wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,931
- 4,550
Binadamu anapokufa mwili wake huachana na roho,(nafsi /uhai) mwili huo hubaki kasha tupu lisilo na chembe yoyote ya uzima.
Na roho yake huenda sehemu inayostahili kulingana na matendo yake duniani.
Roho ndo uzima, roho ndo nafsi kamili, roho ndo uzima wenyewe. Kifupi ni kwamba binadamu hufa mwili ilihali roho ikiendelea kuishi katika ulimwengu mwingine wa roho ambao huwezi kuuona kwa macho ya damu na nyama.
Binadamu akifa anatisha, ukiambiwa ulale chumba kimoja na maiti huwezi, Hata Kama ni maiti ya mtoto bado utaogopa tu .
Sura ya maiti hukaa kwenye kumbukumbu ya ubongo kwa muda mrefu sana, kwa mtu yoyote atakayeikodolea macho maiti usoni.
Tabia ya kuaga maiti haina mashiko na sababu yoyote ile.
Kuaga maiti ni kuisanifu maiti, unaagaje kitu kisicho na uhai? Ni kipi kinakusaidia kumwangalia mfu?
Napenda sana utaratibu wa ndugu zangu waislamu, wao huiandaa maiti na kwenda kuzika basi, kuliko tabia ya mabwana wale wanaopenda kupanga foleni ili kuaga maiti msibani, foleni kubwa utadhani walimu wanachukua mshahara kwenye ATM ya NMB.
Mwisho wake huwa ni mayowe, watu kuzimia na kuanguka hovyo msibani.
Sura ya marehemu unaitakia nini? Unamuaga marehemu ili iweje?