Tabia ya rafiki yangu ni mtihani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,273
Nina rafiki ki umri amenizidi miaka miwili lakini Hii ni age range moja. Huyu rafiki ananipenda mno siwezi kukata, ananichukua kama ndugu yake wa damu. Mfano tu kulikuwa na safari kanisani tulitakiwa kuchangia usafiri, malazi na chakula. Ilikuwa laki tano jumla, wakati ninajipanga niitoe, shost aliniambia amelipa ya kwake pamoja na ya kwangu. Nilimuambia nitamrudishia alikataa kabisa.

Alikwenda holiday akaniletea designer handbag, kwakweli gharama yake nisingewaza kununua kwa pesa yangu.

Tatizo linakonikera anapenda sana kufanyiwa mambo mengi. Mfano ukimwambia kuna kazi nimeona wanatangaza, atakuambia Uje basi nyumbani unisaidie kujaza fomu. Ukifika kwake anakupa computer hii, majina yangu ni haya. Kheri angesama nilijaribu nineshindwa ninaomba msaada.

Kibaya zaidi hata academic work, anaomba msaada, ataniita amepika chakula, kuna glass ya wine kumbe amekuitia assignment yake ya darasani.

Kama anashindwa assignment hii course si aiache. Kwakweli ninampenda lakini urafiki unanishinda.
 
Mshauri atafute rafiki wa kiume sisi huwa hatuchoshwi na kusaidia kama atanipa heshima na nanii basi.

Tatizo sasa shule mimi nilifeli hizo academic work ndiyo kazi za kitaalamu au kitaaluma?

bbade anatafuta rafiki kama huyo.
Yaani weekend unapumzika anapiga simu kuwa anashida, kwa jinsi ninavyomheshimu ninamsikiliza ukitoka hapo akili umeichosha hata haikuwa weekend tena.
 
Yaani weekend unapumzika anapiga simu kuwa anashida, kwa jinsi ninavyomheshimu ninamsikiliza ukitoka hapo akili umeichosha hata haikuwa weekend tena.
Nakuelewa saana.... si Tandale mshost wakija kukutembelea stori zinakuwa za michango ya vijora, mume wa fulani anatoka na mke wa fulani, ......

Sasa huyu mdada anakuchosha na academic work anatakiwa aache mara moja...mfundishe ushosti wa Tandale.
 
Nakuelewa saana.... si Tandale mshost wakija kukutembelea stori zinakuwa za michango ya vijora, mume wa fulani anatoka na mke wa fulani, ......

Sasa huyu mdada anakuchosha na academic work anatakiwa aache mara moja...mfundishe ushosti wa Tandale.
Siku nyingine akipiga simu ninamwambia niko ukweni, lakini ninakuwa nafeel guilty nikikumbuka wema wake.
 
Mimi ninakaa Gheto na Mshkaji.

- Anakunywa Pombe Balaa ( Mshahara wake haumalizi siku 5 ).

- Anavuta Bange Balaa, Tena Wakati Mwingine Uko Gheto Umelala - Yeye Anatoa Anawasha.
( Nilishamwambia Moshi Wa Bange Unaniumiza, Ila Hajali ).

- Akinywa Pombe Mpaka Anazima, Anatapika na Kukojoa Gheto. Usafi ni Mimi.

- Pesa Ya Chakula Hachangii Wala Kodi, Ni Bange Na Pombe tu Ndo Kazi.

- Akiishiwa Hata Nauli Na Hela Ya Sigara Anakusumbua Wewe.

Meanwhile, Mimi Sivuti Chochote wala Sinywi Pombe.

Naishi Nae Kwa Kuwa Na Mimi Mwenyewe Nimesaidiwa Sana Na Watu. Ingawa Ndo Hivyo Vingine Ni Kuvumiliana Tu.
 
Back
Top Bottom