Tulee watoto wa kike waukubali uwanawake

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,584
4,264
Ukifuatilia huku mtaani kuna nguvu ya kutaka kuwalinganisha Watoto wa kike na wakiume kitu ambacho kimsingi sina tatizo nacho ila tatizo ni utekelezaji wake

Namaanisha kuna gap kubwa tunaliacha kwa kukosa kulea Watoto wetu wa kike kujikubali na kujiamini kuwa wao ni Wanawake na kuwafunza mambo yote ya msingi ya kiuwanamke na kuwa mwanamke ni sifa bora kabisa hivyo hakuna haja ya kujifanya mwanamme. Kwa sasa kuna wasichana wengi tu wa miaka 18 na kuendelea ambao hawajui majukumu ya kawaida ya kike na wazazi wao kwa kukosa maarifa hawajaona kuwa ni tatizo
Na hii hulka ya kusema kila anachofanya mwanamme na mwanamke anaweza kufanya ni nzuri ila inatakiwa itafisiriwe vizuri kwani hiyo kimsingi hutumika kama motivation speech ila kwa sasa inatupelekea kuwa na kundi la Wanaume na kundi la wanawake wenye tabia za kiuwanaume.
(Inamaana kwa kutokujua tunaweza kuondoa kundi la wanawake wenye tabia za kiuwanawake)
Labda tu mfano mrahisi; Kwenye aina yeyote ya mchezo, wanawake huwatenga hata wanawake wenzao wanaofanya vizuri kwa kufikiri wana genes za kiume inamaana kiuhalisia wanawake na wanaume ni tofauti kwa mambo mengi tu hivyo nafikiri hizo kauli ziwepo tu kama motivation

Wazungu walipita huko na ndio sababu kwao mambo kama ya Ndoa ni kama mchezo wa Kuigiza; Unaweza kufunga asubuhi na jioni imesha vunjika na huko kwao watoto wengi tu wanalelewa na mzazi mmoja na sasa waeibuka na hii tabia nyingine....
Mbaya Zaidi baadhi ya wazazi walio elimika ndio wanafikiri kila cha kimagharibi ni kizuri
Nafikiri tuwe waangalifu tusije kufanya makosa waliyofanya wazungu ambayo tayari yana wacost....

Huo ni mtazamo wangu
 
Kuna mambo ni ngumu kuyaona mpaka yalete madhara.

Muhimu kila moja apambane watoto wake
 
Back
Top Bottom