Re: ziko wapi shule za vipaji maalum?
Shule za vipaji maalumu zitabaki kuwa hivyo lazima tuukubali ukweli huu hata kama wengine tunamachungu ya kutopata nafasi katika shule hizo.kuweka kumbukumbu vizuri kwa wavulana shule hizi ni Kibaha,Iliboru.Mzumbe na Tabora wavulana.
Kulinganisha shule hizi na feza boys,kisimiri,igawele na shule hizi ni kulinganuisha jua na nyota.
1.Toka mkoloni shule hizi zimedhihirisha ubora wake mpaka leo.
2.Idadi ya wanafunzi wanaotahiniwa katika shule hizi ni kubwa sana ukilinginisha na shule nilizozitaja hapo juu zenye watahiniwa wachache mfano Feza ilikuwa na watahiniwa 60 pekee.daraja la 1-36,daraja la pili 18,daraja la tatu 6,hakuna four wala ziro.igowole ambayo ni ya kwanza ina watahiniwa 30tu,Kisimiri watahiniwa 52 tu.daraja la 1 -34,la pili 10,la tatu 8.
3.Shule nyingi hizi ndogondogo hutegemea sana udanganyifu kwenye mitihani ndiyo maana inaweza chomoza mwaka huu ikapotea kabisa isionekane tena wakati hizi za vipaji watu hutunisha misuli hasa kombi zenyewe nyingi ni za sayansi mfano pcb Hebu tuzipe
kwa mamtiki hiyo shule za vipaji maalumu zimezihirisha uwezo wao angalia matokeo yake na idadi ya watahiniwa.
1.Kibaha watahaniwa 161,daraja la kwanza 82,la pili 59,la tatu 18,la nne 2 hakuna 0.
2.Mzumbe watahiniwa 125,daraja la kwanza 56,la pili 38,la tatu 29,la nne 2 hakuna 0.
3.Iliboru watahiniwa 150,daraja la kwanza 53,la pili 50,la tatu 44,la nne 3 hakuna 0.
4.Tabora wavulana watahiniwa 158,daraja la kwanza 49,la pili 62,la tatu 45,la nne 2 hakuna 0.
Huwezi kuzinganisha na shule za watahiniwa wachache,hebu linganisha na shule zingine za wanafunzi wengi kama Tambaza,Pugu,Milambo ndo utajua kweli hizi shule ni majembe.
hazina daraja 0,daraja la nne ni 7 tu
hongereni madogo kwa kudhihirisha uwezo wenu njia nyeupe vyuo vikuu.
UKIONA NYANI MZEE JUA KAKWEPA MISHALE MINGI