Mtoto wa kiume hapaswi kuwa na tabia za kike

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,483
21,955
Kwenu walezi wote wa watoto nawaombeni tushirikiane kuwafanya watoto wetu wa kiume wakue kiume na wawe wanaume halisi wa kesho

1. Nianze kwenu wazazi akina mama
Toeni nafasi kwa watoto wenu wa kiume kupokea kipigo kutoka kwa watoto wengine wakati wa kucheza mpira.

Waache pia wapande baiskeli na kukwea kuta na miti.

Acha kukimbilia kuwaokoa wakati waangukapo kidogo.

Ruhusu ugumu wa nywele zao, yaani zifanye ziwe ngumu ngumu na sio laini kama za dada zao.

2. Kwenu wazazi akina baba
Wafundisheni watoto wenu wa kiume kuzungumza, kuvaa na kukojoa kama wanaume.

Wazuieni kuvaa suruali inayobana ngozi na kutumia vipodozi, waambieni waziwazi kuwa hayo ni mambo ya kike.

Kwa hali ya sasa mkanganyiko wa kijinsia unachangia kuongezeka kwa hali ya unyogovu na kupoteza kujivunia.

3. Kwenu waajiri
Acheni kutuza na kuabudu tabia za kike kwa wanaume mliowaajiri.

Ikiwa tutaharibu utambulisho wa kijinsia, jamii itaanguka hakika.

Tusherehekee uanaume kwa wanaume.

Hapa sizungumzii mila potofu ya kijadi ya kiume ya kuwadhulumu wengine. Sivyo kabisa!

Wanaume wa kweli ni wazuri, wenye fadhili, wenye huruma na wana hatari. Lakini hawapotezi utambulisho wao wa kiume.

Tuwainue wanaume kutoka kwa wavulana wetu tunaowakuza kiume.

Wanaume halisi wanamtumikia Mungu, pia sio mafisadi kwa nchi na familia.

Wanaume wa kweli wanapendekeza - hawanaga uchumba na msichana kwa muda usiojulikana.

Wanaume halisi wanafanya kazi. Wanaume halisi hulipa bili.

Wanaume halisi hulinda wanawake katika maisha yao.

Ubarikiwe.
 
Hakikaa ukisemacho mm na mwanangu nilitelekezewa akiwa na miaka 2 na malay* mmoja nilizaa nayee ,mtt n wakiumee aiseé naishi nayee Toka akiwa na miaka 2 mpk now anamikaa 7,aiseé namfundishaa kilaa ktu ,hapaa yenyewe tumetoka kucheza mpira uwanjan n vile siwezi share pichaaa humu ,na ajawah muulizia mama yake anaami mm ndio nimezaa .
 
Uanaume pia uwepo kwenye maandishi yako,kuna kauli Mwanaume hutakiwi kuzitumia,

Maneno kama;
Jamani au Jamoni,
Kuandika kwa mkato mkato,
Kudhihaki Imani,dini za wengine,
Kuwakimbia Panya road,
Kunywa mchuzi wa pweza,vikaranga,sijui nazi,mara muhogo mbichi,Mwanaume piga mazoezi,

Mwanaume ni kujiamini,self confidence.
 
Hakikaa ukisemacho mm na mwanangu nilitelekezewa akiwa na miaka 2 na malay* mmoja nilizaa nayee ,mtt n wakiumee aiseé naishi nayee Toka akiwa na miaka 2 mpk now anamikaa 7,aiseé namfundishaa kilaa ktu ,hapaa yenyewe tumetoka kucheza mpira uwanjan n vile siwezi share pichaaa humu ,na ajawah muulizia mama yake anaami mm ndio nimezaa .
Unaishi nchi gani kiongozi?
 
Back
Top Bottom