Tabu Ley afariki

Tabu Ley afariki

Huo wimbo alikuwa anaupiga sana Uncle J. Na sasa hivi Gamba Muyenjwa. Nitaupataje huu wimbo?

Mkuu hata mimi nautafuta. Nimejaribu kutafuta kwenye you tube hamna kitu kwa kuwa jina lake halisi silijui. Ukifanikuwa kuupata nishtue.

Tiba
 
R.I.P Tabu Ley. Wimbo wake ambao sitausahau ni 'I LOVE YOU BABY TOUCH ME'
 
Kuna wimbo wake Sacramento naupenda sana. Kila ninapoupiga unanikumbusha ujana wangu nikiwa Mwalimu. Tulikuwa na kijoint fulani jioni tukienda kula nyama choma, kupata kinywaji na kusikiliza muziki Congolee. A prolific music writer indeed. Kusikia kafariki roho imeniuma sana jamani mwenzenu. Naona nitapiga sana huu wimbo iwe njia yangu ya kuomboleza Tabu Ley. Sacramento, Sango Lamu.... Lakini pia nazipenda nyimbo zake Mokolo nakokufa, Felly Mour, na zile nyimbo nyingine aliimba kipindi chake na Mbilia Bel. RIP mwana wa Afrika. Tulikupenda sana...lakini Mungu kakupenda Zaidi.
Ooops! Mkuu Highlander, umenikumbusha mbali, umenikumbusha jamaa yangu ambaye alipenda sana kusikiliza wimbo wa Sacramento akitumia kiredio chake aina ya Memory Que. APEPE Tabu Ley!
 
Last edited by a moderator:
Ooops! Mkuu Highlander, umenikumbusha mbali, umenikumbusha jamaa yangu ambaye alipenda sana kusikiliza wimbo wa Sacramento akitumia kiredio chake aina ya Memory Que. APEPE Tabu Ley!

ha ha ha ha...bado unazikumbuka Memory Que. Ni kama zilikuwa Made in China vile?
 
Back
Top Bottom