Tafadhari Brother Freeman Mbowe, Tujitafakari upya

Tafadhari Brother Freeman Mbowe, Tujitafakari upya

zitto ndio wa kumdhihaki JJMnyika??mbona ye alipokewa Dar na Mbowe??hadi mademu zake wa mwanzo ambao kwa sasa n wake za watu hatuwasemi tunajua alipatia wapi jeuri kuwapata
 
Zitto kafikishwa hapo alipo na mbowe, ingawa shukrani ya punda ni mateke!
 
Dogo anakufa kiume, atakuja kugundua kuwa alkosea akiwa amechelewa sana.
 
Kila jambo linalofanywa na Serikali yetu CHADEMA hukosoa kwa kutumia neno demokrasia, tena viongozi wao kama Tundu Lisu, Mbowe, Msigwa &Co. huenda mbali zaidi na kusema kwamba Raisi wetu hafanya maamuzi yasiyo ya kidemokrasia na hutupa mifano mingi ya jinsi rais wetu alivyopaswa kufanya kama vile Wazungu wafanyavyo, mpaka hapo labda sina tatizo napo! Ila tatizo langu ni kwanini CHADEMA huwatolea mfano Wazungu na utawala wao nusu nusu tu?

Ni kwanini Wazungu wazuri pale ambapo CHADEMA wananufaika lakini linapokuja swala uongozi wa CHADEMA kwamba nao uwe kama Wazungu walivyo hasa kwenye eneo la demokrasia CHADEMA huruka na kupinga kwa mfano vyama vyote vya siasa vya Wazungu (Magharibi) viongozi hujiuzulu pale ambapo amekiongoza Chama chake na kushindwa uchaguzi, sasa Mwenyekiti wa CHADEMA ameongoza chama chake kwenye chaguzi tatu na zote ameshindwa, kwa nini hajajiuzulu?

Kwa maana hiyo ndiyo demokrasia, Tundu Lisu mbona hajawahi kuliongelea hili?? Ni kwanini hamjawahi kumshinikiza Mwenyekiti wenu Mbowe ajiuzulu kwa maana ameshindwa kukisaidia Chama kuingia madarakani mara tatu, hivyo hana miujiza tena!
Au ni demokrasia tu pale ambapo mnanufaika na pale ambapo hamfaidki ninyi ni waafrika??!
 
Chadema huwa wanashinda uchaguzi ila NECCM wanafanya yao. Sio kosa la Mbowe hilo.
 
Ndugu wala usihangaike na hawa watu
Walipo wapo hali Mbaya
Siasa za Vibendera zimefika mwisho

CDM hawana muelekeo kwasasa
Niheri na Baraka Kila kona ya Tanzania
Watanzania watoto kwa wakubwa
Wanamkubari Rais John Joseph Pombe Magufuli kwa mioyo yao bila kuwa Vibendera.
Waendelee hivyo hivyo na siasa zao Uchwara waone chamoto 2020
 
Ndugu wala usihangaike na hawa watu
Walipo wapo hali Mbaya
Siasa za Vibendera zimefika mwisho

CDM hawana muelekeo kwasasa
Niheri na Baraka Kila kona ya Tanzania
Watanzania watoto kwa wakubwa
Wanamkubari Rais John Joseph Pombe Magufuli kwa mioyo yao bila kuwa Vibendera.
Waendelee hivyo hivyo na siasa zao Uchwara waone chamoto 2020

Motochini mwanangu ni mwehu tu asiyeona mchango wa Chadema na vyama vingine makini vya upinzani. Bila has Jan as hata majipu yasingelitumbuliwa, achilia mbali sasa hivi kila kiongozi kujifanya ni mchapa kazi. Bila cdm hata Maghufuli asingelikuwa RAIS

Pili ukitaka kujua wanaungwa mkono kiasi gani basi vikwazo vya mikutano ya kisiasa, matangazo live ya bunge na sheria kandamizi ya magazeti etc vyote hivi viondolewe

Pia tuwe na Neutral ground kwa ajili ya siasa na taasisi huru za kusimamia usimikaji wa dola. Sio unatamba wakati man mbeleko ya DOLA!!!!!!!
 
