Elections 2010 Tafadhali Jaji Makame zungumza na wananchi mapema, kuondoa wasiwasi Please!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Ninawasihi sana watu wa Tume kuhakikisha matokeo yaanza kutoka mapema jamani. Asubuhi inakuja, watu wanaamka hakuna matokeo, mnawapa wasiwasi na kuanza kutengeneza tension, mtaleta polisi na kujaribu kuwatawanya, mtawaumiza watu please. Au mtu atoke na kuzungumza na wananchi msiache tetezi na uvumi kujengeka. Pleaseeeeee! Liacheni litakalokuwe liwe.


Hali hii ya wasiwasi inazidi kuongezeka na si ya lazima kabisa. Na mtu ambaye asizungumzie hili kwa sasa ni Rais Kikwete au viongozi wa kisiasa mtasababisha manung'uniko yasiyo ya lazima, naomba chonde chonde, mwamko uliopo na hisia zilizopo sasa zitatupeleka pabaya. Tume iamke mapema iwezekanavyo kuwatuliwa wananchi hasa vijana ambao baadhi ya maeneo wameanza kuonesha kupoteza utulivu.
 
Siku zote hapa ndiyo chaguzi za Africa huanza kuwa na utata! Nilitegemea tume watakuwa laiv on TV tukiwaona wanafanya nini na wakitoa updates say kila baada ya nusu saa!

Anywayz ushauri wako MM ni muhimu sana kuavoid unnecessary tensions and possibly injuries
 
kwa sababu Nyambala unajua Dr. Slaa akija Dar sasa hivi, hapatakalika hapo? Saikolojia ya mob inapoanza kupanda msishangae tu yatakayotokea.
 
kwa sababu Nyambala unajua Dr. Slaa akija Dar sasa hivi, hapatakalika hapo? Saikolojia ya mob inapoanza kupanda msishangae tu yatakayotokea.

That is absolutely true na mbaya zaidi muungwana akajitokeza say kukemea fujo, yaani hawa jamaa maeneo kama haya ndiyo huwa wanaprove they are not for the pple!

Tume haina email active? we can send this to them!
 
Ni kweli. Tume ikikaa kimya wananchi wanaweza kudhani imekwenda Ikulu kujadiliana na Rais namna ya kufanya, kama ilivyokuwa Kenya.

Ni vema Tume ikaonekana inafanya nini mpaka uchaguzi ukamilike.
 
Matokeo yalianza kukosekana tangu jana. Huu ni upuuzi wananchi wamepiga kura wanahitaji majibu mambo ya ujambazi yamepitwa na wakati leteni matokeo hili ni jambo muhimu hivi sasa kuliko kitu chochote kile.
 
WATCHDOGS wetu wawe alert na mawasiliano yanayoingia na kutoka NEC maana I smell a RAT.

Mwanakijiji, unajua msemaji mkuu ni aliyekuteua hivyoa lazima akupangie what to say and where. Makame anasubiri maelekezo kutoka kwa manunda wachache wa TISS waliopandikizwa na ccm. Ila sisi wananchi hatutapenda aina yeyote ya UHAINI.

Mungu inusuru tanzania
 
Tume ya Kikwete... What do u expect? A reliable source told me kwamba kuliko kumruhusu Slaa kwenda ikulu, ni bora wakabidhi nchi kwa jeshi ili wakae kwa amani!!
 
Hapa ndipo tume yetu inapobidi itumie busara!!! Kukaa kimya wakati kuna majimbo ambayo yamekwishatoa matokeo ni kuleta hisia mbaya!!
Wanapaswa kutangaza kadri majibu yanavyowafikia ili kuleta imani juu ya tume!!

Ni kweli kuwa hawa jamaa wako tayari tu nchi iparaganyike kuliko Slaa kuingia, ijumaa nilikuwa na makada fulani, yaani wanabisha bila ya sababu ya kubisha, sababu zao ni za kijinga sana!!!:peace:
 
Brazil wako masaa kadhaa nyuma yetu wao tayari matokeo nje nje sisi bado kajinamizi ka Chama Cha Majambazi kanafikiria kanaweza kusimamisha nguvu ya umma.
 
Nia ya kuahirisha baadhi ya maeneo ni kupisha mwanya wa kuweza kuyachakachua vizuri kuweni macho. Kama ni kukaza ni kukaza tuu .Mwanzo mwisho hawa jamaa wameprove failure kabisa. https://jamii.app/JFUserGuide you Kiravu ....(Hata mkini-ban I don't care)
 
Hapana.. matokeo ya Ubunge karibu yote yatajulikana leo.. ya Rais kwa uhakika yatakuwa tayari ifikapo Jumanne! NImeshangaa tume inatumia teknolojia kwenye kuhesabu kitaifa (which they could just use a calculator) na hawakutumia teknolojia kukusanya matokeo.
 
Back
Top Bottom