Tafakari; Je wana jF ni invisibles?

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,722
3,366
Ni rahisi kumuona mtu anachekelea huku anachat kwa uwazi page ya Facebook, Instagram au TikTok.

Ni rahisi kumuona mtu anatazama channel ya YouTube kwa uwazi na bashasha tele.

Ni rahisi sana kumuona mtu anachat au anasoma mtandao wa X (Twitter).

Ni rahisi sana kutomuona mtu yeyote, popote pale anatumia jF.

Cha ajabu ukiangalia posts za hapa jF ni kama zinaingia kila sekunde!

Sasa hawa wanaopost humu wanatoka wapi jamani au ni invisibles?

Eboo,,,hivi namimi ni invisible?

 
Mimi mboni natumia free na wengi wanajua natumia JF ingawa ID yangu hawaijui natumia ID ipi maana hio ni privacy yangu, hippopotamus pita mbali
daah hongera aisee

unakimbizwa na hippo au ndonani uyo?
 
Kuna muda nilikua naichukulia JF poa tu, kuna sehemu flani kama kijiwe huwa nakaa mara kwa mara, nilikuwa natumia JF wazi wazi nikiwa hapo

Kuna siku tunapiga stori tukaanza kutaniana nikashangaa nachekwa eti natumia JF

Tokea siku hiyo, JF naitumia nikiwa mwenyewe
 
Miaka yangu 14 JF sijawahi kukutana na mwana JF.... Wala kujua handle ya mtu. Ingawa yangu kuna baadhi ya watu wanaijua kutokana na maswala mbalimbali waliyoniagiza niwasaidie kutuma kwa jamii....
 
Back
Top Bottom