Tafadhali Usininukuu; Rais Ajaye Wa Tanzania...!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
" Akiingia madarakani anaweza kutumia siku tano za kazi kwenda kuomba ushauri kwa Marais waliomtangulia; Jumatatu atakwenda kwa Dr. Salmin Amour, Jumanne kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi, Jumatano kwa Ben Mkapa, Alhamisi kwa Dr. Aman Karume na Ijumaa atamalizia kwa Jakaya Kikwete.

Naam, inahusu kukua kwa demokrasia na umuhimu wa viongozi kuwa na utayari wa kustaafu uongozi na kuwapisha wengine. Kwamba wakabaki kuwa washauri.

Ona kwa Mugabe na Zimbabwe ya sasa, ni ukweli, kuwa Zimbabwe ya sasa, mbali ya Mugabe, haina Mzimbabwe mwingine yeyote mwenye uzoefu wa kuongoza dola.

Rais ajaye wa Zimbabwe akiingia madarakani baada ya Mugabe kufia madarakani, basi, hatakuwa na uzoefu wa kuongoza dola, na atakapohitaji ushauri, itabidi apande ndege kwenda nchi nyingine, na akija Tanzania atakutana na Marais wastaafu wasiopungua sita!

Na 'Typical Africanity' ni nini?

Ndugu zangu,

Profesa Ayite anasema; " Ni hali ya kiongozi wa Kiafrika kuhofia kuandaa mrithi kwa hofu ya kufunikwa kisiasa". - Prof Ayite.

Hivyo basi, tunaona hapa, kuwa dhana ya balance of power inakosa maana. Na hili ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi za Kiafrika. Si kwenye uongozi wa nchi tu, hata kwenye uongozi wa vyama na taasisi.

Ona Mandela, katika uhai wake , mbali ya yeye kustaafu Urais, ameshuhudia Rais mmoja mstaafu kutoka Chama chake cha ANC. Mugabe hatarajii kuitwa ' Rais Mstaafu' maana atafia madarakani.

Kwamba tangu Aprili mwaka 1980 unaongoza nchi bila kumshuhudia Rais mwingine akiongoza nchi hiyo hiyo, nacho ni kipimo cha udhaifu wa uongozi.

Maana, kwa Zimbabwe, kuna waliozaliwa na kumkuta Mugabe madarakani, nao wamepata watoto, na watoto nao wamepata watoto na kumkukuta Mugabe madarakani.

Ni ukweli, Zimbabwe ya sasa, mbali ya Mugabe, haina Mzimbabwe mwingine yeyote mwenye uzoefu wa kuongoza dola.Typical Africanity!
Inasikitisha.

Maggid Mjengwa.
Iringa.
 
nani anataka rais wa kuomba ushauri na misaada,kwani hawezi ku implement strategy zake??????wabongo ovyo kweeeeli kweli
 
kama kuna rais hajawahi kuomba ushauri hapa dunian basi huyo hafai.misaada umeongeza mwnywe!
 
Vipi ndugu? Wewe ni mwanahabari mzuri inakuwaje leo unatoa habari isiyoeleweka?
Huyo ndio Maggid- mwandishi huru kama anavyojipambanua japo mtu huru huwa siku zote hafinyangi maneno na hufikisha ujumbe ulionyooka na kwa uwazi zaidi lakini si Maggid,huwa anaandika kinadharia mara nyingi na kufinyanga maneno na katika bandiko hili pia kafanya na ukiangalia main subject sio urahisi na Mugabe bali hiyo ni core-subject,tuliozoea maandish ya Maggid wala hatubati tabu!!!
 
!
!
halikadhali Tanzania,kuna watu wamezaliwa wameikuta ccm madarakani,wamezaa watoto wao pia wakakuta ccm madarakani,watoto ndo wamezaa watoto wao pia bado ccm iko madarakani......na bado inaleta fitina iendelee kuwa madarakani, vipi hii sio africanity mkuu?
 
nani anataka rais wa kuomba ushauri na misaada,kwani hawezi ku implement strategy zake??????wabongo ovyo kweeeeli kweli

perfect ukipenda kudesa kila kitu maana yake wewe nimasikini wa kufikiri na hufai kuongoza . kwani mandela alidesa kwa nani ?? na je huyo Mugabe unayemzungumzia wewe alidesa kwa nani??? BE innovative that's all about leadership.
 
nani anataka rais wa kuomba ushauri na misaada,kwani hawezi ku implement strategy zake??????wabongo ovyo kweeeeli kweli

Yaani rais ajaye akaombe ushauri kwa Salmin aliyesaidia kuua watu wa Pemba kisa kudai Demokrasia? pi aende kwa Mwinyi na kuomba ushauri kwa mtu aliyeuza kipande cha ardhi yetu kwa waarabu wa Loliondo ambao wanatesa mpaka leo? au ushauri utoke kwa mkapa aliyeuza nyumba za serikali kwa bei chee na kisha kufanya biashara akiwa IKULU? AU aende kwa Karume aombe ushauri kwa mtu anayeshabikia muungano uvunjike? mtu ambaye baba yake alisimamia eti upoteaji wa akina Hanga? na mwisho ijumaa baada ya masjid aende kwa JK huyu anayelinda ufisadi kwa hali na nguvu zake zote,? mtu anayefinya demokrasia kwa kuweka bajeti kubwa kuua vyama vya upinzani? mtu asiyeweza kukamata wale wote waliohusika na utesaji wa raia, Waliouwa mkutanoni Morogoro, Waliouwa Iringa, waliotupa mabomu Arusha kisha kuwapandisha cheo wahusika wote?

Majjid acha kutukumbusha machungu bana na ni bora tukaangalia mbele kuliko kuangalia tulikotoka au bora ungesema tuanze upya toka pale alipoachia Nyerere na sio hao watu wako

Ushauri wako ni sawa na kumshauri Rais wa Africa kusini wakati Mandela akiwa hai eti akaombe ushauri kwa "Botha" na sio kwa Mandela
 
Huyo ndio Maggid- mwandishi huru kama anavyojipambanua japo mtu huru huwa siku zote hafinyangi maneno na hufikisha ujumbe ulionyooka na kwa uwazi zaidi lakini si Maggid,huwa anaandika kinadharia mara nyingi na kufinyanga maneno na katika bandiko hili pia kafanya na ukiangalia main subject sio urahisi na Mugabe bali hiyo ni core-subject,tuliozoea maandish ya Maggid wala hatubati tabu!!!

Ee Bw. ndiyo umenisaidia kujua mfinyazi anavyofinyanga habari, na kutumia ID nyingine kuona watu wana akili ndogo, nilitaka kujua au ametumia siku za wiki kuonesha muda wote alioutaja atakuwa anashauriwa tu, je akili yake ataitumia lini?
 
" Akiingia madarakani anaweza kutumia siku tano za kazi kwenda kuomba ushauri kwa Marais waliomtangulia; Jumatatu atakwenda kwa Dr. Salmin Amour, Jumanne kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi, Jumatano kwa Ben Mkapa, Alhamisi kwa Dr. Aman Karume na Ijumaa atamalizia kwa Jakaya Kikwete.

Naam, inahusu kukua kwa demokrasia na umuhimu wa viongozi kuwa na utayari wa kustaafu uongozi na kuwapisha wengine. Kwamba wakabaki kuwa washauri.

Ona kwa Mugabe na Zimbabwe ya sasa, ni ukweli, kuwa Zimbabwe ya sasa, mbali ya Mugabe, haina Mzimbabwe mwingine yeyote mwenye uzoefu wa kuongoza dola.

Rais ajaye wa Zimbabwe akiingia madarakani baada ya Mugabe kufia madarakani, basi, hatakuwa na uzoefu wa kuongoza dola, na atakapohitaji ushauri, itabidi apande ndege kwenda nchi nyingine, na akija Tanzania atakutana na Marais wastaafu wasiopungua sita!

Na 'Typical Africanity' ni nini?

Ndugu zangu,

Profesa Ayite anasema; " Ni hali ya kiongozi wa Kiafrika kuhofia kuandaa mrithi kwa hofu ya kufunikwa kisiasa". - Prof Ayite.

Hivyo basi, tunaona hapa, kuwa dhana ya balance of power inakosa maana. Na hili ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi za Kiafrika. Si kwenye uongozi wa nchi tu, hata kwenye uongozi wa vyama na taasisi.

Ona Mandela, katika uhai wake , mbali ya yeye kustaafu Urais, ameshuhudia Rais mmoja mstaafu kutoka Chama chake cha ANC. Mugabe hatarajii kuitwa ' Rais Mstaafu' maana atafia madarakani.

Kwamba tangu Aprili mwaka 1980 unaongoza nchi bila kumshuhudia Rais mwingine akiongoza nchi hiyo hiyo, nacho ni kipimo cha udhaifu wa uongozi.

Maana, kwa Zimbabwe, kuna waliozaliwa na kumkuta Mugabe madarakani, nao wamepata watoto, na watoto nao wamepata watoto na kumkukuta Mugabe madarakani.

Ni ukweli, Zimbabwe ya sasa, mbali ya Mugabe, haina Mzimbabwe mwingine yeyote mwenye uzoefu wa kuongoza dola.Typical Africanity!
Inasikitisha.

Maggid Mjengwa.
Iringa.

Tupenadhalia yako juu ya CCM kukaa madarakani kwa muda wa miaka 50 bila kuona haja ya kubadilishana na chama kingine.
 
meseji sent and probably delivered.
 
Naona maggid anataka kuwachokoza wafuasi wa Mbowe hapa!!

Wameshachokozeka.

Mtu akikaa madarakani miaka 10 na ameshindwa kufanya revolutionary change, hata akiongezewa miaka mingine 30 hakuna la ajabu atakalofanya. Mtu huyo anakuwa tayari ameshatengeneza utamaduni ambao watu anaofanya nao kazi wameuzoea na kujirekebisha kuendana nao. Ndio maana baada ya miaka 10 madarakani (serikalini au kwenye chama cha siasa au taasisi nyingine) kiongozi hana tena uwezo wa kufanya mabadiliko ya makubwa.
 
Maggid sijui kwamba amemsahau mzee wetu Aboud Jumbe au ndio mambo ya "outlaw".

Kikwete amekuwa akimtembelea mzee Jumbe kwa "mazungumzo". Anao uzoefu na taarifa muhimu sana zinazoweza kumsaidia kiongozi aliye madarakani kufanya maamuzi sahihi...
 
Vipi umeshapiga kura kupunguza aibu ya mmeo zitto? Naona mpo 59 tu. Accounts zako zote zimeunganishwa. Akili mavi
 
Mi naona Jongwe na Zimbabwe wako sawa tu. Kila nchi duniani ina staili yake na version yake ya uongozi,whatever that works for them, is right for them, mradi wananchi wengi wameridhia staili hiyo. Hivi unaeza kusema honestly hiyo 'demokrasia' yetu hapa Tz ina edge ipi over dictator Mugabe au Kagame? 'demokrasia' gani isiyozaa maendeleo wala utawala wa sheria? #nonsense
 
Back
Top Bottom