Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
hayo mambo ya hapo penye bold, nadhai kwenye kampeni za 2010 waliyafafanua vya kutosha, ulisoma chapisho lao la ilani?

Dada judi usipate shida na watu kama Agy, hoja zake tayari zipo hasi kuhusiana na chadema.

Ila safi,tushichoke kuwakumbusha hata pale watakapoamua kujitoa ufahamu.
 
Kufafanua hakutoshi, kinachotakiwa ni utekelezaji. Wametekeleza lipi toka uchanguzi umalizike? au wanasubiri tena uchaguzi ndio waanze kukremisha watu mapambio?

lakini mpendwa, kumbuka kuwa walioshinda na kuunda serikali ni ccm, hawa ni wapinzani walio nje ya serikali, sasa mipango yao watatekeleza vipi? hata halmashauri wanazoongoza ziko chini ya tamisemi (na ultimately waziri mkuu) ambayo ni wizara inayoongozwa na ccm, ukiangalia mamlaka ya waziri wa tamisemi kisheria utagundua kuwa hata wakiongoza halmashauri, hawataweza kufanya mambo makubwa sana kwa sababu waziri atawafunika. recall halmashauri ya tarime waliyoiongoza kwa muda mrefu, walimudu kulipia watoto karo tu kutokana na chanzo kimoja tu cha mchango wa mgodi wa north mara kwa halamshauri (amabyo nadhani ni around 200m kwa mwaka!) na machache mengine ila mengi hasa yanayotegemea sapport ya serikali kuu yalikwama
 
lakini mpendwa, kumbuka kuwa walioshinda na kuunda serikali ni ccm, hawa ni wapinzani walio nje ya serikali, sasa mipango yao watatekeleza vipi? hata halmashauri wanazoongoza ziko chini ya tamisemi (na ultimately waziri mkuu) ambayo ni wizara inayoongozwa na ccm, ukiangalia mamlaka ya waziri wa tamisemi kisheria utagundua kuwa hata wakiongoza halmashauri, hawataweza kufanya mambo makubwa sana kwa sababu waziri atawafunika. recall halmashauri ya tarime waliyoiongoza kwa muda mrefu, walimudu kulipia watoto karo tu kutokana na mchango wa mgodi wa north mara kwa halamshauri na machache mengine ila mengi hasa yanayotegemea sapport ya serikali kuu yalikwama

Kwa hiyo mnadeclare kwamba mmeshindwa kuiwajibisha serikali?

Any way, hao mawaziri vivuli wana kazi gani hasa? maana ilikuwa mbinde nikadhani wanagombania kuonyesha uwajibikaji na ufanisi wao (kama sio kupata title na posho za vikao) - wanajua fika hawaiwezi serikali.
 
Asante Dr Slaa na Mapambano ya Civil Rights na Democratic Reforms Tanzania. Mungu Akulinde Siku Zote na Njama za Uhaini wa ccm

Hii timu ya mafisadi ndio wanajiita timu ya taifa stairs? Wanajiteua wao wenyewe serikalini ili kutumaliza sio. Hatutanyamaza na wala hatuogopi hata kama wewe ni mkuu wa jeshi wala usalama wa taifa.

Asanteni watanzania dani ya Usalama wa Taifa, Jeshi la ulinzi na usalama, PTCB na wengine serikalini. Wengi mnafanya hii kazi katika mazingira magumu na hatari lakini bado mnatupa inform muhimu sana. Nyie ndio MASHUJAA.
 
Atakuwepo Salva rweyemamu, Ngeleja, Masha, Wasira
Acha upuuzi wewe,
Mhe.wasira Hana kashfa yeyote,hajawahi,Hana na wala hahusiki kwa lolote.wasira msafi sana kati ya viongozi bora na wanaotumainiwa na
ccm.msimamo wake ni kutetea wanyonge na amekuwa msatari wa mbele kupinga ufisadi.usiwaseme Watu usiowajua vizuri, Kama una ushahidi kuhusu huyu mhe. Tumwagie hapa ushahidi tuuchambue tujue mbivu na mbichi.otherwise the man is strong and wise!
 
Kwa mwendo huu, nahisi na mimi Selemani pia nitatoka kwenye list ya mafisadi one day. @Dr. W. Slaa vipi muheshimiwa na mimi simo kweli?

Nakumbuka niliwapoza vijana wa Majembe na wekundu ili wasikitow ki-Starlet changu pale Barclays opposite na Movenpick. I did cost the city of Dar 120K that day.
Naona Mzee kaamua kupumzika, haya we endeleza mbwembwe
 
Haaha! Watu wengine ovyo kweli...... Unasema hana jipya mbona nawe ujioni kuwa huna jipya!!! Mambo ya nyani hayo.
List imebadilika kulingana na wakati sasa unataka mapya gani? :A S 465:
aaah... hana jipya!
 
Hakuna jina jipya, hebu tupe feedback wa nani aliyefilisiwa baada ya kutajwa fisadi? Lowassa kapelekwa mahakamani, Chenge je, Karamagi, Meghji, Sumaye - tena huyu kageuka kuwa mlaani ufisadi, lolestiest.

Kama CHADEMA walishawataja hawa mvua kadhaa zilizopita kwa nini wanarudia kuwataja - tena hata wakifanya hivyo kwa matarumbeta na brass band - sirikali haiwezi wapeleka mahakamani na wanajua hilo.

Je ndio kusema CHADEMA wameishiwa hawana mawazi mapya pamoja kuwa na vijana wengi - if Lissu is also kijana.

@ Jasusi - nawaomba CHADEMA waandae sera, mipango, mikakati na malengo mbadala kuhusu uboreshaji wa maisha ya Mtanzania. Kama wamejaa hapa mbona wamekurupuka kwenda Tabora na kurudia mambo ambayo ni 'so over'.
Kama wewe ni kichwa cha panzi itachukua muda mrefu kuelewa alichofanya leo Slaa, hata CCM hawakumwelewa wakati anataja list of shame Mwembe Yanga lakini leo baada ya miaka kadhaa wanakiri kuna ufisadi binafsi sikushangai mko wengi.
 
Ikiwa ni takriban miezi sita tangu uchaguzi mkuu wa rais na wabunge, umaarufu wa DR umeshuka kwa asilimia 60% hii ni kwa mujibu wa shirika binafsi linalo jishughuliza na tafiti mbali mbali nchini hapa la clybase foundation, habari zaidi tembelea tovuti yao.
 
Kwa hiyo mnadeclare kwamba mmeshindwa kuiwajibisha serikali?

Any way, hao mawaziri vivuli wana kazi gani hasa? maana ilikuwa mbinde nikadhani wanagombania kuonyesha uwajibikaji na ufanisi wao (kama sio kupata title na posho za vikao) - wanajua fika hawaiwezi serikali.

mpendwa,

mimi si mwanachama wa chadema wala si mwanasiasa, ninachangia tu mawazo hapa na kujifunza kutoka kwa wengine, kwa hiyo usinijumlishe humo pamoja na wenye chama chao.

nijuavyo mimi, waziri kivuli hana nguvu za kisheria za kiutendaji na hana hata bajeti wala fungu lolote. ni mbunge wa kawaida tu na ile kuitwa kivuli ni kama watch dog rasmi (japo kila mwakilishi ni watch dog kwa serilkali). nadhani wapo kama wasemaji rasmi wa kisekta tu wa kamabi ya upinzani ka mujibu wa kanuni za bunge. pia kama ujuavyo uchache wao pamoja na spika wa bunge kuwa kinyume chao, kunawafanya hata wakiwa na hoja muhimu kutupiliwa mabli kirahisi.

siamini kama wameshindwaa kuiwajibisha serikali. angalia kwa mfano suala la muswada wa katiba mpya, au hata kujivua magamba kwa chama tawala wiki ilyopita. utaona wana mafanikio mengi sana na hata serikali na cham wanajua. japo bado iko madarakani lakini inajua kuwa kuna wath dogs na ina-respond kwa hiyo inayoitwa nguvu ya umma. kama unafuatilia siasa za kwingineko duniani utagunduoa ccm inaheshimu sana changamoto za chadema na inajua kuwa ikishindwa kukabiliana nazo siku moja itanyang'anywa madaraka ya kuongoza serikali na bunge
 
Wadau mmeona, kama hamjaona kwa nini iwe hivi? binafsi nimeangalia ITV, TBC na Star tv sikuoana zaidi ya zile za ccm
karibuni
 
Kama wewe ni kichwa cha panzi itachukua muda mrefu kuelewa alichofanya leo Slaa, hata CCM hawakumwelewa wakati anataja list of shame Mwembe Yanga lakini leo baada ya miaka kadhaa wanakiri kuna ufisadi binafsi sikushangai mko wengi.


kama wewe kicha cha kakakuona analyse pros and cons za aliyoyafanya Slaa. Kuna tofautu gani kati ya aliyoyafanya leo na aliyofanya mwembe yanga?`What is the implication kwenye kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida.

