Tabasamu la Tulia

Tabasamu la Tulia

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,096
Reaction score
828,932
Ni mara chache mno kukuta bosi na msaidizi wake wakipendana na kuwa marafiki..wengi hawapendani kabisa..! Ukikuta hao wawili ni washikaji basi tambua kuna mambo yanayowaunganisha, Ama mmoja ni superior kuliko mwingine na mwingine hana kinyongo

Mabosi wengi muda mwingi hawawaamini wasaidizi wao wakuu wakiamini kuwa wanawapangia mbinu za kuwapokonya kiti... Wasaidizi wengi hawawapendi mabosi zao wakiamini kuwa wao ni bora zaidi na hupenda kuwasimanga kila wanapopata nafasi

Matamanio kaumbiwa mwanadamu.. Daima hutaka zaidi na hapati vyote mpaka kifo.. Madaraka ni matamu hasa madaraka ya kisiasa yasiyohitaji ujuzi wa kusomea darasani! Kwa kila nafasi unayopanda unatamani na ya juu zaidi na aliyeko hapo unatamani umpopoe mawe aanguke ukae wewe
Kufa ni kufaana ndio maana kuna urithi na mirathi, kugawana vya marehemu na vingine kurithishana.. Mali hata ukuu.. Si wote waliao misibani ni vilio vya majonzi na huzuni.. Wengine ni machozi ya mamba na vilio vya furaha!

Kwa makasiriko haya.. Kwa magumu haya.. Tulitegemea kuona wale tulio pamoja walau tukipeana neno la faraja.. Lakini aah wapi tuko busy tukijipanga na kuomba sana ili litokee la kutokea lile linalotupa matamanio ya kila siku... Mimi ndio nafaa kukaa pale...!

Maono ni mengi lakini machache hubeba unabii

 

Attachments

  • Screenshot_20220106-050627.jpg
    Screenshot_20220106-050627.jpg
    23.7 KB · Views: 69
Sasa huyo Boniface ndio source yako kweli? bora angeandika Chahali ningeamini.

Hivyo katika akili za kawaida barua usiku unakabidhi kwa walinzi au kuna office za serikali 24 hour kama kituo cha kuuza mafuta?

Taarifa ambazo hatujathibitisha kutoka kwa mtu wa karibu wa Speaker Ndugai amenidokezea kwamba Spaker Ndugai aliandika na kukabidhi barua ya kujiuzulu u speaker wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tutawajuza mara tutakapoiona hino barua au baada ya kupata taarifa zaidi

Mimi nipo nae jirani hapa sijaona dalili zozote, ni vigumu kuachia top layer halafu aende wapi jua ana kundi kubwa kuliko lile la Lowassa au la G55 licha la humu ndani JF,
nilichosikia ataomba tena msamaha hadharani kabla ya Kikao cha 29/ Jan
 
Mimi nipo nae jirani hapa sijaona dalili zozote, ni vigumu kuachia top layer halafu aende wapi jua ana kundi kubwa kuliko lile la Lowassa au la G55 licha la humu ndani JF,
nilichosikia ataomba tena msamaha hadharani kabla ya Kikao cha 29/ Jan
Kusema Ndugai ana kundi kuliko la Lowasa ni propaganda tu.

Hakuna mwanasiasa ndani ya ccm kwa miaka ya hivi karibuni ambaye anaweza kuwa na ushawishi kama wa Lowasa, na ukae ukijuwa ushawishi ndani ya ccm unaendana na ukwasi ulionao.

Ndugai hawezi kuwa na influence hata kwa wabunge wa Dodoma tu, achilia mbali bunge zima.

Ingekuwa ni wakati wa Samwel Sitta ningekukubalia kwamba ana influence kwa wabunge wake, huyu Ndugai labda wale covid 19 aliyowaweka yeye bungeni ile ndio base yake.
 
Back
Top Bottom