Huwa kuna kosa gani mtu/watu/kundi linapo chukua calculator/karatasi na kalamu/komputa/au kifaa chochote kile ili kura zake zilizopigwa kuzihesabu ili mwishoni ajue ni kiasi gani ijulikane no kiasi gani amepigiwa? Je huyu mtu unapovamia vifaa vyake vya kuhesabia ukavibeba chini ya mtutu wa bunduki na yeye ukamuweka mahabusu kwa kumtishia kumfikisha mahakamani, vifaa vyake baadae unaviharibu na inapita miezi 6 hakuna cha mahakama au ndugu ya mahakama, tafsiri yake ni nini? Sio kuwa ktk uchaguzi wa 2015 Ukawa walivamiwa wakaharibiwa vifaa vya kuhesabu kura zao? Hilo tukio sio linaonyesha kuna kilichotakiwa kufichwa? Kama ushindi ndio lilikuwa lengo hilo si no dhahili ulifichwa au ulifanyiwa mazingaombwe ushindi? Kama ni ushindi ni ushindi wa ccm? Chadema? au wa nani? Hapa inahitajika digrii gani ya alinaye kupata jawabu? Hata ambaye hakusoma atakupatia jibu. Msijiondoe akili wapenzi.
 
Majuzi rais wa Ufaransa alitembelea Misri akaambiwa "Ustaarabu uliopo Ulaya hauwezi fanya kazi kwenye nchi za dunia ya 3, mtuache"

Juzi Rais wa Uturuki amesema "Kama suala ni sheria za ndani ya nchi ndo mnaona hatuwezi kujiunga na Umoja wa Nchi za Ulaya basi mbaki, maana tunakabiliana na hali ngumu ya kijamii kuliko mnachoona".

Hii ni mifano ya watu wanaoona hawawezi fanya sawa na wazungu katika suala la kuendesha nchi zao.

Taifa hailiendeshwi kwa ubia na mataifa yaliyoendelea.

Zaidi ni kuangalia hali halisi ya jamii na mahitaji ya wakati huo kwa mstakabili wa taifa si siasa.
 
FREEMAN MBOWE APOTEZA MVUTO CHADEMA NA KWA WATANZANIA KWA SASA.

Watanzania wenzangu Freeman Mbowe ni mwanasiasa aliyezaliwa tarehe 14,September mwaka 1961,na ni miongoni mwa waasisi wa Chadema chama kilichoanzishwa mwaka 1992 akiwa kijana kwa wakati huo, alichaguliwa kuongoza kurugenzi ya vijana na mshauri wa usimamizi wa fedha

"Freeman" Mbowe alipewa jina hili kwasababu alizaliwa kipindi ambacho Tanganyika ilipata Uhuru, mke wake anaitwa Liliani Mtei yani mtoto wa muasisi wa Chadema na ndo maana Mzee mtei karidhia Mbowe kuwa mwenyekiti wa Chadema, na kwa utafiti niliyoufanya kuna mkakati wa ndani unaolatibiwa na Mbowe pamoja na mkwe wake kuhakikisha baada ya Mbowe anafuatia mwenyekiti mwingine kutokea katika ukoo huo wa Mtei pamoja na Mbowe kitu kinachoanza kuzua taharuki ndani ya Chadema.

Mwaka 1995 mbowe aligombea Ubunge katika jimbo la Hai nakushindwa vibaya sana kwa asilimia 28.6 kwa wakati huo jimbo liliongozwa na mgombea wa NCCR lakini mbowe alilalamika kuwa ameibiwa kura.
Mwaka 2000 Mbowe aligombea tena ubunge katika jimbo la Hai na kushinda kwa asilimia 64.5 tena mh,mbowe japo alishinda alidai kura zake nyingine aliibiwa na chama Tawala. Mwaka 2004 mbowe alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chadema akichukua nafasi iliyoachwa na Mzee Bob makani.

Mwaka 2005 Mbowe alichaguliwa na chama chake kuwa mgombea Urais katika uchaguzi mkuu uliyopangwa kufanyika tarehe 30 October mwaka 2005 na mgombea mwenza alikuwa Jumbe Rajab Jumbe lakini kwa baati mbaya huyo mgombea mwenza alifariki Dunia na Tume aliamua kupanga tarehe 14december mwaka 2005 kuwa ndo siku ya uchaguzi mkuu lakini katika uchaguzi huu Mbowe alikuwa mshindi wa tatu kwa asilimia 5.88 cha ajabu Mbowe alisikika akisema ameibiwa kura na kama kawaida yake kuibiwa kura ni kama wimbo wake, lakini hakuwambia wafuasi wake je na professor Lipumba aliyepata asilimia 11 na kuwa wa pili nae alimuibia?

Mwaka 2010 Mbowe alichaguliwa kuwa mbunge wa Hai kwa asilimia 51.63 kwa wakati huu aliogopa kugombea Urais maana alikuwa amepoteza mvuto maana kama mtu jimboni kwake anapata asilimia 51.63 hakika kwenye Uraisi kwa Wakati huu angeweza kupata asilimia 0.008 lakini bado alidai kuibiwa kura zake.

