Tabia ya Mume inanitesa

Tabia ya Mume inanitesa

Aaah ina maana ni copy paste ngoja basi niuchune lol tunahangaisha vichwa kumbe ilishaga jadiliwa. Leke nahumole

ni copy and paste mwaya; itakuwa ilitolewa kwenye mitandao mingine basi mtu kaja kuileta humu.
Habari za familia?
 
mi kwakweli natamani sana kujua kuweka link!
kuna vitu huwa natamani sana kufanya ulinkisho lakini nashindwa !
na si wanijua nilivo na makumbukumbu!
we acha tu!
itabidi EMT atupe twisheni!
lakini hata mwaJ anajua ujue!tumwambie atufundishage!

Naogopa kuambiwa ninachakachua uzi ila mwanangu sijakusoma siku nyingi. Mei najua kuweka link lakini najua kienyeji tu sio kitaalamu. Mie huwa ninafungua hiyo link kawaida na kui-copy kutoka kwenye ile sehemu ya juu inayoonesha address (sijui kitaalamu hiyo sehemu inaitwaje) kisha ninai - paste kwenye comment yangu. snowhite nadhani umeelewa maana kwa vile mie sio teacher huwa nafundisha kwa njia ndefu.
 
Last edited by a moderator:
Wapendwa Amani iwe kwenu daima,
Naomba niwashukuru sana wote mliochangia kwa busara na hekima zenu ambazo zimekuwa ni mwanga kwa tatizo la mdogo angu kupata utatuzi wa yaliyojitokeza kwenye ndoa yake.

Kwa Upande wangu mniwie radhi kwa kutowajibu papo hapo mlipochangia kwani nilipatwa na masaibu ya ugonjwa na kulazwa hospital na sasa namshukuru Mungu naendelea vyema.

Nilichokifanya nimemwita mdogo angu na kukaa nae chini na kuhoji mengi sana ambayo kabla ya kuomba ushauri kwenu sikuwa nimemuuliza na hivyo nikapata historia yao ambayo imenifanya niamini kuwa yawezekana wana tatizo wote,Ingawa mume kununa si sahihi na sio pia njia ya kutatua tatizo.Mdogo angu na mumewe walikutana chuo wakichukua degree zao za kwanza,Mume alikuwa hivyo mara kwa mara, na aliongea nae kuhusu hiyo tabia na baadae akabadilika na kuiacha kabisa,mwanaume alikuwa mbele darasa moja na hivyo alipomaliza waliendeleza mahusiano mpaka pale mwanaume akapata kazi na msichana alipomaliza tuu chuo ndipo alipokuja nyumbani kwa wazazi kujitambulisha na taratibu zingine kukamilika na kufung ndoa.

Ndani ya ndoa kwa mwaka mzima hakurudia tena hiyo hali na baada ya kujifungua na mtoto kutimiza miezi 6 ndipo imejirudia tabia hiyo.Ameshamwambia mumewe kama kuna tatizo analo aseme lakini wapi...sasa miaka miwili hii ameona imezidi na hata kumkosesha raha ya ndoa kabisaaaaa.

Nimeona si vyema familia yetu kuingilia tatizo hilo la ndoa yake na nimemshauri arudi tena na aongee kwa upole na unyenyekevu kwa Mumewe kuhusu hali hiyo na jinsi inavyomtesa .Mwanaume asipobadilika basi awashirikishe waliowasimamia ndoa yao na iwapo yakiwa magumu kupata ufumbuzi zaidi ya hapo basi warudi kanisani kwa wachungaji ili kuona jinsi ya kusaidiwa .

Mwisho kabisa naomba niseme hivi kwa wanaJF kuna mchangiaji mmoja ameweza kusema kuwa story hii ilishaletwa hapa nimekopi,Kwa namna moja naomba niseme kuwa dunia ilivyo sasa ukiachwa na mume na mie nikaachwa na mume huku wote tupo JF ina maana kila mmoja akileta kilio chake hapa atakaewahi ndio yuko sahihi kaachwa na akija mwingine basi atakuwa amekopi?
Matatizo ya mahusiano,mapenzi kwa asilimia kubwa ni yaleyale tu na kamwe siwezi kuchukua tatizo la mtu asiyenihusu nikalileta hapa na kupoteza muda wangu bure wa kupambana na maisha,pia nathamini sana muda na michango ya wanaJF ambayo watu wenye busara huitoa.

Mbarikiwe sana.
 
Jamani hili tatizo la kununa kwa wanaume lipo sana tu. Sio tu kwa wanandoa hata kwa wachumba, na linatesa sana na linaondoa raha ya mapenzi. Na wengi wenye tabia hii ni washamba hawajui majukumu yao kwa wapenzi wao. Mimi ninavyojua raha ya mahusiano yoyote ni mawasiliano. Kila mtu awe huru kuelezea pale ambapo anakwazwa. Mara nyingi watu wanaonunanua huwa ni KIBURI, hivyo unapaswa kwanza umsome mwenzi wako ni wa aina gani, vinginevyo utaishia kupigwa. Ushauri uliotolewa wa kuwaona viongozi wa dini naona unafaa, kama hatabadilika basi chukulia kuwa ni tabia yake mbaya ndio inayomsumbua. Achana naye ww endelea na maisha yako, ila usivunje ndoa yako kuna siku atajiona mjinga ataacha.

Unakosea unaposea kununua, sema sanctions za mawasiliano baada ya kutenda kosa. Hii haiwezi kutokea kama hakuna kutokuelewana katika mahusiano.
 
Pole sana, japo sijui kama ndio wewe yamekukuta? Huyo dada aende kanisani, maombi ni silaha!
 
hapa naona kumbukumbu ya matukio ya nyuma huenda yameshika hatamu ndani ya ndoa yao.
Kuna uwezekano kuna mambo ambayo huyu dada amemfanyia au alimfanyia kipindi cha nyuma huenda hata wkt wa uhusiano wao na ikajenga chuki ndani ya moyo wa mwanaume.Mbaya zaidi iwe mwanaume naye ni mkimya basi hapa ndio mgogoro lazima ufike JF nasi tutakutuma urudi kwake kwani hatuachanishi ndoa bali kukushauri uangalie ni wapi ambapo unahisi kuna mwanya wa tatizo la mumeo.La sivyo,jiangalie kipindi cha nyuma na sasa,kuna watu wa ajabu sana ndani ya ndoa unakuta wkt wa mwanzo wa ndoa alikuwa hodari sana kwa mumewe anahakikisha mume amevaa vzr,amekula vzr,na kama haingii kazini asbh sana basi utakuta anaandaa kifungua kinywa mapema ila baada ya muda anaona havina umuhimu tena kwa kuwa ni mzoefu ndani ya ndoa.NDOA HAINA UZOEFU KILA SIKU KUWA MWANAFUNZI KWA KUWA PROFESSIONAL NYUMBANI,halafu nashangaa sana kumtetea kuwa hana mtu mwingine huko nje,hivi unatujua vzr wanaume??????
 
Pole sana kwa yaliyomsibu mdogo wako, me simshauri kabisaa aache ndoa yake bila kujua sababu inayomfanya mumewe awe vile.
Chamsingi awaite viongozi wa dini awaeleze iloswala mbele ya mumewe ninauhakika kama mke ndiye anayemkwaza ni lazima atasema na mambo yatakaa sawa.

Ndoa si lelemama mjue, ukiwa kwenye ndoa kuwa tayari kukabiliana na lolote otherwise usiingie kabisa!

...Unafikiri kuwaita wazee au viongozi wa dini itasaidia best......kwa kifupi huyo mmewe ana nyumba ndogo....na yuko smart kuliko maelezo....hajafanya uchunguzi wa kina....ila asikubali kuacha ndoa yake...katu katu....agande kabisa....
 
Hapo itakuwa ni history tuu imeharibu...kwa uzoefu wangu kama mshauri nasaha kesi kama hizi huwa zinatokana na historia iliyojificha..labda mwananmke anamabaya yake ya nyuma jamaa kayajua hivyo kagundua thamani halisi ya huyo mama....anahisi labda anadharaulika au anajidharau mwenyewe kwa kujua labda kila mtu anafill ile pinch anayofill yeye na hii inatokana na misimamo ya mtu binafsi kwa jinsi anvyoweza kuvalue thamani ya utu bora.espcly kama jamaaa anaamini katika ubora kabisa...1st class.ni complicated issue na inatibika..

Sababu ya pili kwa scenario kama hii mwanaume anakuwa shoga labda....kwa sababu wanaocheat huwa hawabehave hivi....
 
habari zenu wapendwa!
jamani mie nimeletewa hili jambo na mdogo angu wa damu kabisa akiniomba ushauri na kwa kweli nimeona nije kwenu mnisaidie tumshauri cha kufanya kutokana na yeye kukata tamaa na kufikiria kuondoka kwenye ndoa yake.

Ameolewa miaka 3 iliyopita na ana mtoto mmoja.
Kwa muda mrefu tabia za mume wake zimekuwa zinamkosesha raha sana na kumfanya ajute kuolewa ingawa Ndoa ni baraka kutoka kwa Mungu.kwanza anasema kuna mengi sana anayofanyiwa na mume lakini hili kalinyooshea mikono,Mwanaume anaweza kununa hata wiki nzima bila kuongea ndani,akitoka kazini mwanamke atapika,atamuandalia maji ya kuoga,atakula na ataangalia TV huku kanuna ,akienda kitandani basi ndio kulala pembeni kabisa ya kitanda,ikitokea ukamgusa hata kwa bahati mbaya ntakavyosukumwa daah..

Alishajaribu sana kumuuliza mwenzie kama kuna tatizo na husema hakuna,akamwambia basi kama hakuna tatizo kwa nini awe hivyo mpaka mwanamke anakosa raha na amani moyoni?alimweleza kuwa tabia hiyo huwa inamkwaza na kujiona labda mwenzie hampendi tena na anamuona kero pale nyumbani,hapo Mwanaume anabadilika kwa muda na kuwa wa kawaida na baada ya muda mfupi hali ni ileile inajirudi.

Ukienda hata upande wa kufanya tendo la ndoa ni mpaka mwanaume aamue yeye,ameshamchunguza sana kama ana mwanamke mwingine lakini kwa asilimia 100 hana mtu.

kwanza anasema hakumbuki mara ya mwisho mwanaume amemkiss ni lini,amekuwa anamiss vitu vingi sana kutoka kwa mumewe lakini asilimia kubwa ya mume ni mkali na busy,anatamani hata wale sahani moja huku wanaongea lakini hataki.

Ikitokea mtoto akalia hata kidogo mume anamfokea mwanamke hata mbele za wageni..na pia hajali ni wakwe wala shemeji.

Na anachoshangaa nyumba anahudumia vizuri kwa chakula ingawa kikiisha mama huwa ana kazi ya ziada kujieleza katumiajetumiaje mafuta yakaisha na hii kumpelekea hata vikiisha kutoomba tena kwa hofu.


Ameshamsihi sana kuhusu hiyo tabia lakini mabadiliko yameshindikana ,kamwambia kama kamkosea ni bora akamwambia kwani yeye si malaika,lakini anasema hapana,amejaribu kutafuta detail za kazini kwake kama kuna tatizo lakini hakuna lolote na mara nyingi kununa huku hukufanyia nyumbani tuu.Nyumbani kwao na mume haoni wa kumuomba ushauri kwani wako familia ya Mama yake,dada yake na yeye wa mwisho kuzaliwa,Wote hao mara nyingi wana matendo ya kuwasiliana na mumewe kwa chinichini wakieleza shida zao na hawataki yeye ajue iwapo anawatumia fedha,huku hilo nalo linamsononesha kwa kuona mama mkwe labda anamuhisi yeye kuwa anaweza kumkataza mtoto ake asimsaidie,anatamani mama mkwe angekuwa huru kwake basi angeomba ushauri.

Kwakweli mie mwenyewe aliponisimulia mwili umesisimka na kuogopa nimtie moyo kwa neno lipi,Samahani kwa maneno mengi na kama ntakuwa nimechanganya maelezo mnisamehe...Karibuni tusaidiane kuokoa taasisi yetu ya ndoa.

Mbarikiwe sana kwa Michango mtakayotoa.


HAPO KWENYE RED, hebu acha kuchekesha watu! huyo si ana mtu tu pengine watu halafu inavyoonyeha ni mwanaume ---- tu. Na kama hana mtu nje basi ni senge tu.

Nitaishia hapa maana ushauri wangu ni bora nibaki nao mwenyewe tu.

Ila kwa kifupi hilo lijadume lina mtu., ningekua mie nadhani mnajua ningefanya nini!
 
Back
Top Bottom