Barua Kuhusu Nyaraka za Nangwanda Lawi Sijaona

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
BARUA KUHUSU NYARAKA ZA NANGWANDA LAWI SIJAONA

Barua hizi tatu zinajieleza vizuri na zinajitosheleza kueleza tatizo linalokabili uhifadhi wa historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Katika barua ya kwanza kwenda CCM Sijali Sijaona anatahadharisha kupotea kwa historia muhimu ya sehemu ambayo baba yake, Nangwanda Lawi Sijaona na wazalendo wengine walipoanza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya chama cha TANU.

Jibu ya barua hii kutoka CCM ambayo Sijali kaipa jina ''Kichekesho,'' barua inazungumza kuhusu, ''miaka 30 ya uhuru,'' ilhali mwaka wa 2011 Tanganyika ilikuwa inasheherekea miaka 50 ya uhuru.

Barua ya Sijali kujibu barua hiyo Sijali anaeleza masikitiko kuwa katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika hapakutajwa mzalendo hata mmoja aliyeongoza harakati za kudai uhuru kutoka Kusini.

Kusini TANU ilipata upinzani mkubwa kutoka kwa Wamishionari wa Peramiho wakiwatisha wananchi kutojihusisha na TANU kwani inataka kuanzisha vita vingine vya Maji Maji.

Ilikuwa mmeshionari kutoka Peramiho ndiyo aliwaendea makamanda wa Maji Maji waliohukumiwa kunyongwa kuwaeleza kuwa endapo watakubali kubatizwa hawatanyongwa.

Makamanda hawa wote zaidi ya 60 walinyongwa na Wajerumani na kuzikwa katika kaburi la halaiki isipokuwa Nduna Abdulrauf Songea Mbano.

Katika hawa makamanda yupo mwanamke Khadija Mkomanile.

Historia ya kusikitisha.

Lindi mjini kazi kubwa ya kuhamasisha wananchi ilifanywa na Salum Mpunga na Yusuf Chembera.

Angalia picha zao katika jalada la kitabu hapo chini.

Kulia juu ni Salum Mpunga na kushoto ni Yusuf Chembera.

Salum Mpunga alikuwa dereva wa lori na Yusuf Chembera akifanya kazi Canteen ya Lindi Welfare Centre.

Hawa katika utoto wao walisoma madrasa ya Sheikh Muhammad Yusuf Badi na ndiyo waasisi wa TANU Southern Province 1955 na vijana hawa ndiyo waliomtia mwalimu wao katika harakati za kupigania uhuru.

Kusini kuna historia kubwa ya ukombozi wa Tanganyika.

1696653229903.jpeg
1696653299663.jpeg

1696653340933.jpeg
 
Back
Top Bottom