Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,640
- 697,940
Hivi ni vifaranga vya ndege vilivyofariki kwa njaa vikiwa ndani ya kiota baada ya kumsubiri kwa muda mama yao awaletee chakula lakini kumbe mama yao alikuwa ameuawa na mtu asiyejua umuhimu wa uhai wake kwa watoto wake na watu wengine wanaomheshimu na kumtegemea.
Mambo ya kujifunza:
1. Kila unapopigana na mtu, jua unapigana na wategemezi wake pia.
2. Ukiua roho umeua ndoto za watu wengi zaidi.
3. Usiue ndoto ya mtu mwingine kwa sababu tu haukubaliani na mawazo yake.
4. Msaidie aelimike kama wewe ili aone mwanga zaidi, baadae atakushukuru na kukuombea mema.
5. Ukishindwa kumpa mtu manufaa basi usimpe mtihani.
6. Usipoweza kumnusuru basi usimdhuru.
7. Kama huna la kumfurahisha basi usimuhuzunishe.
8. Ukiwa hukubaliani nae basi usimfanyie uadui.
9. Usipofurahia neema zake basi usimuonee wivu.
10. Ukiwa humkubali basi usimuharibie kwa kumfanyia fitna.
11. Ukiwa huna la kumsifu basi usimkejeli.
12. Ukiona amekuzidi maarifa au maisha, basi usimchukie au kumchafua.
13. Usiwe sababu ya watu kuacha ndoto zao.
14. Kila unayemuona mdogo, pamoja na udogo wake naye pia ana watu wanaomtegemea kama wewe.