Miongoni mwa vitu vingine vinavyopelekea Mbowe achokwe na wanachama wake pamoja na wananchi ni zifuatazo;

1, kufanya maamuzi ambayo hayatekelezeki na yasioleta mafanikio, mfano mnamo tarehe 13 mwezi wa nane mwaka 2006 Chadema walifanya uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhakikisha wanashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na Mbowe aliwakikishia wananchi kuwa atahakikisha chadema wanaingia Ikulu mwaka 2010, ni hii ni mwaka mmoja baada ya mbowe kushindwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Na mkutano huu ulifanyika katika ukumbi wa PTA Dar es salam,kampeni hii ilipewa jina la TUMAINI JIPYA cha ajabu wanachama na wananchi wanajiuliza mbona mwaka 2010 uchaguzi uliisha wala Chadema hatukushinda na mbowe hakutoa mlejesho kwa wananchi na kamati kuu yao ispokuwa aliendelea na wimbo wake wa kuibiwa kura na huu ni mzimu unaotafuna Chadema kuwa mazuzu wakudanganywa kila siku na wao wanafuata.

2, Mbowe ni mhoga na mtu anayependa kutanguliza watu wengine ili waumie yeye akiwa salama, mfano mwaka 2010 mbowe alitangaza maandamano makubwa pale Arusha lakini baadae wakiwa wanaandamana yeye alikimbia na kumuacha Dr.slaa na mkewe wakipigwa vibaya baada ya kukaidi amri ya polisi sisi wana chama wa Chadema sasa tumeshutuka hatutakubali tutangulizwe bila yeye kuwepo, hayo ni maneno ya mtoa taarifa wangu na kiongozi mkubwa wa Chadema.

3, katika vikao vya Chama Mbowe ni dikiteta asiyezingatia akidi ili kufanya maamuzi, mfano mwaka 2010 kamati kuu ya Chadema ilifukuza madiwani watano wa wilayani Arusha ambao ni, Estomih mallah,John Bayo, Charles Mpanda, Rehema mohamedi na Reuben Ngowi lakini taarifa za ndani za kamati kuu zinadai, kamati kuu ilikataa wasifukuzwe lakini yeye alipotoka nje katangaza kuwavua madaraka hawa madiwani kitu ambacho kinalalamikiwa mpaka leo ndani ya chama.

4,Mbowe ni kigeugeu na mtu asiyeshaurika, mnamo Sunday, September 14,2014 katika ukumbi wa mlimani city Mbowe alitangaza maandamano yasiokuwa na kikomo nchi nzima mara baada ya kuchaguliwa na kuwa mwenyekiti wao kwa kura 789 huku mpinzani wake akipata kura 20 ambae ni Gambaranyere Mwangateka, taarifa za ndani zinasema Mbowe alikurupuka kutoa kauli hiyo maana haikujadiliwa sehemu yeyote ile, kibaya zaidi baada ya Mbowe kuona hali ni mbaya kakimbia kwenda Afrika kusini huku kaacha wafuasi wake hawajui chochote na hii kupelekea maandamano hayo kufeli.
Mwezi July mwaka 2016 mbowe alitangaza maandamano makubwa nchi nzima yatakayo anza tarehe moja lakini inasemekana Mbowe hakupata baraka za kamati kuu isipokuwa yeye kalazimisha.m

Na sasa baada ya kuona hali ni mbaya habari za kina na za kuaminika zinasema tena mh,mbowe kapanga safari ya ghafula kwenda Ujerumani tarehe 28 augost mwaka huu yani siku nne kabla ya siku ambayo maandamano yamepangwa na hii ni hatari kwa vijana wenzangu tusikubali kuingia barabarani wakati mbowe akiwa Ulaya anakula kiyoyozi.

Mwisho nawashauri wanachadema hususani wabunge wasiomkubali na viongongozi wanaopinga maamuzi yake wampinge hadharani kama walivyonipa ushirikiano kupata taarifa hizi za ndani kuhusu Mbowe.
Imeandaliwa na
Comrade,

Mwita Nyarukururu
mwitanyarukururu@gmail.com
 
Amepotezaje mvuto wakati wewe mwenyewe UMEVUTIWA kuandika juu yake kwa siku nzima ya leo?
 
Sio mboe pekee hata Chama kiujumla kimepoteza mvuto
 
Sio mboe pekee hata Chama kiujumla kimepoteza mvuto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom