Tafakuri chokonozi: Ni dengu, dengi, au ni propaganda?!

Kikombe cha Mwaisapile ulikunywa au?

Funguka akilinchi inaibiwa

Nilikuwa nabishana na Babu Slaa juu ya Gongo tahamaki muda wa kwenda kwa Mwaisapile ukawa umekwisha.

Lakini hongera sana kwa kuishi nchi hizo.

Hao woote pamoya na weye ni katika wasaka tonge.

Unachotakiwa kujua ni kjwa mirija yao ya kufyonzea nchi ilikatwa, sada ndo ukaona wamevamia kwa ile aina ya NITOKEJE...!?

Iringa wanakusalimia sana wanauliza utakuja lini maana kilimo ulichokikwepa kimekwisha na sasa wanajiandaa kuvuna.

Karibu mavunoni najua bado wasaka tonge pitia pale Msimbazi harakati za uchaguzi huenda ukaambulia chochote kitu.

Na ntarejea ...
 
Kama ni ugonjwa hatari kama wizara na media wanavyotaka tuamini, basi waweke karantini watu wasitoke wala kuingia DSM, Mtwara na kwingineko. Nje ya hapo nakubaliana na mleta mada!
 
dah! hapo kamanda bado sijakusoma vizuri, maana nasikia kuwa ni kweli umekuwa tishio halafu upo huko Dar es salaam, sasa kama ndio hivyo kama unavyosema kwanini iwe Dar es salaam tu?
 
Last week nilikua na malaria kali sana, nikaenda kituo kimoja cha Afya pale maeneo ya Mabibo Mwisho, mtu alienihudumia nikawa napiga nae story mbili tatu ili apate vizuri background ya tatizo langu! Akasema kuwa huo ugonjwa umekuepo muda mrefu tu na kwamba wala hauna IMPACT ya kihivyoo na kwamba unakuzwa tu na media au kwa malengo mahususi ILA hao mbu wamekuepo eversince!
HP nimepoteza mawasiliano yako aisee, nicheki kwa phone
 
Watu wanakufa wewe unaleta siasa. Inamaana wanaokufa wanaigiza. Subiri yakukute ndo utajua.

Mkuu nilijua kwenye hili ungetaka CCM itoe tamko bil 200, unafikiri hizi zingeenda Pale Muhimbili zingeokoa maisha ya watu wangapi? Uozo ndani ya report ya CAG bill 2 hazikutumika sector ya ukimwi wangapi wanakufa huko?
 
dah! hapo kamanda bado sijakusoma vizuri, maana nasikia kuwa ni kweli umekuwa tishio halafu upo huko Dar es salaam, sasa kama ndio hivyo kama unavyosema kwanini iwe Dar es salaam tu?

Mkuu unapoteza malighafi zako kufikiri kuwa kweli ugongwa huo ni tishio kiasi hiki,

Ugonjwa ulikuwepo tangu na tangu kama ilivyo kifua kikuu ama matende,

Afadhari tukubaliane kuwa maralia ni ugonjwa hatari na unahitaji hamasa za serikali
 
Mkuu Yericko labda niwe muwazi zaidi kwamba hata ikibidi tatizo linaweza likatengenezwa maabara,likawepo kweli lakini kwa sababu hizo ulizosema,kudivert akili za watu kwa manufaa fulani.na tatizo linalotengenezwa makusudi ni baya,maana waliolitengeneza wanasubiri reaction yenu ya kuomba msaada ili waitumie kuwaweka kwapani kabisa.watu hawafahamu kuwa zipo maabara za kutengeneza matatizo na wapo wataalam waliosomea fani hiyo ambayo huwezi kuikuta kwenye mainstream education system.tatizo ni kwamba watu wengi hatufahamu kiwango cha juu cha uovu na usaliti ambacho wale tunaowaamini wamekifikia na wanatumia imani yetu kwao kutufanya misukule yao huku tukiwapigia makofi na kuwasifu sana..aargh!
 
Mkuu Yericko labda niwe muwazi zaidi kwamba hata ikibidi tatizo linaweza likatengenezwa maabara,likawepo kweli lakini kwa sababu hizo ulizosema,kudivert akili za watu kwa manufaa fulani.na tatizo linalotengenezwa makusudi ni baya,maana waliolitengeneza wanasubiri reaction yenu ya kuomba msaada ili waitumie kuwaweka kwapani kabisa.watu hawafahamu kuwa zipo maabara za kutengeneza matatizo na wapo wataalam waliosomea fani hiyo ambayo huwezi kuikuta kwenye mainstream education system.tatizo ni kwamba watu wengi hatufahamu kiwango cha juu cha uovu na usaliti ambacho wale tunaowaamini wamekifikia na wanatumia imani yetu kwao kutufanya misukule yao huku tukiwapigia makofi na kuwasifu sana..aargh!

Nakatika mazingira yakawaida hili linaweza kutendeka hapa tz tena kwa kiwango cha juu kabisa
 
umenipa tafakari, ngoja kama nakupata hivi? maana vyombo vyote vya habari vimehamamia kwenye dengue, wanasema hauna tiba, hapohapo watu mia 4 wanaumwa, sasa najiuliza wanaponaje? kutokana na hatari ya ugonjwa huo kwanini bado muingiliano wa watu kuja dar unaendelea? wacha niendelee kutafakari.
 
Sijasema Dengue halipo, najua lipo! Bali wasiwasi wangu ni namna linavyopewa promo wakati huu kuliko magonjwa mengine yanayo uwa watanzania wenzetu kwa maelfu kwenye hospital.

serikali ingenyamaza kimya au isingelichukulia kwa uzito tatizo ungekuja kuponda kwamba haijali wananchi wake,unajua wamekufa watu wangapi? ulitaka wafe watu 1000 ndio ujue kwamba ni tatizo? Au kwa sababu hakuna nduguyo aliyefikwa? sio kila kitu siasa tu mohamed Mtoi
 
Last edited by a moderator:
Kuna haka ka ugonjwa ambako huenda kanakuja kufunika maswala mazito kwenye huu mchakato wa katiba na maswala mazito ya muungano tuliyokuwa nayo sasa, naanza kupata wasiwasi maana watawala wanawajua vizuri watanzania kuwa ni watu wanaobebwa na matukio. Likija tukio fulani na likapambwa kwa mapambo ya aina ya kuwatoa watu kwenye mstari basi watu wanahama.


Kama mnakumbuka baada ya serikali kubanwa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na watu kuwa tayari kuingia barabarani kipindi kile ambacho pia kulikuwa na maandamano ya kuondoa utawala ulioshindwa kuleta tija kwenye nchi za uarabuni,ghafla likaja zengwe la kikombe cha babu wa Loliondo.

Kwenye kikombe cha babu wa Loliondo viongozi wa serikali wakawa wa kwanza kwenda kupata kikombe, inasemekana alianza MSAFIRI, akaja mtoto wa mkulima aliye pinda mgongo, orodha ndefu ikafuata, kibaya zaidi serikali ikaruhusu mpaka wagonjwa waliokuwa mahospitalini eti watoke na kwenda kwenye kikombe, baada ya hapo vikafuata vifo na adha zilizotokana na msusuru wa watu kule Loliondo.


Likapita la kikombe cha Loliondo watu wakawa wamehama kwenye kufikiria kupanda kwa gharama za maisha na uhaba wa umeme. Akili zikahamia Loliondo, Kila unaye mgusa, mwenye sukari, mwenye utamu, mwenye mafua, aliye jikwaa kidole wote wimbo wao ulikuwa mmoja "Loliondo" Kwa hili serikali ikapata ahueni, ikajipanga, ikafanikiwa kuwapumbaza watanzania, waliokufa wengine wakatupwa vichakani. Maisha yakaendelea watawala wagongena mvinyo..


Siku hazikuganda, Umekuja mchakato wa katiba, ukweli uliokuwa unafichwa umeanza kudhihiri, nondo zimeanza kushushwa, wasiotaka ukweli ujulikane wameanza propaganda za kufa mtu! Hawataki ukweli ujulikane, wanataka tuzidi kukaa kwenye nusu karne ya uwongo! Ghafla eti tunasikia Dengua, wengine wanaita Dengi, wengine Dengu, wengeni Dengelua yaani ngonjwa moja hata wataalamu wetu kila mtu anatamka anavyotaka yeye!


Wasiwasi wangu eti gonjwa hili limeanza na wasanii maarufu! Limeanza na Ray C akapata coverage front page kwenye magazeti, akaja Dr Cheni naye hivyohivyo! Halafu eti tunaambiwa umeua mpaka Daktari, na wanatajwa wagonjwa wengine kadhaa, wanasahau kuwa kwa tanzania ugonjwa hatari ni Maralia na vifo vya kina mama wajawazito, kila dakika 10 maralia huua si chini ya watu 5, na kila dakika 5 kuna si chini ya mama mjamzito mmoja anaye poteza maisha.Sio hili DENGE, Sijui DENGUA, SIjui DENGI, sijui DENGELUA.


Wanataka kututoa kwenye agenda muhimu hawa! Hii ni propaganda! Baada ya hapa utasikia mikusanyiko hairuhusiwi, Lakini hawatasema kuwa hata kwenye dalaladala na boti kuna mikusanyiko! Kuna watu wanalengwa kunyamazishwa hapa.


AKILI KUMKICHWA poleni watanzania wenzangu sijui kwa gonjwa gani vile?!... Ni Dengi, Dengu, Dengua au Dengelua?! Sikatai kuwa lipo, napata wasiwasi na gonjwa hili linavyopewa promo kana kwamba limekuwa tishio kuliko Maralia na vifo vya kina mama wajawazito.

ImageUploadedByJamiiForums1399977108.155816.jpgImageUploadedByJamiiForums1399977125.468330.jpg
 
Back
Top Bottom