Tafakuli

Wagabuli

Member
Nov 28, 2015
78
144
Sijawahi kusikia mkono ukipewa shukrani na mguu kwa kuutoa mwiba, lakini ni ujinga na uzuzu wa mguu kufikiri kwamba unapaswa na unastahili kutolewa mwiba, maana kuna miili isiyo na mikono, na miguu ya miili hiyo ichomwapo na miiba hutaabika sana.

Hivyo ni neema na baraka kwa mguu kuwa na mwili wenye mikono.
Lakini siku moja ujinga wa miguu utakwisha pale utakapokuja kugundua kwamba kuna miili isiyo na miguu, na miili inatembea na kufanya kazi kama kawaida!! ikigundua hilo ndio uzuzu na ujinga wote utaisha na kama haitakuwa imechelewa kutoa shukrani hata kwa kusuguliwa magamba basi itakuwa inaenda kuzikwa peke yake bila kiwiliwili.
Jumamosi njema wana Jukwaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom