Tabia chafu ya TBC

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,407
1,110
leo muda wa saa 5 kasoro 10,chanel ya TBC1,wamekata matangazo maksudi ili tusione hotuba ya mh.zitto kabwe na hili jambo linatokea mara kwa mara.mnaonaje kuhusu hili?ni nani anahusika kukata matangazo ya bungeni?na hii sio mara ya kwanza ,hata juzi kati siku anaapishwa Joshua nassari walizuia sauti ili tusisikie alivyokuwa akishangiliwa.jamani wanaJF,tufanyeje kuhusu hili?hii TBC si ya kodi zetu?
 
TBC=CCM. Inatakiwa ipelekwe hoja binafsi bungeni kuhusu CCM kuimiliki TBC indirect.
 
ndio,wabunge wa CDM watakuwa hawalitambui hili,wenye links nao wawajulishe
 
Mimi naangalia TBC chanel 143 kupitia DSTV na hamna saa matangazo yamekatika. Labda tatizo litkuwa la antena yako au king'amuz chako
 
Naona dawa ni kutia virus ktk computers za TBC1 ili kuwalostisha wara kwa mara ili wapotee kabisa, vinginevyo wajanja wanaweza kuwapata wadada/kakas wanaofanya kazi hapo then kutumia nafasi ya kujua TBC1 na hatimaye to bring it to ZERO start.

Maoni yangu.
 
kweli kabisa. TBC wamekuja na kamtindo ka kuminya sauti wakati kitu HOT kinazungumzwa. Mnyika na Sanya wamefanyiwa hivyo.
 
Nadhani kwa wale wanaotumia antenna peke yake bila ya king'amuzi ndo wamepata tatizo hilo.. Kwa wanaotumia ving'amuzi wanaendelea kuona vizuri kabisa..
 
Magazeti siku hizi wanasoma Uhuru,Mzalendo,Zanzibar leo Habari leo then kwisha kazi
 
au tuandae maandamano dhidi ya TBC tunajipanga watu wa dsm tunatembea hata km2 tu,tunaita press,au tufanya ka-movement flani hivi
 
Mimi naangalia TBC chanel 143 kupitia DSTV na hamna saa matangazo yamekatika. Labda tatizo litkuwa la antena yako au king'amuz chako

Kweli nimeamini upo kazini!hata hili hutaki kukubali?
 
leo muda wa saa 5 kasoro 10,chanel ya TBC1,wamekata matangazo maksudi ili tusione hotuba ya mh.zitto kabwe na hili jambo linatokea mara kwa mara.mnaonaje kuhusu hili?ni nani anahusika kukata matangazo ya bungeni?na hii sio mara ya kwanza ,hata juzi kati siku anaapishwa Joshua nassari walizuia sauti ili tusisikie alivyokuwa akishangiliwa.jamani wanaJF,tufanyeje kuhusu hili?hii TBC si ya kodi zetu?
Suala ni mfumo kandamizi wa hawa watu wa uhasama wa taifa,wao ndio wanaratibu matangazo yote haya wako kila sehemu hapo dodoma kazi yao ndio hiyo wakimuamuru lolote msimamizi wa matangazo basi hana ubishi nalo.halafu kuna kitu kingine cha kujiuliza kwamba inakuwaje ITV hawajihusishi kabisa na matangazo haya? Na je hatuna wazalendo wengine nchini wasionufaika na hi mifumo mibovu nchini ili wawekeze kwenye hii tasnia ya Haabari ili wananchi tupatew haki yetu ya msingi?
 
tunawashauri ccm waisajili tbc kama shirika lao la chama tujue moja.over
 
leo muda wa saa 5 kasoro 10,chanel ya TBC1,wamekata matangazo maksudi ili tusione hotuba ya mh.zitto kabwe na hili jambo linatokea mara kwa mara.mnaonaje kuhusu hili?ni nani anahusika kukata matangazo ya bungeni?na hii sio mara ya kwanza ,hata juzi kati siku anaapishwa Joshua nassari walizuia sauti ili tusisikie alivyokuwa akishangiliwa.jamani wanaJF,tufanyeje kuhusu hili?hii TBC si ya kodi zetu?

Hawa jamaa ipo siku watakumbana na Nguvu ya Umma kama ilivyo kwa Marine Hasan marine siku ya uzinduzi wa Kampeni 2010.

Hawa jamaa wanafanya kazi kwa maslahi ya wakoloni na Mafisadi wa nchi yetu.

Can you imagine wanaonyesha filamu badala matukio muhimu kwa jamii.

Mfano ile Meli ya ZNZ imezama wao wanaonyesha Taarab na mikanda ya Kizungu wakati watu tunataka kujua hatima ya waTZ wenzetu.

Siku ya Uchaguzi Arumeru badala ya kutuonyesha wao wana sakata rumba na kukata Viuno.

Pongezi kwa StarTV at least 70%, na ITV at least 40% ya kuwaridhisha watZ.
 
Jamani nakiri tbc huwa wana mapungufu sometimes lakini leo toka bunge limeanza saa 3 asubuhi naangalia na bado naangali mpaka muda huu sijaona mahali mawasiliano yamekatika. Nakushangaa. Kuna mtu juu kasema anaangalia kupitia dstv mimi binafsi natumia dish la kawaida na wala mawasiliano hayajakatika.
 
Nadhani kwa wale wanaotumia antenna peke yake bila ya king'amuzi ndo wamepata tatizo hilo.. Kwa wanaotumia ving'amuzi wanaendelea kuona vizuri kabisa..
Thanx mkuu na wewe kwa kuliona hili.
 
Mimi naangalia TBC chanel 143 kupitia DSTV na hamna saa matangazo yamekatika. Labda tatizo litkuwa la antena yako au king'amuz chako

Mie natumia king'amuzi(Digitareee) fresh matangazo ya TBC1 hayajakata labda Antenareee yake kimeo au Matangazo ya Analogaree yalikata.
 
Back
Top Bottom