Tabia ya mtu haibadiliki

Tabia ya mtu haibadiliki

KalamuTena

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Posts
13,181
Reaction score
17,174
Ni jambo lipi au mradi gani aliowahi kuufanya John Pombe Magufuli, akiwa mbunge na sasa akiwa rais aliowahi kuubuni na kuukamilisha kwa utulivu, bila ya mitifuano na watu, wafanya kazi, contractors, raia au taasisi.

Ukiangalia barabara zilizojengwa, utakuta mikwaruzano kila sehemu. Naikumbuka ile Shell ya Mwanza; samaki wa Magufuli; wakazi wa Kimara; Kivuko cha Kigamboni, na mengi mengineyo.

Pamoja na kusifika kupiga kazi kwa nguvu, lakini weledi ni mpungufu anaposimamia kazi hizo. Kwake, kufuata taratibu zilizopo hakuna maana sana, mradi kazi inafanyika.

Kujifanyia yake nje ya katiba na sheria zilizopo ni kielelezo tosha cha tabia zake hizi mbaya.
Anasifika kwa kupambana na rushwa, lakini kwa taratibu zipi, na matokeo yake yatapimwa vipi?

Kuna taratibu za kisiasa zinazofahamika nchini, yeye kaja na njia zake za kununua wapinzani na vurugu tu nyingine nyingi.

Bunge na Mahakama zina taratibu zake, hata huko hakupaacha, mihuri ya utendaji wake wa vurugu inaonekana wazi kabisa.

Sasa tabia hizo hizo zinajirudia wakati akiwa rais. Kila sehemu ni mikwaruzano tu, hakuna linalofanyika bila kupigishana kelele, kutumbua, na mengine yasiyofaa.

Hili la COVID-19, ndilo linaloonyesha wazi kabisa tabia yake ya kutotaka kufuata taratibu. Yeye anajipigia tu anavyoona/hisi inafaa hata mahali asipokuwa na ufahamu napo

Hatari kubwa zaidi inayotokana na tabia yake hii ya kutofuata taratibu ni kwamba hata kama Taifa, sote tumeanza kuangukia kwenye tabia hiyo hiyo ya kutofuata taratibu zinazoeleweka katika kufanya mambo yetu; na hii imetugharimu na itaendelea kutugharimu sana tusipobadilika haraka.

Kuna umhimu mkubwa sana, kama taifa, turudi kwenye kufanya kazi zetu kwa kufuata taratibu zilizowekwa. Hili lisisitizwe sana hasa kwa watoto na vijana ambao bado wapo mashuleni. Taifa haliwezi kujengwa kwa kufanya mambo bila ya mipangilio isiyoeleweka.

Najua chini ya utawala wake hakuna kitakachoweza kubadilika. Bahati yetu kama taifa, huyo mwingine atakayekuja baada ya Kajoni, awe ni mtu msikivu na awe na ari ya kutuweka kwenye taratibu zinazoeleweka.
 
Kiukweli binafsi sijawahi kumkubali huyu kiongozi hata kidogo. Hafuati kanuni, taratibu na sheria ya chochote.

Hajali watumishi, hajawapandisha madaraja wala mishahara Miaka mitano sasa.

Anaona fahari kutumbua watumishi hata kwa vimakosa kidogo. Hana utu hata kidogo.
Kwa hili la corona tutadharaulika na Dunia nzima.
 
The end justifies the means.

Amefanikiwa kwenye mengi na huwa anayaongea sana kwenye hotuba zake.

Jaribu kurejea.
Mafanikio ni mazuri lakini yasiwe chini ya mafuvu na mabega yanayovuja damu.. Mafanikio yasivae viatu vyenye soli yenye misumari iliyochongoka... Itawachoma na kuwaumiza wengi matokeo yake badala ya furaha hugeuka jinamizi linalotisha sana

Jr
 
Ukweli mchungu mafanikio yanahitaji mtu ajitume na atoke machozi, jasho na damu!

Mafanikio hayaji hivihivi! 😝
 
Wewe umeangalia mapungufu tu, rejea na upande wapili kama hauoni basi ni bahati mbaya
 
Umeeleweka na nimekuelewa, maana tunaposema Serikali ni mifumo na ili mifumo ifanye kazi lazima sheria, kanuni na taratibu zifanye kazi na kuheshimiwa. Nje ya hapo tutakuja kushangaa kitakachokuja kutokea huko mbeleni ndani ya Taifa letu.
 
Mimi nakumbuka na sitasahau umeme (TANESCO). Sijui kwanini walikuwa wanakatakata na kutusababishia kutumia majenereta. Mpaka Wakurugenzi wakuu (km Mrema) alimgomea Rais wetu ili aendelee kukata umeme

Leo umeme chee, friji haiozeshi tena JF siikosi kama si mvua naweza kwenda popote TZ na Vits
Hayo mabaya nawaachieni lkn angekuwa Rais mwingine sijui matajiri wangetuweka wapi?
 
Hili la covid 19 linaeza tuumbua huko mbele, unless tuwe na bahati sana ,ila pamoja na kufundishwa na wataalamu, tumeamua kuchukua njia za miujiza kupambana na covid19, badala ya Ile zinazopendekezwa na wataalam, na kibaya zaidi bado kuna watu wanaamini hilo.

Jana inasemekana wagonjwa wamevunja mlango huko Amana, hii si dalili nzuri, inaonekana ukweli ni kuwa huduma za afya zimekuwa exsausted, mwanzo kabisa wa mpambano, katika kipindi amabapo pengine tulikuwa tunazihitaji sana .

ĺ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kalamu1,
Alipokuwepo Jakaya Kikwete watu wakawa wanajipigia fedha,na wengine kubeba kwenye sandarusi mkawa mnasema rais gani huyu mpole anacheka cheka tu.

Amekuja huyu mzee wa kazi mnaanza maneno mengine. Rais lazima awe mkali na lazima aogopwe ili mambo yaende. Sasa ile Petrol station kama ilikuwa kwenye hifadhi ya barabara we ulitaka iachwe? I am not a politician but i have common sense.
 
Ukinipa mifano mibovu yote, halafu uniambie nichague moja nafuu, nakuona huna umakini wowote.

Huo mfano wa kituo cha petroli nao umeutoa kwenye 'context' iliyotumiwa. Kukfanya mambo kwa kukiuka taratibu zilizopo, hata kama haina lazima.

Wewe hujui huyo aliyevuniwa mali zake pasipo kufuata taratibu alifidiwa?
 
Kwani sheria inasemaje ukijenga ndani ya hifadhi ya barabara? Ukivunjiwa unalipwa?
 
Back
Top Bottom