Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Ninawasihi sana watu wa Tume kuhakikisha matokeo yaanza kutoka mapema jamani. Asubuhi inakuja, watu wanaamka hakuna matokeo, mnawapa wasiwasi na kuanza kutengeneza tension, mtaleta polisi na kujaribu kuwatawanya, mtawaumiza watu please. Au mtu atoke na kuzungumza na wananchi msiache tetezi na uvumi kujengeka. Pleaseeeeee! Liacheni litakalokuwe liwe.
Hali hii ya wasiwasi inazidi kuongezeka na si ya lazima kabisa. Na mtu ambaye asizungumzie hili kwa sasa ni Rais Kikwete au viongozi wa kisiasa mtasababisha manung'uniko yasiyo ya lazima, naomba chonde chonde, mwamko uliopo na hisia zilizopo sasa zitatupeleka pabaya. Tume iamke mapema iwezekanavyo kuwatuliwa wananchi hasa vijana ambao baadhi ya maeneo wameanza kuonesha kupoteza utulivu.