Tafakari ..!!!

Tafakari ..!!!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,459
Reaction score
872,119
1421865483525.jpg1421865352582.jpg
 
Wachomwe tu, roba za mbao, wizi wa reja reja ni mateso sana.
 
Si kwamba sina ubinadamu ila kuna wakati unafika unasema inatosha, mjusi hawezi kuwa mamba ila vibaka waweza kuwa majambazi ndo yale ya kuvuliwa nguo ukiwa na mkweo, mashemeji, bosi n.k na kuimbishwa juu.
 
Nunua Vogue yako tena kwa mkopo........siku moja ukute taa hakuna au power windows........utaelewa maana ya hiyo picha ni nini.........ni mfano mmoja tu huu.........
 
Badala ya kuyachoma majizi makubwa(mafisadi),majangili wenye madhara makubwa kwa jamii wao wawachoma vibaka wenye madhara madogo kwa jamii kwa kukwapua cm(vimeo),power window,kuku nk.
 
Wewe ujawai ibiwa au kukatiwa nyavu za dirisha.roba za mbao au kupigwa mapanga.walio wai wanajua uchungu wake
Chipukizi nilishafanyiwa hicho kitu mwananyamala walinisafishia sitting room na kwenye gari walifanya kufuru walikuwa kama sita hivi Jumamne, Morroco, Tito, Pembe, Twaha na Baharia! Walikufa wote kwa nyakati tofauti kasoro Pembe ambaye sasa kalemaa miguu yote yuko pale geti la mwananyamala hospital anaomba msaada! Huyu ndio alikuwa kiongozi na mtoa mchongo
 
Last edited by a moderator:
Nunua Vogue yako tena kwa mkopo........siku moja ukute taa hakuna au power windows........utaelewa maana ya hiyo picha ni nini.........ni mfano mmoja tu huu.........

Shikamoo!
Walikuja home usiku, TOYOTA raum yangu waliigeuza ndafu, power windows, taa za nyuma, taa za mbele, side mirrors na battery!
Walikomba!
Mwenyewe nikaenda shule kulipia sch bus fee ya mtoto! Elfu 60/month!
2 days later, wife anatakiwa clinic kwa Dr. Kairuki!
Home ni Mbezi ya Goba!
Nina kidumu cha mafuta, nikiskia kelele za "wimbo wa taifa" natoka nacho, na kibiriti juu!
Mtanisamehe wenye moyo wa masihi!
 
slim5 kwanza pole sana nayajua maumivu yake yalivyo!! Kuibiwa ni negative altitude kumchoma mwizi moto ni kuifuata ile negative altitude yaani hasi inazalisha hasi

Umeisoma mfano wangu hapo juu? Walikufa wote lakini sikushiriki kwenye mauaji yao aliyebaki hai ni mlemavu wa miguu sasa na kila nikienda pale alipo nampa chochote

Ni phenomenon ngumu kuilewa, mimi nilichukua hatua za kisheria nikaripoti polisi nikakaa kimya nikamwachia Mungu! Kuna nguvu ya ajabu katika hili KUMWACHIA MUNGU

Huyu Pembe anayeteseka ndio alitoa mchongo wote alikuwa anapafahamu ninapoishi vilivyo na nilikuwa namsaidia mara kwa Mara! Tito aliuliwa MK akiiba, Morroco hivyo hivyo aliyepewa ahifadhi mzigo alikufa wiki moja baadae pale jangwani alitaka kupora cheni wakamuwahi, mwingine Alifia bagamoyo walipukutika wote ndani ya Siku 90

Nilishauriwa mwanzoni nisome albadiri/ albadli au niende kwa waganga sikufanya hivyo na wezi wangu wakaandibika ningefanya moja kati ya hayo ningeamini kitu ambacho hakipo
 
Huku kwangu alietoa mchongo kwa "wazee wa kazi" ni jirani yangu, tena ni askari wa kituo kimoja hapa town, ni mvuta bangi na chapombe tu, nikaamua kumdharau tu!
Aibu kwake!
Hata ule ushirikiano tuliokuwa nao, ss hv anaukwepa!
 
Last edited by a moderator:
Baada ya kipigo na moto juu.

Huyo jamaa huyo anataka kuhakikisha mpaka anakata roho huyo aliewekewa tairi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom