Tabiri matukio magumu kutokea world cup 2014

Tabiri matukio magumu kutokea world cup 2014

Mc Tilly Chizenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2012
Posts
4,641
Reaction score
3,686
Salamu wapenzi kabumbu

Hapa tunatoa utabiri wa kawaida tu ule wa kiushabiki sio wa ki-tb joshua au ki-shehe yahaya

Huu hapa utabiri wangu
*UJERUMANI ATATOLEWA ROUND YA KWANZA
*KATI YA ITALIA NA UINGEREZA MMOJA ATAAGA ROUND YA KWANZA
*TIMU ZILIZOCHEZA FAINALI 2010 HISPANIA NA UHOLANZI MMOJA ATAAGA MASHINDANO ROUND YA KWANZA
*ALGERIA ATAVUKA HATUA YA MAKUNDI
*USWIZI NA UBELGIJI ZITAENDA HADI NUSU FAINALI AU MMOJAWAPO ATAINGIA FAINALI

Tupia utabiri wako na wewe tusubiri na kuona nani kapatia nani kachemsha
 
Brazil ataondolewa kwenye makundi
Gana atavuka round ya kwanza
Ureno watacheza nusu fainal
Ujerumani watasuasua lakini watacheza fainal
 
Utabiri wangu ni kuwa Wenyeji Brasil watatolewa hatua ya makundi na ubingwa mwaka huu unaenda Ufaransa..!!
Utabiri huu ni kwa hisani yangu mwenyewe


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Brazil akikosa kuchukua hili kombe au kufungwa hapo kwa kweli ile nchi haitakalika. Amini nisemacho ili Brazil iwe safi basi timu ya taifa ichukue kombe
 
algeria itatutoa kimasomaso waafrika

uruguay na belgium zitaishangaza dunia

welbeck atakuwa mfungaji bora

msitarajie jipya kutoka kwa messi kwani atapwaya sana
 
Back
Top Bottom