Tabia gani usiyoipenda sebuleni?

Tabia gani usiyoipenda sebuleni?

Inasikitisha sana...
Ila mimi nipo cool soon, mgeni/wageni wanapokuja kwangu... Sinaga muda wa kuangalia anafanya nini au atafanya nini...

So nakuaga poa...
Hata mahondaw ananijua vizuri nilivyo...


Cc: mahondaw
 
Mi sipendi(mwenyeji) nije kwako alafu unakuwa unalazimisha niongeze chakula...unakuta mtu anasema mgeni mbona kidogo hivo jamani ongeza bhaassii wakati mwingine anadiliki hata kukuongezea [HASHTAG]#sipendi[/HASHTAG]
 
Mi sipendi tabia ya kipande kikubwa mamamwenye nyumba kukiwekeka chini a lafu juu unaweka vipapatio alafu tukicharuacharu unanuna si uweke juu vipande vikubwa vote hahahaha
 
Habari zenu wa Jf
Kuna tabia ambazo wageni wamekua wakifanya masebuleni mwetu na sisi kiukweli hatuzipendi ila tunashindwa kuwaambia coz ni mgeni unaogopa kumuuzi.
Baadhi ya tabia zinazonikera mimi ni kama ifuatavyo
1. Mgeni kupandisha miguu juu ya kochi, inakera, kama unajisikia kukunja miguu yako si bora ukae chini basi uikunje vizuri. Kuliko kupandisha milonjo yako kochini.

2. Wakati wa chakula labda umekaanga kuku umeweka kwenye bakuli self service unamkaribisha mgeni badala achukue vipisi asepe yeye anaanza kuchakura chakura yani atafukua mpaka kipande cha chini sijui ndio anatafuta kikubwa zaidi inaboa. We ukikaribisjwa fika chukua sepa.

Je wewe ni tabia gani hupendi kutoka kwa mgeni wako? Funguka hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mgeni umemkaribisha ndan anaingia, ata kabla hajaketi kwny kochi mimacho kodoooo kuangalia vilivyomo ndani..... Wananiboaga sana wageni wa aina io asee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wageni wengine wanatema miguu akivua viatu yaani mpaka kero.... bora hata waingiage na viatu
Mgeni wa namna hiyo usipate tabu,, Mpe maji asafishe miguu yake, Viatu vyake weka Juani, kama linaangaza vema,
 
Hapo ndipo wenyeji wetu huwa mnayumba kunanyumba moja nilikaribishwa kwa mbwembwe nikawa nazingua dk yamwisho nikajisemea nisije nikaonekana nimewadharau ngoja niingie basi wakati wakukata ukali nikapewa kisu wa kwanza ile kufunuliwa poti nikakuta kilichomo ndani hakiakisi watu tulio lizunguka hilo poti lakini kiukweli ilibidi wajute tu maana baada ya mimi kukata niliona wengine wakiondoka kuelekea nje
Uwiiiiiiiiiiiiii huo ulaji wa kutia kijiugali kijidogo kwenye hotpot halaf walaji wengi siupendi min huo ni uchoyo
 
Kuwa remote controller
Unakaribishwa sehemu, mwenyeji wako anakuacha sebuleni na Tv yenye Tamthilia za wale Jamaa au Bongo Movie, yeye yupo busy kukuandalia ulichofuata au lah, Chakula huko jikoni, Utakuta nimezima Tv mkuu!!
 
Mgeni au jirani kuingia sebuleni kupiga stori Mara mwanae kuibuka gafla alafu kachafu vumbi au matope alafu mamake kuanza kumnyanyua na kumweka kwenye kochi lenye vitambaa vyeupe!! Nawapenda watoto ila hapa wananikeraga!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom