Nilipata neema ya kusoma kibaha o level na baadaye Tabora boys shule hizi kweli ni za vipaji maalum zote, lakini zinatofauti sana,angalia mabweni ya Alevel ya Kibaha,walimu lukuki,chakula wanachokula wanafunzi! nakumbuka miaka ile kibaha tulikuwa tuna kunywa uji na sukari saa moja saa nne chai na andazi nk,wali mara 3 na nyama,mwanafunzi hakuchapwa viboko zaidi ya 6.nilipokwenda Alevel Tabora boys hali ilikuwa tofauti kabisa hakuna chai ila uji usio na sukari,wali mpaka siku ya sikukuu lol,walimu wachache mpaka tulikuwa tunaazima wa girls,wanajeshi walikuwa wakichachaa mnapigwa viboko watakavyo wao shuruba mtupu.Mazingira mazuri yanamuweka mwanafunzi ktk nafasi nzuri ya kufanya vizuri.
Kwa kweli wahusika waitendee Tabora boys kama zilivyo shule maalum zingine kama Kibaha,Mzumbe,Iliboru.
Wako wanaohoji uwezo wa kazi wa watu waliopita katika shule hizi kwa kweli wengi wako juu mno kwenye utendaji wao,wale ambao hawakupata bahati kupitia shule hizi wasiponde tu vile walikosa nafasi za kusoma shule hizo.