Table manners

😀😀😀

Thanks for making up my day...lol!
The pleasure has been all mine. Worry not though should you ever decide to invite for dinner I do know how to use knife and fork though I will forever prefer my hands to any other cutlery.
 
Reactions: kui
Hahaha umenifurahisha sana mm pia napenda kumla kuku kwa mkono
Cku moja nlkuwa mahala akaja dada mmja na jamaa akaagiza wali samaki alikuwa anapata shida kumla samaki hadi huruma,nkajisemea c amle kwa mkono tu?
hahahhaa!sijikalifishi nafsi hata Siku moja!!
 
Wakuu, na wale tunaokula kwa kutumia mikono, table manner yetu ni kama ifuatavyo:

1. Usimege ugali kwa mkono wa kushoto.

2. Using'ate ugali kwa meno kisha kuchovya tonge hilo kwenye bakuri hasa mnapokula kwa kushirikiana (kushare) chakula kwenye sahani moja.

3. Ukinawa mikono kabla na baada ya kula usi-shake mikono yako....acha maji yakauke kwa hewa yenyewe.

4. Usikombe au kunywa mboga mboga.

5. Ukila nyama au kuku usisukutue mdomo wala kupiga mswaki. Fanya hivyo pale tu unapokula mboga za majani au mboga nyingine sizisoeleweka.
 
Kha!hizi mambo sisi wandengereko hazituhusu kwa kweli !mwendo lete maji ya kunawa ,finyanga tonge poteza !kamata paja ng'ata peleka pwani! Na kama nguna kwa ndondo kata tonge ,design shimo moja matata jaza ndondo peleka pwani tena sio kimyakimya hapo hadithi kibao mmezunguka plate!
 

Katika vitu ambavyo huwa sitaki kujibania kwenye msosi huwa ni mboga, bora mboga izidi ugali au chchte
 
Safi sana ila hii inatumika kwa elite families. Ninafikiria zile familia ambazo zinasubiri ugali kwa samaki wadogo a.k.a vidagaaa. Ukweli hata viongozi wetu wanapopata madaraka inabidi wafundishwe table manners maana wengine walizoea wakirudi wanakuta msosi kwa hot pot na sahani na kijiko tu kama ni chakula cha kijiko au beseni na kajaji ka kunawia kama ni ule ugali wetu pendwa. Kwa misingi hii kwa Tanzania yetu naweza kusema pangine ni 5% ya population wanazingatia yote uliyosema kuhusu table manners and arrangements of cutlery.
 
Mmmmh! Hadi kula kuna sheria! Hayo makorokoro yooote nitashiba lini, unanawa mikono unapiga kitu, kwisha habari.


..hehe, atoto unakuwa kama yule mdau aliyesema akitumia uma na kisu hashibi.
 
Mkuu shukrani, u Mkuu shukrani, umenifundisha ustaarabu zaidi, ila kwenye kushika umma na Kijiko nashindwaga ku balance kwa sababu ni left handed, hayo mengine ni dhahabu, ahsante sana.
 
..hehe, atoto unakuwa kama yule mdau aliyesema akitumia uma na kisu hashibi.
Kuna kipindi tulikuwa tunakwenda mahali, acha tupewe semena ya table maners, aisee kidogo nighairi maana huo mlolongo! Lkn taratibu nikazoea.
Hawa wazungu wanatuletea balaa tu, maana hata hauli kwa amani unaogopa kukosea.
 
Reactions: kui
Hao Watanzania 2% ndio wamelengwa hapa. Kama mzungu kaja kwako akakukuta unakula kwa mkono naye akala kwa mkono kwanini wewe ukienda kwake usile ki utamaduni wake? IQ kubwa hujengwa kujua masuala mengi tofauti tofauti. Huwezi kuwa na IQ kubwa kwa kujua tu namna ya kusaidia 98% ya Watanzania wasiotumia uma na kijiko wakati wa kula. Umefanya kitu gani katika jamii yako ambapo utaendelea kukumbukwa milele kama anavyoendelea kukumbukwa hayati Mwl. J. Nyerere?
 


Ni ujinga kwa sababu hao chini ya 2% hawahitaji kufundishwa kutumia uma na kisu kwani wanajua tayari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…