Tabia za kujibu text wanawake walizonazo zinazokera

Tabia za kujibu text wanawake walizonazo zinazokera

Habari wanajamvi, hii tabia iko hasa kwa wanawake naamini kuwa every one is different ila kuna vitu vingine huwa vinaboa

1)Unakuta mtu unamuandikia mwanamke text ndefu ya maana (sio love text) umejielezea vizuri na text inahitaji long explanation lakini mtu ana kujibu "k"

2)Au unakuta kwenye makundi ya whatsapp demu akichangia anaandika maneno mawili tu hadi watu wanashindwa kuelewa kuwa kuwa huyu mtu anamaanisha nini.

3)Au unamtext demu leo na unamuona yuko online lakini anakuja kukujibu massege yako baada ya 9hrs au anajibu kesho yake.Na sio kwamba yuko busy sana au massege yako haina maana, yani ni basi tuu

Sasa sijui wengi wao wanafanya hivyo ili waonekane expensive sana au?

Ukiona hiyo ujue anaku-admire sana il nafanya siri usije ukajua. Huyu mara nyingi anakuwa ni yule ambaye huna uhusiano naye ila kuna matarajio ya namna hiyo baadaye!
 
Ukiona hivyo heshima hakuna au huyo mwanamke amekuzoea sana nowdayz au mwanamke anaona hunamsaada kwake yye ndie anakupatia vijipesa Fulani so yye ndie don no need ya kuact kwako haraka.Ndio hivyo kemea hizo tabia mapema kabisa kabla hazijajengeka.
 
Back
Top Bottom