Tabora yangu Tabora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabora yangu Tabora

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpevu, Jan 23, 2012.

 1. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,817
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mji wangu mkongwe wa Tabora,
  Wewe ndio chimbuko la vuguvugu la uhuru wa Tanganyika,
  Ndio mji mkubwa wa kwanza hapa Tanganyika enzi za ukoloni,
  Leo umesahaulika mkoa wangu Tabora,
  Sijui ni nani amekupoteza Tabora yangu,
  Umezalisha wasomi na wazalendo wengi Tabora yangu,
  Hukujipendelea kwa kujipendelea mkoa wangu Tabora,
  Leo unaonekana ni mkoa ulio mwishoni kabisa,
  Hata sherehe za miaka 50 hujakumbukwa na kupewa nishani kwa harakati zako Tabora,
  Akina Fundikira na Kasangatumbo walikiona cha moto japo walipigania uhuru,
  Tabora mji wangu wee...leo umebakiwa ni magofu,
  Utalii haushamiri, japo fursa za historia zipo,
  NANI KAKUPOTEZA TABORA WANGU,
  Umezalisha viongozi lukuki, lakini wamekusahau Tabora,
  Leo miundombinu hafifu, shauri ya kukuikomboa Tanganyika,
  Nani atakukumbuka Tabora, iwapo hata nishani za uhuru hukupata,
  Umejaaliwa ardhi rutuba, misitu na wanyama pori,
  Wajanja wanakutafuna Tabora, na kukuachia jangwa bila maendeleo
  AMKA TABORA AMKA, NAWE UONJE KEKI YA TAIFA.
  Umeibeba historia ya nchi, lakini miaka 50 huthaminiwi.
  Umeletewa Sanamu, na uwanja wa mpira usiokamilika,
  Barabara hazipitiki, ndio leo wanaamka kukutengenezea barabara baada ya miaka 50,
  Si reli wala ndege, barabara ndio tegemeo,
   
 2. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 604
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tabora ndo alitoka mbongo wa kwanza kwenda unyamwezini wacha weee
   
 3. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,107
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Wenyeji walishajikatia tamaa, wengi ukiwauliza wanakwambia "haya ndio majaaliwa yetu". (Eshene sisi kwa lahilizwa) na ndio maana wanachagua watu kama Rage (ingependeza na ingeendana na tabia zake kama jina lake lingekuwa RAG) kuwa wabunge.
   
 4. Mboka Manyema

  Mboka Manyema Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ahhhh Mboka Manyema...
   
 5. Fighter

  Fighter JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu na kupm!
   
 6. s

  sikiolakufa JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I was born there but I will never set my foot there...wachawi wizi wazinzi..mji mbaya kabisa ilaaniwe tabora
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,639
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  likataa kwao ni nilitumwa by wahenga..
   
 8. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 3,568
  Likes Received: 1,955
  Trophy Points: 280
  Tatizo la tabora ni aina ya watu iliyonao....huu ni ukweli unaouma!
   
 9. s

  sikiolakufa JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mazinzi mana tabora...matoborwa ku.....make
   
 10. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ipunda yafa, mligo gwafika!
   
 11. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,548
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  I love my tabora and freedom is coming. Usjali koz nimezaliwa hapo milambo baracks na isevya cheo, kiloleni, mihogoni, ng'ambo, kanyenye ,mwinyi etc ndo vitaa vyangu" so doncare tabora bkoz SHARD and CHADEMA will b ur saviour.
   
 12. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Tabora haina tatizo, tatizo ni kwa watu ambao NEC huwa wapatia, Just imagine SITA, KAPUYA, Eng Msekela, Tatu ntimizi, Mfutakamba,Rage, Kaboyonga, Mgombero, Nk. Sijaona kiongozi hata mmoja hapo. Kapuya alikuwa waziri tangu mimi nipo Darasa la kwanza takriban miaka 25 iliyopita, miezi miwili iliyopita nilikwenda urambo yaani ukiimaliza milambo secondary ndio mwisho wa lami, achilia mbali yule jamaa anaejiita SELELI, yaani ukiimaliza ipuli basi mpaka unapofika Tanesco Nzega ndio unaona kipande cha lami,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,La mwisho madogo hawapendi kufanya kazi, masela wanakaa vijiweni san, wanywa kahawa sana, na wacheza bao, so maendeleo ya wana TABORA yataletwa na wageni.
   
 13. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Mkuu, mbona umekasirika hivyo, ama hujui maji hata yakichemka kuwa mvuke ni lazima yatarejea hali yake ya umaji. Ni sisi wenyewe watu wa Unyamwanga, Unyanyembe 'Kulugo' ndio tutakaoikomboa Tabora yetu.

  Kuna mipango mizito sana inaendelea kuratibiwa ili kuuweka mkoa wetu mzuri kwenye ramani ya Maendeleo na Demokrasia iliyotukuka. Wewe na wana JF wengine mmejaaliwa kuwa na access na mitandao yenye kukutanisha maelfu ya watu na wenye uwezo wa kujadili mambo nyeti kama hili, katu usikate tamaa. Uchawi na ujinga wa wakazi wa Tabora ni zao la serikali yetu kupiga siasa hadi vilioni.

  Rage alichaguliwa si kwa mapenzi halisi bali ni kwa hujuma na Tabora kukosa wagombea makini na wazawa wenye uzalendo. Tabora ndugu yangu imecheleweshewa elimu ya uraia na hivyo wakazi wake walikuwa wamelala usingizi wa pono. Twende tu kwetu Mboka Manyema tukawaelimishe Wanyamwezi tukiwaambia 'Mtunule kwasyaga' yaani amkeni kumekucha. Nashukuru vyuo vikuu binafsi vimeanza kupelekwa Tabora ili tu watu wa huko nao wapate elimu bora kwa ukombozi wao mmoja mmoja, jamii na mkoa mzima. Tushikane tu tusaidie, usiuchukie ukweli, tafuta namna ya kuuhubiri ukweli ili siku moja tuimbe wote wimbo wetu wa 'matunda ya mji mzuri mji ambao babu na babu zao kabla yao waliishi kwa upendo na umoja.

  Hizi ni salaam kwa Rage na mabwenyenye wote. Siku ipo inakuja.

  Ni mimi,
  Pangu Pakavu,
  Nawasalimia.
   
 14. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu badala ya kulalamika sana kuhusu mkoa wako kuwa nyuma karibu ktk sekta zote takribani miaka 50 ya uhuru, unadhani nini kifanyike? Nadhani ni mkoa pekee ambao kiunganishi kati ya Makao makuu ya mkoa na wilaya zake zote, Nzega, Sikonge, Igunga, Urambo, Kaliua na Wilaya mpya ya Uyui bado ni barabara za vumbi! What are some possible solutions to the problem? What efforts should be made to rescue Tabora region?
   
 15. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwenu ni kwenu tu, hata kama ni pangoni mkuu.
   
 16. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kaka tuliza, kuna mkakati underway mkuu, Tabora kitaeleweka tu. Tuko njiani tunakuja, ukombozi umewadia Unyamwezini, tega sikio utaskia sauti za mashujaa wa Unyanyembe wakiunguruma kama simba wa Ipembampazi, tega usikie akina mama, vijana na wazee wetu wanavyoshangilia ukombozi wao, tuko njiani baba tunakuja....

   
 17. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huo ndio ukweli wenyewe kuhusu Tabora! Uswahili mwingi. Kamuulize Tumaini Eli Kiweru yaliyo mkuta alipokuwa RC mkoani Tabora miaka ya nyuma.
   
 18. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Worthy!!!!
   
 19. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Mtakatifu Kayagila taratibu tafadhari, usiwakosee heshima mashujaa wa unyanyembe, watakucharaza bakora bana...
   
 20. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Siyo venevyo mhenga, kwizile mkulu wane, ikalaga tayari nyanda kwizile. Yaani tunakuja comrade, tunakuja mkuu wangu, kaa tahari kijana tunakuja. Ukombozi umefika, ninachohitaji ni ushirikiano wenu, muda si muda nitatoa picha na jina langu ili tuwe pamoja katika mtanange, tuko karibu baba...

   
Loading...