Tabia za Kike

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,604
Za wikiendi Wana JF!
Tumekuwa tukisikia wakaka wakilaumiwa na wakaka wenzao kuwa wana tabia za kike. Mara nyengine hata wadada huwalaumu wakaka hao kwa tabia za kike, na hufika mbali hata kuwalaumu wadada wenzao kwa kuwa na tabia za kike.
Hata humu JF kuna posts zinashutumiwa ama mtoa mada ana tabia za kike au hata kutilia shaka jinsia yake. Angalia mifano katika michango No. 4,5, 6 kwenye thread hii:

https://www.jamiiforums.com/complaints-congrats-advice/196393-nimekwazika-kwa-herini-mmu.html

Je nini zipi hizi tabia za kike? Nini uzuri kama upo) au ubaya wake.

Nawasilisha na kuwatakieni wikiendi njema.
 
tabia za kike badala ya ku-fight waishia kulalamika kuseek attention ili usaidiwe, kuskilizwa na hatimae kumegwa.
 
Hiyo inatokana na kuhusisha udhaifu (wa aina yoyote ile) na uanamke.Ndio maana hua haitumiwi positively. . . kwasababu inahusiana na mtu kuwa mdhaifu katika nyanja fulani.

Mf. kulia,kuongea sana,kuwa mmbea/mchonganishi, kulalamika, kutoweza kujitetea, kununa, kuwa sensitive n.k
Binafsi hua nakwepa sana kutumia hayo maneno maana hayana maana nzuri kwa mwanamke.Pia inatengeneza mentality ya kutokua huru haswa kwa watoto wa kiume.Ndio maana kwenye jamii yetu bado kuna ugumu kwa wanaume kueleza/onyesha hisia zao za kweli.
 
Ninakubaliana nawe Mkuu, nimeuliza swali hili nikiwa na hofu, kwanza, ya kuwakwaza wanawake kwani si kila mwanamke huwa na tabia hiyo, pili sioni kama kuna uhusiano mkubwa na baadhi ya hizo sifa ulizozitaja, ukiwachia kulia na kuwa sensitive kwa sababu ya ubinadamu wao.

Ukiangalia sana, utaona kuwa hizo ni tabia za baadhi ya watu na haina uhusiano na jinsia bali ni kwa tabia tu ya kuwaona wasichana kama viumbe dhaifu.

tabia za kike badala ya ku-fight waishia kulalamika kuseek attention ili usaidiwe, kuskilizwa na hatimae kumegwa.
Umenichekesha sana. Unataka kusema hata wanaume wenye tabia alizozitaja na zile alizo taja Husninyo, wanaweza kuishia kumegwa? Pole zao!

Kupaka poda, vaa hereni, suka nywele, tinda nyuzi, paka wanja.
This is most interesting! Kwa wanawake hizoingawa zimeenea lakini nahisi wameingia katika uwanja sio wao huku wakijidai ni vidume vya mbegu.
ANGALIZO: Ninaheshimu uhuru wa kila mtu bila ya nia kumvunjia heshima yeyote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom