" Akiingia madarakani anaweza kutumia siku tano za kazi kwenda kuomba ushauri kwa Marais waliomtangulia; Jumatatu atakwenda kwa Dr. Salmin Amour, Jumanne kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi, Jumatano kwa Ben Mkapa, Alhamisi kwa Dr. Aman Karume na Ijumaa atamalizia kwa Jakaya Kikwete.
Naam, inahusu kukua kwa demokrasia na umuhimu wa viongozi kuwa na utayari wa kustaafu uongozi na kuwapisha wengine. Kwamba wakabaki kuwa washauri.
Ona kwa Mugabe na Zimbabwe ya sasa, ni ukweli, kuwa Zimbabwe ya sasa, mbali ya Mugabe, haina Mzimbabwe mwingine yeyote mwenye uzoefu wa kuongoza dola.
Rais ajaye wa Zimbabwe akiingia madarakani baada ya Mugabe kufia madarakani, basi, hatakuwa na uzoefu wa kuongoza dola, na atakapohitaji ushauri, itabidi apande ndege kwenda nchi nyingine, na akija Tanzania atakutana na Marais wastaafu wasiopungua sita!
Na 'Typical Africanity' ni nini?
Ndugu zangu,
Profesa Ayite anasema; " Ni hali ya kiongozi wa Kiafrika kuhofia kuandaa mrithi kwa hofu ya kufunikwa kisiasa". - Prof Ayite.
Hivyo basi, tunaona hapa, kuwa dhana ya balance of power inakosa maana. Na hili ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi za Kiafrika. Si kwenye uongozi wa nchi tu, hata kwenye uongozi wa vyama na taasisi.
Ona Mandela, katika uhai wake , mbali ya yeye kustaafu Urais, ameshuhudia Rais mmoja mstaafu kutoka Chama chake cha ANC. Mugabe hatarajii kuitwa ' Rais Mstaafu' maana atafia madarakani.
Kwamba tangu Aprili mwaka 1980 unaongoza nchi bila kumshuhudia Rais mwingine akiongoza nchi hiyo hiyo, nacho ni kipimo cha udhaifu wa uongozi.
Maana, kwa Zimbabwe, kuna waliozaliwa na kumkuta Mugabe madarakani, nao wamepata watoto, na watoto nao wamepata watoto na kumkukuta Mugabe madarakani.
Ni ukweli, Zimbabwe ya sasa, mbali ya Mugabe, haina Mzimbabwe mwingine yeyote mwenye uzoefu wa kuongoza dola.Typical Africanity!
Inasikitisha.
Maggid Mjengwa.
Iringa.