Tafadhari Brother Freeman Mbowe, Tujitafakari upya

Tafadhari Brother Freeman Mbowe, Tujitafakari upya

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,936
Tatizo ni kiburiiii tu cha kawaida au academic Arrogance!!!Dogo ulijiona mkubwa kuliko chama au kuna mahali mlikoseana?Nenda Zitto nenda,Angalikuwapo Mama yako Shida Salumu angekuombea msamaha wangemuonea aibu na kukurudisha kundini.Asingekubali na hajawahi kukubali kukuona unaiacha Chadema yako.

Mama hayupo tena,hakuna wa kukutetea na kukuombea msamaha...hata Mama nakumbuka tukiwa Tabata Magorofani aliwahi kukuonya kuwa achana na miruzi mingi kumbuka waliokulea na walikokutoa...nakumbuka Bi Shida alitoa machozi tukiwa pale Tabata.Alikuasa kuachana na wanaokupotosha,alisema aliongea kwa kirefu na wazee wa Chama akiwemo Mzee Kimesela na Mzee Mtei,akakwambia na yeye kagundua kuwa umekosea na ujirekebishe,Kwa ushahidi wa namna ulivyouzwa majimbo ya Musoma Vijijini nk,Mama alikuomba sanaaa usirudie wala usishindane na waliokulea,alisema tuache tamaa,tusirubuniwe na vijipesa tukawasahau wenzetu na kuwauza,akasema familia ina heshima ya kuwa waasisi wa Chadema,tusiipoteze historia hiyo.Nakumbuka akasema miaka 20 ijayo mwanetu Chachage Zitto Zubeir Kabwe aje ajivunie uasisi wa bibi na baba ndani ya Chadema

Nasikitika umepuuza ushauri wa mama,Japo ulisema utamuenzi lkn kwa hili hujamuenzi..umemuangusha Mama umemuangusha,angakuwa hai asingekubali uondolewe ktk chama alichojua unakipenda toka ukiwa mtoto,anakumbuka jinsi wakati mwingine alivyokugombeza usome kwanza badala ya kupendelea siasa...Leo mama asingekubali hata kidogooooo ...

Jitafakari Zitto,najua baba yako si sehemu ya washauri wako kisiasa lkn rudi nyuma tazama ulipokosea..Wewe siyo wa kufa kibudu hivyo kisiasa Ndani ya Chadema,Weeee Zitto Zubeir Kabwe!!!????Yaani wakati 2005 Salumu Mwalimu akiwa bado haijui Chadema Wewe ulikuwa ndani ya harakati,2003 wakati Ole Sosopi akiwa shule ya msingi akichunga ndama...wewe ulikuwa kwenye hostel za Chuo kikuu usiku wa manane tena kwa Siri na Mbowe mkipanga mikakati ya kupata wanachama toka Chuo kikuu.

Nakumbuka siku zile za mwisho wa week chuoni...Freeman Mbowe akija Hall kwa gari binafsi usiku wa weekend,akitubeba kwa gari mpaka club billicanas,wakati huo tukimuita brother,kwenda kupoteza mawazo na kurefresh then kuturudisha au wakati mwingine kulala huko huko,tukila chips ndani ya sahani moja,tukipita katikati ya jiji usiku tukishangaa jinsi habari za mitaa ya Ohio tulizosoma magazetini sasa twaziona kwa macho.Ni wapi wewe na brother Freeman mlipotofautiana??Yule Freeman aliyekwambia hata kwa kuiuza Bilicanas wewe lazima ukagombee jimbo la Kgm Kaskazini,Freeman aliyekuwa anakutegemea kwa mambo Mengi leo mmegeukana???kweli siasa mchezo mchafu...yaani urafiki na undugu wenu unavunjika sababu ya tofauti za siasa????

U sometimes used to feel our pocket money kipindi cha miezi dume..ilifikia mpaka Siri za ndani baina yenu mkawekeana bayana!!Ni siasa tu au kuna mengine??Kama ni siasa tu,basi kweli siasa "mchezo mchafu",hufitinisha ndugu na jamaa.Hivi ule ushauri wa Bro Freeman kwenda Hull City kuongeza elimu hukuwa sehemu ya mshauri bwana ZZK pale Hotelin Dar??
Camonnnnn!!Guys come on the round table,yamalizeni haya...kuna maisha nje ya siasa,kuna maisha baada ya siasa..mnatupa wakati mgumu sisi marafiki zenu ambao hatuwezi kutenganishwa nanyi kwa ugomvi wa kisiasa.
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1426023462.022248.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1426023462.022248.jpg
    55.6 KB · Views: 1,821
umeandika kwa hisia sana ndugu, ila nafikiri mtu huvuna anachopanda, pindi wakati wa mavuno ukifika.
 
Ungeweza kabisa kuandika makala yako bila kumuingiza Mama Zitto, Mungu amrehemu.Sio busara leo kuanza kumlisha Marehemu maneno mdomoni.

Kabla hajafa tayari kwenye vyombo vya habari alimshukuru Mungu kwa Zitto kufukuzwa Chadema akiwa mzima.

"NAMSHUKURU MUNGU KWA KUJALIA MWANANGU KUFUKUZWA CHADEMA " HAYA NI MANENO YA MAMA ZITTO

Mama+Zitto+Clip.jpg
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.

“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.

Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”

Katika ufafanuzi wake wa jana, Shida aliwataka wanachama wa Chadema kuwa watulivu kwa maelezo kuwa Zitto hajafukuzwa uanachama, “Siku nyingi walikuwa wanamwinda na hata hilo jambo ambalo Chadema wanasema amefanya, hawana uhakika nalo.”

Juzi wakati akisoma uamuzi wa Kamati Kuu, mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema wamebaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.

Alisema kikundi hicho vinara wake wapo wanne, Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne ambaye alieleza kuwa hajatambulika na anatumia jina la M2.

Mama Zitto ambaye wakati akizungumza na gazeti hili alikuwa amelala kutokana na kusumbuliwa na maradhi alisema kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, kwamba chama hicho walimwondoa Aman Kabourou (aliwahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini-Chadema) itakuwa Zitto, inaonyesha jinsi watu walivyo na chuki na mwanaye.

Alisema tangu siku nyingi ndani ya Chadema kulikuwa na mpango wa kumng’oa Zitto, akifafanua kuwa hata katika kikao cha Kamati Kuu iliibuliwa hoja ya ruzuku za vyama, huku wajumbe wakimshutumu Zitto kwamba kwa nafasi yake na Naibu Katibu Mkuu alitakiwa kuitetea Chadema kuhusu ruzuku.

Katika vikao vya Kamati ya PAC, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akitaka ruzuku kwenye vyama hivyo isimamishwe.

“Zitto alipoingia katika kikao cha Kamati Kuu alishikilia msimamo wake kwamba kama Chadema inachukia ufisadi, nacho lazima kihakikishe kinakaguliwa,” alisema na kuongeza;

“Wao wanaona ili waweze kusalimika katika suala hili la ruzuku ni lazima wamfukuze Zitto. Chadema hawako sawa, hesabu zao haziko sawa.”

Alisema kuwa tatizo lililopo ni kuwapo kwa mkakati wa watu fulani kuiyumbisha Chadema , hivyo kila juhudi zinafanywa ili kukitingisha chama hicho kipoteze mwelekeo.

“Siwezi kusema wamemwonea au hawajamwonea, wao wametumia waraka wa Mwigamba ambao Zitto amekiri katika Kamati Kuu kwamba hajawahi kuusikia wala kuuona, tofauti na Dk Kitila ambaye amesema amewahi kuuona,” alisema na kuongeza;

“Zitto anahusishwa na kitu ambacho Chadema hawana uhakika nacho, ukiusoma ule waraka katika aya ya mwisho umeandikwa hivi, ‘Huyu mtu tunayefikiria awe mwenyekiti hajaoa,

tumshauri aoe akikataa tutafute mtu mwingine’, maana yake ni kwamba waraka huo ulikuwa haujamfikia Zitto, kama ungekuwa umemfikia Zitto watu hao wasingemwomba Zitto agombee uenyekiti.” Alipoulizwa nafasi yake ndani ya Chadema kutokana na yaliyomkuta mwanaye alisema, “Mimi hawawezi kunitengenezea jambo. Hivi Zitto anaweza kuwa mbaya mimi nikawa mzuri.”

Ushauri kwa mwanaye

Alisema kuwa mwanaye ana uamuzi wake na kwamba hata kama Chadema itamfukuza uanachama, haitaweza kumnyang’anya vyeti vyake vya elimu aliyoipata.

“Zitto anaweza kufanya kazi mahali popote duniani, lakini pia ni mwalimu anaweza kuamua kufundisha. Ubunge ni mgawanyo wa madaraka. Watu wote hatuwezi kuwa wabunge,” alisisitiza.

Alisema wakati Kikao cha Kamati Kuu kikifanyika Zitto alikuwa nje ya nchi na kwamba yeye alimshauri kuhakikisha kuwa anahudhuria kikao hicho.

“Alipotua tu na ndege aliniambia kuwa kuna foleni na alitaka kukodi pikipiki ili awahi kikao, aliniambia lazima aende ili kujua hatima yake.

Aliacha gari lake na kwenda na hata mimi nilimsisitizia kwamba ni lazima aende katika kikao,” alisema. Alisema kuwa Zitto alipofika katika kikao hicho aliweza kuzima hoja zote zilizomhusu ikiwamo ya ruzuku za vyama, kwamba baadhi ya wajumbe walipoona amebadili mwelekeo wa kikao, mjumbe mmoja (akamtaja kwa jina) aliibua waraka uliomng’oa Zitto katika wadhifa wake.

“Unajua Kamati Kuu ilijadili zaidi kuhusu ruzuku. Hata ule waraka uliongezwa maneno baada ya baadhi ya wanachama kumpora Mwigamba laptop yake alipokuwa mkoani Arusha katika kikao cha Chadema,” alisema.

Huku akiwataja wanachama wa Chadema walioongeza maneno katika waraka huo (wakiwamo wabunge wawili) na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, mama Zitto alisema kilichomkuta mwanaye ni ushindi mkubwa, kwamba alipangiwa kufanyiwa makubwa zaidi ya yaliyomkuta.

“Hakuna amani maana ukisikia kengele inagongwa hapa nyumbani unasema hao ndiyo wamekuja kumuua Zitto nini, hivi sasa mpaka walinzi wanaolinda hapa wakisikia unakuja nyumbani kwa Zitto lazima wakuandike jina na kukufuatilia,” alisema mama huyo.
 
ZZK akisoma huu ujumbe lazima machozi yamtoke
 
Katiba ya Chadema Ibara ya 8.0.
HATUA ZA KINIDHAMU KWA WABUNGE, MADIWANI,WENYEVITI WA VIJIJI/MITAA NA VITONGOJI

x. CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi nawanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za Chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama.
 
Tatizo ni kiburiiii tu cha kawaida au academic Arrogance!!!Dogo ulijiona mkubwa kuliko chama au kuna mahali mlikoseana?Nenda Zitto nenda,Angalikuwapo Mama yako Shida Salumu angekuombea msamaha wangemuonea aibu na kukurudisha kundini.Asingekubali na hajawahi kukubali kukuona unaiacha Chadema yako.

Mama hayupo tena,hakuna wa kukutetea na kukuombea msamaha...hata Mama nakumbuka tukiwa Tabata Magorofani aliwahi kukuonya kuwa achana na miruzi mingi kumbuka waliokulea na walikokutoa...nakumbuka Bi Shida alitoa machozi tukiwa pale Tabata.Alikuasa kuachana na wanaokupotosha,alisema aliongea kwa kirefu na wazee wa Chama akiwemo Mzee Kimesela na Mzee Mtei,akakwambia na yeye kagundua kuwa umekosea na ujirekebishe,Kwa ushahidi wa namna ulivyouzwa majimbo ya Musoma Vijijini nk,Mama alikuomba sanaaa usirudie wala usishindane na waliokulea,alisema tuache tamaa,tusirubuniwe na vijipesa tukawasahau wenzetu na kuwauza,akasema familia ina heshima ya kuwa waasisi wa Chadema,tusiipoteze historia hiyo.Nakumbuka akasema miaka 20 ijayo mwanetu Chachage Zitto Zubeir Kabwe aje ajivunie uasisi wa bibi na baba ndani ya Chadema

Nasikitika umepuuza ushauri wa mama,Japo ulisema utamuenzi lkn kwa hili hujamuenzi..umemuangusha Mama umemuangusha,angakuwa hai asingekubali uondolewe ktk chama alichojua unakipenda toka ukiwa mtoto,anakumbuka jinsi wakati mwingine alivyokugombeza usome kwanza badala ya kupendelea siasa...Leo mama asingekubali hata kidogooooo ...

Jitafakari Zitto,najua baba yako si sehemu ya washauri wako kisiasa lkn rudi nyuma tazama ulipokosea..Wewe siyo wa kufa kibudu hivyo kisiasa Ndani ya Chadema,Weeee Zitto Zubeir Kabwe!!!????Yaani wakati 2005 Salumu Mwalimu akiwa bado haijui Chadema Wewe ulikuwa ndani ya harakati,2003 wakati Ole Sosopi akiwa shule ya msingi akichunga ndama...wewe ulikuwa kwenye hostel za Chuo kikuu usiku wa manane tena kwa Siri na Mbowe mkipanga mikakati ya kupata wanachama toka Chuo kikuu.

Nakumbuka siku zile za mwisho wa week chuoni...Freeman Mbowe akija Hall kwa gari binafsi usiku wa weekend,akitubeba kwa gari mpaka club billicanas,wakati huo tukimuita brother,kwenda kupoteza mawazo na kurefresh then kuturudisha au wakati mwingine kulala huko huko,tukila chips ndani ya sahani moja,tukipita katikati ya jiji usiku tukishangaa jinsi habari za mitaa ya Ohio tulizosoma magazetini sasa twaziona kwa macho.Ni wapi wewe na brother Freeman mlipotofautiana??Yule Freeman aliyekwambia hata kwa kuiuza Bilicanas wewe lazima ukagombee jimbo la Kgm Kaskazini,Freeman aliyekuwa anakutegemea kwa mambo Mengi leo mmegeukana???kweli siasa mchezo mchafu...yaani urafiki na undugu wenu unavunjika sababu ya tofauti za siasa????

U sometimes used to feel our pocket money kipindi cha miezi dume..ilifikia mpaka Siri za ndani baina yenu mkawekeana bayana!!Ni siasa tu au kuna mengine??Kama ni siasa tu,basi kweli siasa "mchezo mchafu",hufitinisha ndugu na jamaa.Hivi ule ushauri wa Bro Freeman kwenda Hull City kuongeza elimu hukuwa sehemu ya mshauri bwana ZZK pale Hotelin Dar??
Camonnnnn!!Guys come on the round table,yamalizeni haya...kuna maisha nje ya siasa,kuna maisha baada ya siasa..mnatupa wakati mgumu sisi marafiki zenu ambao hatuwezi kutenganishwa nanyi kwa ugomvi wa kisiasa.

View attachment 233609View attachment 233610View attachment 233611View attachment 233614View attachment 233615

Imenitia uchungu mimi km mzazi. Nimemkumbuka mama yangu rip na mana wa zzk (rip). Tusikie yale tunayoshauriwa na wazazi wetu. Zito akisoma hii atalia sana kumlilia mama sana. Lakini hayupo tumuombee tu. Kakiangukia chama kwa niaba yake km yupo tayari kujirudi. Amesahahu chama kimeshika mpini na yeye kashika kwenye makali?
 
Pole zako Zitto kwa kukubali kurubuniwa na Mwigulu Nchemba. Ndo imetoka hivyo!

-----------NI Tafakari nzuri sana umeifanya mwanakwetu,kwenye maisha hakuna adui wa kudumu wala rafiki. Yahitajika unyenyekevu na roho isiyo na majivuno kuyatenda kwa ukamilifu wake yote uliyonena. Nami naamin walengwa na sisi hadhira tunayo sababu ya kurejea bandiko hili katika kupata suluhisho la kudumu.
 
Mtoa mada umeongea kwa hisia mpaka umenigusa... Lakini kabla ya yote nimefanya tafakuri kidogo juu ya Zitto Kabwe na mazongezonge yanayomzunguka..

Tatizo Zitto amejawa kibuli na dharau.. Hakuna ubishi kwamba alipewa fedha na nyoka wa Serikali kwa lengo la kumwezesha kugombea Uwenyekiti wa chama. Lakini sijui kwa makusudi au hakujua lengo la hawa nyoka.. Nyoka waliamini kabisa Zitto akigombea Uwenyekiti atatikisa misingi na uhai wa CHADEMA.. Hata kama angekosa, CHADEMA ingeachwa vipande vipande..!! Ndiyo maana hata baadhi ya Mawaziri kama Wassira waliamini kabisa ndiyo mwisho wa CHADEMA mpaka kudiriki kusema CHADEMA inakufa 2014..

Pongezi za kipekee ziende kwa Idara ya Usalama ya CHADEMA.. Hawa jamaa wanatakiwa wapewe heshima na pongezi zinazostahili.. Idara hii imekuwa ndiyo kama moyo wa chama kwa sasa.. Wanafanya kazi zao kwa ueledi, uvumilivu na moyo wa kizalendo kulinda maslahi si ya chama tu bali ya taifa kwa ujumla. Waliweza kufanya udukuzi na kupata taarifa zote za mipango dhalimu ya kina Zitto Kabwe.

Kwa mtu mwenye akili timamu,, Zitto angetumia muda ule kukubali na kutubu kosa... angeweza hata kuwaomba wazee wamwombee msamaha ili chama kimsamehe.. Lakini kwa kibuli na dharau akapigwa upofu na akawa bado anaamini kwamba yeye ni mkubwa kuliko chama na bila yeye hakuna CHADEMA.. Akajazwa kibuli na wapambe waliokuwa hawamtakii mema.. Mkutano na waandishi wa habari aliouitisha ulipigiwa debe na kusimamiwa na makada wa CCM (Mwampamba, shoza na wenzake) waliofukuzwa CHADEMA kwa makosa ya kuhujumu chama..

Akiungwa mkono na CCM akafanikiwa kwenda mahakamani kuokoa ubunge wake... Lakini kwa kuwa amejawa na kiburi na tamaa za uongozi uliopitiliza akahusishwa na kuanzishwa kwa chama cha ACT na kuendelea kuhonga baadhi ya makada wa CHADEMA mikoani kujitoa uanachama, kuzomea na kuhujumu shughuli za chama. Rejea zomeazomea ya vijana wa ACT kwenye mkutano wa Dr. Slaa Kigoma.. Pili akawa anatumia PAC kujijenga upya kisiasa... Mfano ni kukomalia sakata la Escrow na kashfa zingine lakini akasau kuwa kuchokonoa ESCROW ni kuigusa CCM moja kwa moja pamoja na muhimili wa Mahakama..

CCM wakagundua kuwa malengo yao ya kumsaidia Zitto ili akihujumu CHADEMA yamekwama... Mbaya zaidi kwa kutumia PAC kuirarua Serikali ambacho ilikuwa ni neema kwa CHADEMA na UKAWA kupata jukwaa jingine la kujijenga kisiasa.. Naamini kabisa maamuzi ya Mahakama kuu yanamsukumo na sakta la Escrow.. kama CCM ingeridhika na hujuma za Zitto dhidi ya CHADEMA hii kesi ingepigwa danadana mpaka muda wa Ubunge upite.. Mfano kesi ya Hamad Rashid Mohamed hatujui hata muendelezo wake.. lakini ipo kimya kwa sababu CCM wanafufaika kupitia Hamad Rashid

Matokeo yake Zitto amekuwa mzigo kwa CCM na wameamua bora wamuache afe na zigo lake maana madhara yake ni makubwa kuliko faida.!!

Ukiangalia kisiasa CHADEMA ndiyo washindi wa jumla,, CCM na ZITTO wamepoteza.

Kwa kweli bado tunamhitaji katika siasa za Tanzania nimwombe atulie, kama anaweza kuomba radhi afanye hivyo ili arudi kundini...

Tanzania bado inamhitaji!!
 
Its very sad...lakni ndio ivo Kiburi si maungwana...Na sikio la kufa halisikii dawa
 
Tatizo la chadema ni wakuja wakina lissu na lema. Hao ndio wanaaminiwa na Mbowe siku hizi
 
Katiba ya Chadema Ibara ya 8.0.
HATUA ZA KINIDHAMU KWA WABUNGE, MADIWANI,WENYEVITI WA VIJIJI/MITAA NA VITONGOJI

x. CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi nawanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za Chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama.

Je imekaa sawa hii? Au ndio kuminya demokrasia?
 
Mimi naamini ZZK ingawa amechelewa atafanya yale aliyoyafanya Kafulila ili arudi kwenye chama. Asipofanya hivyo ataishia kuwa kama yule wa CUF ambae credibility yake kisiasa imebakia kuwa mtumwa wa CCM.
 
Tatizo la chadema ni wakuja wakina lissu na lema. Hao ndio wanaaminiwa na Mbowe siku hizi

Hivi niwaulize nyinyi misukule ya Lumumba aka buku 7 mnalipwa vile mnavyochangia au mnalipwa malipo ya kwa siku maana kila mada mpo halafu cha maana mnachochangia hakuna zaidi ya kukashifu watu tu na kuharibu uzi.hebu jamani tulieni kidogo basi Mods hebu watazameni hawa watu wanaliharibu hili jukwaa inaonekana wote ni watoto humu watu makini wanalikimbia hili jukwaa jamani hawa vijana watazamwe kwa jicho la tatu
 
Zito amekua akiijenga chadema kumfukuza itawacost sana hata leo akiludi jimboni kwake atapata ubunge kwa chama kingine ishu sio ubunge ishu ni zito kuijenga chadema mimi ni CCM ila i can see CHADEMA is dying soon chadema itakua kama UDP kwa umaarufu mark my words na huu mtego umesukwa vizuri sana na mabere marando yule jamaa ni usalama hawa jamaa huwa hawaachi kazi hadi wanakufa
 
Back
Top Bottom