Tabia za kibongo ambazo ni kero kidogo

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,815
wabongo tuna tabia fulani hivi ambazo sometimes huwa kero, kama vile;
1.Kuulizia bei vitu vya mwenzio, akikuta una simu ataanza umenunua sh.ngapi?, akija geto akikuta kitu atauliza..... ni kuulizia bei kila anachokiona
2.Kusifia hata kama sio kweli pale anapohitaji msaada,yaani atatoa sifa hadi kero kuna sifa unajua kabisa huna ila yeye anasifia tu
3.Kulazimisha kufahamu vitu vingi vingi na kusema anamiliki, anafahamu aina za magari ikiwezekana na bei zake na kujisifia amewahi kumiliki ,anawafahamu watu wote maarufu na kujifanya naye wanamjua sana
4.Kupenda kuonekana anasafiri safiri ili aonekane ana michongo mingi, utasikia juzi nilikuwa Arusha, wiki iliyopita nilikuwa mwanza, kesho naenda moro mara moja, next wiki napanga kuwa iringa ili niiwahi semina kule mtwara kabla Makonda hajanipigia simu nikamilizie mchongo fulani Dar
5.Kujifanya hataki msaada mbele ya watu wengi baadae utasikia una laki moja mkuu hapo nitakutoa next week...

hizi ni baadhi tu.. tiririka Kama kuna zingine
 
kero yangu me misos kuadimika mtaani kipind ich cha mwezi hapa magomeni vibanda vya mama ntilie vyote wanaanza kupika jion Futari Only
 
Kujifanya hataki msaada mbele ya watu wengi,,, hii ninayo na ninaipenda coz nyie mna tabia ya kutangaza shida za watu as if nyie hamna shida. Ukiniomba nikusave sintasema pia,ni heshima
 
Kuna Tabia tupo kwenye daladala.. tunapita eneo la ajali atajitokeza mjuaji mmoja ataanza kusimulia mkasa mzima (mwanzo hadi mwisho) wa ajali ilivyotokea wakati tumekaa wote siti moja kwenye gari na wote tumeikuta ajali imeshatokea.. na anamalizia kusema nani ndio Chanzo cha Ajali.

Hii ni Kati ya tabia adimu utakayokuta Bongo tu.
 
wabongo tuna tabia fulani hivi ambazo sometimes huwa kero, kama vile;
1.Kuulizia bei vitu vya mwenzio, akikuta una simu ataanza umenunua sh.ngapi?, akija geto akikuta kitu atauliza..... ni kuulizia bei kila anachokiona
2.Kusifia hata kama sio kweli pale anapohitaji msaada,yaani atatoa sifa hadi kero kuna sifa unajua kabisa huna ila yeye anasifia tu
3.Kulazimisha kufahamu vitu vingi vingi na kusema anamiliki, anafahamu aina za magari ikiwezekana na bei zake na kujisifia amewahi kumiliki ,anawafahamu watu wote maarufu na kujifanya naye wanamjua sana
4.Kupenda kuonekana anasafiri safiri ili aonekane ana michongo mingi, utasikia juzi nilikuwa Arusha, wiki iliyopita nilikuwa mwanza, kesho naenda moro mara moja, next wiki napanga kuwa iringa ili niiwahi semina kule mtwara kabla Makonda hajanipigia simu nikamilizie mchongo fulani Dar
5.Kujifanya hataki msaada mbele ya watu wengi baadae utasikia una laki moja mkuu hapo nitakutoa next week...

hizi ni baadhi tu.. tiririka Kama kuna zingine

Mbwembwe na kujishebedua kwingi..., hatuna tujualo zaidi ya kuwaonea wengine wivu/kijicho!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom