Tabia ya Mume inanitesa

Tabia ya Mume inanitesa

Tabia ya mwanume kununa from know where naichukia sana ,akinuna na mimi nanuna mpaka atakapoamua kuacha na lazima aseme kilichomnunisha ,hapo kuna tatizo kuna kitu ila nduguyo hajakuambia vizuri
Hili ndiyo suluhisho.naona huyu dada anabembeleza sana ndiyo maana na mumewe anaona burudani kununa devj hebu mwambie huyu ndugu yako na yeye aamue kununa kama vile amegundua jambo fulani kuhusu mumewe, na yeye aji-keep busy na mambo mengine aone itakuwaje?
 
Last edited by a moderator:
hili ndiyo suluhisho.naona huyu dada anabembeleza sana ndiyo maana na mumewe anaona burudani kununa devj hebu mwambie huyu ndugu yako na yeye aamue kununa kama vile amegundua jambo fulani kuhusu mumewe, na yeye aji-keep busy na mambo mengine aone itakuwaje?
na sio eti anagonga mzigo biashara imeisha kesho tena ananuna akija akigonga wamchekea nakuambia hagongi mpaka aseme nini kimemnunisha hii ni generation nyingine kabisaa
 
na sio eti anagonga mzigo biashara imeisha kesho tena ananuna akija akigonga wamchekea nakuambia hagongi mpaka aseme nini kimemnunisha hii ni generation nyingine kabisaa
Umenikumbusha kitu.Hii nilishaikuta kwa ndugu yangu mmoja.na yeye alikuwa ana katabia ka-kununa. akichemkwa mwili, wife anampa huduma, akishapata mzigo anaendelea kununa.
mkewe akaleta malalamiko kwa wazee.na wazee wakauliza vipi usiku anakuchokoza, akawajibu "mzigo anakula kama Kawaida".wazee wakamfukuza huku wakimwambia "hebu ondoka, hapa hamna kesi kama huduma hii inapatikana".
 
Kero za muda mrefu ndani ya ndoa, ambazo zimekosa suluhisho husababisha hili; kuna wanawake huwa hawajali na kujihesabia haki, hivyo hata mume anaposhauri au kueleza jambo kama ni kero huwa hawajali; mwisho wake wanaume wengi sio wepesi wa kuongea mara kwa mara na badala yake anabaki kuishi ndani ya uchungu.
 
Nachukia sana tabia ya kununa.

But hii ya huyu ni kiboko.. Ananunaje from know where hata kama hakuna mkwaruzano??

Lakini pia najiuliza hizi tabia ni mpya kwa mkewe au alikuwa nazo tangu wakiwa wachumba??



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwanza, napenda kutoa pole kwa mhusika.
Lakini pia naamin, kwamba nivigumu sana kutoa ushauri katika jambo kama hili kwa kupata maelezo ya upande mmoja ndio maana hata mahakaman Hakimu husikiliza pande zote mbili. Zaidi ya hapo napenda kutoa LABDA zangu katika hili.

1. Labda yawezekana Mume amejua jambo ambalo Muke alilifanya siri katika mahusiano ya awali.
2. Labda yawezekana Mume ameona tabia flan kwa Mke ambayo haimpendezi na amejaribu kumrekebisha imeshindikana.
3. Labda katika maongezi Mume hapati ile stahili yake anapoongea na Mke, kwa mfano. mke kuwa na majibu ya mkato, mke kujiona anajua kila kitu (mke kukosoa kila jambo lisemwalo na mumewe), lakin pia hata dharau katika maongezi.
4. Labda Mke sio mtunza siri za ndoa, kwa maana ya kuongelea mambo ya ndoa kwa watu wengine na Mume kuzipata habari hizo.
5. Labda mke siomtekelezaji wa mipango mbalimbali ambayo huwa wanapanga kufikia malengo yao.
6. Lakini pia labda yawezekana mke hatimizi baadhi ya wajibu wake katika Ndoa kama Vile heshima, usikivu na kumtii mume.
Zaidi ya hapo simshauri kuacha ndoa yake, maana kila shetani na mbuyu wake,
Chamsingi ni kuendelea kutafuta chanzo cha tatizo ili uweze kupata ufumbuzi wake.
Nimtakie heri katika hili.
 
Kuna kipindi wanaume huwa tunakasirika mpaka unaamua kupiga kimya tu na wala siyo kununua kama unavyosema. Hiyo inaitwa sunctions kwa mwanamke hasa mwanamkea anapokosea nakujifanya hajui hilo kosa. Kikubwa awemuwazi kumwambia kitu alichokosea na kumuomba masamaha ili ya ishe. Akijifanya kana kwamba hakuna kitu, mwanaume anakuwa anajiuliza kana kwamba mkwewe hajitambui.
 
Saa nyongine mwenzie ananuna katoka kudaiwa kodi ya nyumba huko kwa small hausi! Nyie uanaume mnaona rahisi eeh? Ohoooo.
Nachukia sana tabia ya kununa.

But hii ya huyu ni kiboko.. Ananunaje from know where hata kama hakuna mkwaruzano??

Lakini pia najiuliza hizi tabia ni mpya kwa mkewe au alikuwa nazo tangu wakiwa wachumba??



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
habari zenu wapendwa!
jamani mie nimeletewa hili jambo na mdogo angu wa damu kabisa akiniomba ushauri na kwa kweli nimeona nije kwenu mnisaidie tumshauri cha kufanya kutokana na yeye kukata tamaa na kufikiria kuondoka kwenye ndoa yake.

Ameolewa miaka 3 iliyopita na ana mtoto mmoja.
Kwa muda mrefu tabia za mume wake zimekuwa zinamkosesha raha sana na kumfanya ajute kuolewa ingawa Ndoa ni baraka kutoka kwa Mungu.kwanza anasema kuna mengi sana anayofanyiwa na mume lakini hili kalinyooshea mikono,Mwanaume anaweza kununa hata wiki nzima bila kuongea ndani,akitoka kazini mwanamke atapika,atamuandalia maji ya kuoga,atakula na ataangalia TV huku kanuna ,akienda kitandani basi ndio kulala pembeni kabisa ya kitanda,ikitokea ukamgusa hata kwa bahati mbaya ntakavyosukumwa daah..

Alishajaribu sana kumuuliza mwenzie kama kuna tatizo na husema hakuna,akamwambia basi kama hakuna tatizo kwa nini awe hivyo mpaka mwanamke anakosa raha na amani moyoni?alimweleza kuwa tabia hiyo huwa inamkwaza na kujiona labda mwenzie hampendi tena na anamuona kero pale nyumbani,hapo Mwanaume anabadilika kwa muda na kuwa wa kawaida na baada ya muda mfupi hali ni ileile inajirudi.

Ukienda hata upande wa kufanya tendo la ndoa ni mpaka mwanaume aamue yeye,ameshamchunguza sana kama ana mwanamke mwingine lakini kwa asilimia 100 hana mtu.

kwanza anasema hakumbuki mara ya mwisho mwanaume amemkiss ni lini,amekuwa anamiss vitu vingi sana kutoka kwa mumewe lakini asilimia kubwa ya mume ni mkali na busy,anatamani hata wale sahani moja huku wanaongea lakini hataki.

Ikitokea mtoto akalia hata kidogo mume anamfokea mwanamke hata mbele za wageni..na pia hajali ni wakwe wala shemeji.

Na anachoshangaa nyumba anahudumia vizuri kwa chakula ingawa kikiisha mama huwa ana kazi ya ziada kujieleza katumiajetumiaje mafuta yakaisha na hii kumpelekea hata vikiisha kutoomba tena kwa hofu.


Ameshamsihi sana kuhusu hiyo tabia lakini mabadiliko yameshindikana ,kamwambia kama kamkosea ni bora akamwambia kwani yeye si malaika,lakini anasema hapana,amejaribu kutafuta detail za kazini kwake kama kuna tatizo lakini hakuna lolote na mara nyingi kununa huku hukufanyia nyumbani tuu.Nyumbani kwao na mume haoni wa kumuomba ushauri kwani wako familia ya Mama yake,dada yake na yeye wa mwisho kuzaliwa,Wote hao mara nyingi wana matendo ya kuwasiliana na mumewe kwa chinichini wakieleza shida zao na hawataki yeye ajue iwapo anawatumia fedha,huku hilo nalo linamsononesha kwa kuona mama mkwe labda anamuhisi yeye kuwa anaweza kumkataza mtoto ake asimsaidie,anatamani mama mkwe angekuwa huru kwake basi angeomba ushauri.

Kwakweli mie mwenyewe aliponisimulia mwili umesisimka na kuogopa nimtie moyo kwa neno lipi,Samahani kwa maneno mengi na kama ntakuwa nimechanganya maelezo mnisamehe...Karibuni tusaidiane kuokoa taasisi yetu ya ndoa.

Mbarikiwe sana kwa Michango mtakayotoa.


Jamani hili tatizo la kununa kwa wanaume lipo sana tu. Sio tu kwa wanandoa hata kwa wachumba, na linatesa sana na linaondoa raha ya mapenzi. Na wengi wenye tabia hii ni washamba hawajui majukumu yao kwa wapenzi wao. Mimi ninavyojua raha ya mahusiano yoyote ni mawasiliano. Kila mtu awe huru kuelezea pale ambapo anakwazwa. Mara nyingi watu wanaonunanua huwa ni KIBURI, hivyo unapaswa kwanza umsome mwenzi wako ni wa aina gani, vinginevyo utaishia kupigwa. Ushauri uliotolewa wa kuwaona viongozi wa dini naona unafaa, kama hatabadilika basi chukulia kuwa ni tabia yake mbaya ndio inayomsumbua. Achana naye ww endelea na maisha yako, ila usivunje ndoa yako kuna siku atajiona mjinga ataacha.
 
Huyo mwanaume ni made from iringa? mana watu wa huko ndo wana tabia ya kuacumulate vitu moyoni mwisho wananuna nuna mwanzo mwisho
mmh kama atakua wa iringa basi baada ya kununa hujinyonga lol , watani zangu mna mambo.
 
story kama hii ilishakuja humu jamvini; ningekuwa kama EMT ningeweza kuifukunyua na kuweka link.
Aaah ina maana ni copy paste ngoja basi niuchune lol tunahangaisha vichwa kumbe ilishaga jadiliwa. Leke nahumole
 

kama kanuna na yeye anune coz dume zima
kumnunia mkewe bila sababu,ingekua mimi mbona angeisoma!!khaaa!!
 
Back
Top Bottom