nawasalimuuuuu all MMU
leo naomba nidondoshe hii habari kidogo, wanawake pia mwakaribishwa kuongezea baadhi ya tabia za wanaume wachache wakiwaga na hela.
1)yeye sio mkosaji: hapa nazungumzia kupatikana na hatia. yaani kama kakukosea lazima atengeneze maelezo mengi mpaka akuset ujione wewe ndie uliye kosea kumbe ni yeye.
2) hajui kuomba/kutamka SAMAHANI. hapa hata kama kakukosea kamwe samahani hajaumbiwa kinywani mwake.
3)kujikweza: hapa utakuta kila mwenzie au jirani yake akifanya jambo zuri utasikia yeye anaona kama hamna kitu .
4)ujuaji:hapa atataka kuonesha umwamba wa kila kitu kwamba anakijua. mfano unakuta ye ni daktari basi akifika kwa mjenzi atampelekesha kiudaktari na wakati professional ya udaktar haiingiliani na ujenzi
5)kiburi: hapa huwa hasikilizi ushauri haambiwi haambiliki anaweza akanya mlangoni kwako ukimuuliza utasikia ina gharimu kiasi gani kwani? badala hata utoe excuss.
6)sifa: hapa akitoa hela ndani atatangaza ukoo mzima hadi wale marafiki wa utotoni wajue. au akisikia michango utaona atatoa kiwango kikubwa tofauti nakilichopangwa ili aonekane zimo.
7)wanamsahau Allah /Mungu. hapa ibada kwao ni mwiko siku ya ijumaa ni siku ya kununulia bia wanaita weekend mood. wale wajumapili utasikia ndio nafua.
8)----------
9)--------
10------
nawakaribisha mmalizie sifa za wanaume baadhi wakipata hela za ghafla..