Members mwenye macho kasoma, mwenye akili isiyo ya panzi kaanalyse na kuchukua cha kuchukua.

@Miss Judith, mimi sio mwamnachama wa chama chochote cha siasa, sio mwanaharakati, ila nina mapenzi mema na mustakabali wa nchi yangu, nchi ya wanangu na wajukuu zangu, ndugu, jamaa na wengi wa marafiki zangu, wananchi wenzangu.


One love, stay blessed.
 
Duh, Pamoja na Kelele zote zilizopigwa za kutaja mafisadi nilithani leo angezaliwa tembo kumbe ni ka-panya kametoka, tena kadogooooo !

Any way, HONGERA DR. SLAA Vita ya kupambana na mafisadi lazima inendelee. Halali mtu mpaka kimeeleweka. Miaka 50 ya uhuru inatufundisha kwamba, ukilala tu kidogo na kufumbua tu macho, mamilioni ya tani za madini yetu yameshapotea. Mafisadi wa CCM jamani ni nyoka wa baya sana !!!!
 
Hili la kuwataja Mafisadi waliopo CCM na Serikalini ni la muhimu sana. Tusisahau ya kwamba CCM wanajaribu kutuonyesha ya kwamba kwa Sekretariati yake kujiuzulu na wajumbe wake kutorudishwa tena basi wapo safi. Au isidhani kwa viongozi wake wenye tuhuma nyingi kama Chenge, RA na EL kutokuwamo katika Kamati Kuu ya Chama hicho basi tena wapo safi, hii si kweli.

Ufisadi umezidi kuongezeka na hali ya maisha ya Mtanzania imezidi kudorora. Kwa hili ni ishara ya wazi kabisa ya kwamba bado kuna viongozi wengi tu na wafuasi wao ndani ya CCM bado wanaendelea kufisadi mali ya umma. Hivyo kitendo cha Chadema kuamua kuwataja ni kuonyesha jinsi gani CCM inavyojaribu kufanya usanii ambao ni wa kitoto sana.

Wanamdanganya nani ya kwamba sasa chama ni safi na kinapambana na ufisadi? Hivi hawaoni ya kwamba maisha yanazidi kuwa magumu kwa mwananchi wa kawaida? Hivi wanadhani wananchi hawaelewi ya kwamba kila kukicha miradi mingio ya maendeleo haimaliziki kwa sababu ya utafunaji wa fedha za miradi hiyo? Nani asiyejua ya kwamba hatuna dawa hospitalini? nani asiyejua ya kwamba wamechakachua huduma zote za kijamii kwa manufaa yao ya kisiasa?

Lazima CCM ijue, michezo yake michafu na ya kitoto isiyo na manufaa kwa watanzania walio wengi inaonekana. Hawajajivua gamba, hili ni wazi kabisa, usanii mtupu.

Hivyo kitendo cha Chadema kujiandaa kuwaonyesha wananchi ya kwamba kunamafisadi wengi tu ndani ya chama na si ajabu baadhi yao wapo katika Sekretariati mpya na Kamati kuu ya CCM ni kitendo kizuri kwa mustakabali wa taifa letu.


Mziki walioanzisha utawapiga mweleka, huwezi kudanganya kizazi cha sasa kwamba unafukuza mnafisadi kwenye chama lakini wanaendelea kupeta mitaani na mali za kifisadi, wanapaswa kutekeleza kwa vitendo - kamata, filisi, funga. Wakifanya hayo hawana haja tena ya kutangaza ila watatangazwa na cdm watabaki midomo wazi, lakini hilo haliwezekani kabisa labda hapo jua litakapobadili mwelekeo (kuibukia magharibi na kuzama mashariki). Nape ajue anakazi bado ya kucheza ngoma ya cdm kwa miaka mingi ijayo mpaka hapo ccm itakapokuwa chali...
 
..........Kweli nimekubali kauli ya mtoto wa mkulima asiye mkulima namnukuu "Mafisadi wana nguvu"
 
jamani inasikitisha ccm ni chama cha mafisadi alafu msekwa analalamika vijana hawana adabu kumbe kuwa na adabu ni kushabikia mafisadi.wakome hawa mafisadi wa ccm walikua wanadangavya watanzania hiki ni kizazi cha kijanja sipati picha gamba la ccm
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom