Taazia: prof. Immanuel Kilima Bavu hupigi goti kwake kusoma ila atakuacha na elimu ya kudumu

Rohombaya,
Kuna mtu aliniuliza kwa nini kila unapotaja historia ya TANU lazima umtaje na Abdul Sykes?

Mimi nikamjibu kwa kumuuliza swali.

Unaweza kuandika historia ya Azimio la Arusha bila kumtaja Nyerere?

Unaweza kuandika historia ya TANU bila ya kumtaja Abdul Sykes?

Watu wanatajwa kwa stahili zao.
Ikiwa unaona nakosea nifahamishe.

Nyerere na BAKWATA historia inawataja kwa stahili zinazowagusa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah... Sheikh,
Tatizo langu siyo kuwataja....ni namna unavyowataja...aghalabu huwataja kwa mapungufu....hata hivyo uchambuzi wako ni mzuri...tatizo ni uchambuzi elemevu...hauna haki...

Sent using Beretta ARX160
 
Abdul Sykes na yeye alikuwa anavuta sigara " clipper" kama Nyerere?
Laki...
Hii ni taazia ya Prof. Bavu kwa bahati mbaya umeleta habari za Abdul Sykes, Julius Nyerere na Sigara Clipper.

Hapa si mahali pake lakini nitakujibu.

Swali lako kwanza umekosea kuliuliza.
Kuwa Abdul anavuta sigara gani si swali ambalo nitalijibu na barza itakuwa imeelimika.

Kuna mtu kasoma ile makala yangu na alipoona kuwa Mwalimu baada ya kuona rafiki yake Hamza Mwapachu yamemsibu maradhi na akafariki na sababu ni uvutaji, yeye akaamua kuacha sigara ili kulinda afya yake.

Huu ulikuwa uamuzi wa busara.

Sasa nataka nikueleze kitu ambacho siku zote kikiwataabisha viongozi wa TANU pamoja na Abdul Sykes.

Hii ilikuwa usalama wa Nyerere kuwa vipi watamlinda maadui wasimuue.

Ajabu hawa viongozi hawakufikiria kuwa uvutaji wa sigara wa Nyerere pia ni moja ya tishio kwa maisha ya Mwalimu.
Wao walichokiogopa zaidi ilikuwa Nyerere kulishwa sumu.

Mwalimu alikuwa akiwa Iringa basi chakula chake popote pale kilikuwa kinasimamiwa na Abbas Max na walichokuwa wakifanya ni Abbas Max kubadilishana sahani na Nyerere baada ya chakula kishatengwa dakika ya mwisho wanataka kula.

Mwalimu alikuwa akimuuliza Abbas Max ana uhakikika gani na ''ujanja,'' ule?

Abbas Max alikuwa akijibu kuwa hakuna mtu anaeweza kufikiri hata kwa mbali kumdhuru yeye Iringa nzima kwani wote wale walikuwa ni ndugu zake na ikiwa Mungu apitishie mbali limemkuta la kumkuta basi koo zitamalizana kwa visasi.

Alikuwa akimwambia Nyerere kuwa hakuna atakaeweza kupenya katika ngome ile yao ya Wahehe.

Tabora Mwalimu katika mkutano wa Kura Tatu mwaka wa 1958 alikuwa akipikiwa chakula chake na Jaffari Iddi na yeye alilishwa yamini kuwa hatomdhuru Nyerere.

Nimekutangulizia mkadama huu ili ujifunze kufikiri mbali zaidi na uulize maswali yenye maana.

Sasa hata nikikuambia kuwa Abdul Sykes alikuwa anavuta Pall Mall taarifa hii ina maana gani kwako na kwa wasomaji?

Iko siku Nyerere katika ''retreat,'' nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya kula chakula cha mchana walipomaliza kikao Nyerere akashikwa na tumbo kali sana akawa amelala kwenye sofa anaugulia.

Taharuki kubwa ikatokea kwa haraka watu wakadhani Nyerere kalishwa sumu.

Mama yake Mwalimu alikuwapo uani na akina mama wengine ambao ndiyo walikuwa kila pakiwa na kikao pale kwa Abdul wanakuja kupika.

Bi. Mugaya Nyang'ombe, mama yake Mwalimu alipoona hali ya mwanae akawa analia ana hakika mwanae katiliwa sumu kwenye chakula inabidi wanawake wenzake pamoja na mama yake Abdul Bi. Mruguru bint Mussa wamtulize.

Swali kubwa likawa nani anaweza kumtilia sumu Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes kwani kwenye nyumba ile Nyerere alikuwa kazungukwa na nduguze watupu?

Hii ilikuwa siku za mwanzo za TANU na Nyerere keshakwenda UNO.

Yaliyobakia ni historia.

Ndugu yangu Laki wewe unauliza habari za sigara.

Nikikuambia alikuwa anavuta Sigara Kali....
 
Mzee Mohammed Said ni aina ya watu unayekutana naye katika maandishi juu ya chochote akakusababisha UJUE KUWA HUJUI na mara nyingine KUKATA TAMAA YA KUJIFUNZA kwani kina anachokwenda katika kulisema jambobna ushahidi ataotoa, havita kuacha tu kinywa wazi bali kitakufikirisha na jibu lake ni ANAJUA HADI ANAKERA.

Allah akupe umri mrefu Akhy ili tuendelee kula matunda ya mti huu.

Sent using Jamii Forums mobile appCronell
Chere...
Najua hadi nakera...
Nacheka peke yangu kama mwehu kwa maneno haya hata sijui niseme nini zaidi ya kumshukuru Allah.

Wakati wa sakata la Salman Rushdie mwaka wa 1989 Prof. Ali Mazrui alialikwa Cornell University, New York kuzungumza.
Basi mkaribishaji akamweleza Prof. Mazrui kwa sifa zake na akampamba mwisho wake.

Mazrui anamsikiliza hadi akamaliza.

Aliposimama kuongea Mazrui akamshukuru kwa kusema, ''Thank you for that generous introduction.''
Maneno hayo tu basi.

Prof. Mazrui kama wewe nilipokusoma ni bingwa wa kucheza na lugha.
Mmeshahabiana kwa hilo.

''Generosity,'' kwa Kiingereza ni ukarimu.

Kuna maneno Mazrui angeweza kuyatumia kumshukuru yule bwana lakini kama Mswahili na yeye mgeni pale Cornell na mgemi lazima akirimiwe ndipo nadhani akaamua kutumia neno hili kuwa kwa utangulizi ule yeye kakirimiwa kama vile mgeni kupewa chai.

Sasa wewe umetumia neno, ''kukera,'' huna maana kama ''kuchukiza,'' ila unataka kusema kuwa ''imefurtu ada.''
Ahsante sana ndugu yangu.

Namshukuru Allah kwa yote.
 
Maprofesa Wa enzi hizo umeme ukizimika ofisini Hamna standby generator wala Hamna solar iwe ofisini au nyumbani akifundisha kutengeneza board paper!!!!! Board members Wa enzi hizo hawana laptop zenye betri na hawana email uwarushie hizp board paper wasome kwenye laptop au simu zao!!!

Kweli kila zama na kitabu chake ndio maana kustaafu muhimu kupisha damu mpya
 
Chere...
Najua hadi nakera...
Nacheka peke yangu kama mwehu kwa maneno haya hata sijui niseme nini zaidi ya kumshukuru Allah.

Wakati wa sakata la Salman Rushdie mwaka wa 1989 Prof. Ali Mazrui alialikwa Cornell University, New York kuzungumza.
Basi mkaribishaji akamweleza Prof. Mazrui kwa sifa zake na akampamba mwisho wake.

Mazrui anamsikiliza hadi akamaliza.

Aliposimama kuongea Mazrui akamshukuru kwa kusema, ''Thank you for that generous introduction.''
Maneno hayo tu basi.

Prof. Mazrui kama wewe nilipokusoma ni bingwa wa kucheza na lugha.
Mmeshahabiana kwa hilo.

''Generosity,'' kwa Kiingereza ni ukarimu.

Kuna maneno Mazrui angeweza kuyatumia kumshukuru yule bwana lakini kama Mswahili na yeye mgeni pale Cornell na mgemi lazima akirimiwe ndipo nadhani akaamua kutumia neno hili kuwa kwa utangulizi ule yeye kakirimiwa kama vile mgeni kupewa chai.

Sasa wewe umetumia neno, ''kukera,'' huna maana kama ''kuchukiza,'' ila unataka kusema kuwa ''imefurtu ada.''
Ahsante sana ndugu yangu.

Namshukuru Allah kwa yote.
Nafarijika sana ninaposoma maandishi yako maana yamejaa busara na mafunzo ya kutosha. Ningependa nijue vitabu ulivyoandika hasa vinavyohusu masuala ya Afrika na Tanzania ili nione namna ambavyo naweza kuvipata kwa ajili ya kujiongezea maarifa. Hongera sana mzee Mohamed Said.
 
Mtego...
Screenshot_20200506-090316.jpg
20200306_100857.jpg
20200306_104306.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii maana ya "futuristic" Professor Bavu aliitoa wapi? Mtu kukwama kwenye kazi yako sababu umeme umekatika, halafu ukaamua kwenda kumalizia hiyo kazi mahali ambapo kuna umeme wa generator ndiyo "futuristic"? Kwahiyo nikishona barakoa yangu ya kitambaa kwa fundi cherehani sababu sina uwezo wa kununua disposable barakoa za Mchina kila siku, basi huo ni mfano wa "futuristic" thinking?
 
Ndjabu...
Taazia huwa haijadiliwi.

Unaweza kuleta hili pengine ambako hatutomgusa marehemu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rohombaya,
Kuna mtu aliniuliza kwa nini kila unapotaja historia ya TANU lazima umtaje na Abdul Sykes?

Mimi nikamjibu kwa kumuuliza swali.

Unaweza kuandika historia ya Azimio la Arusha bila kumtaja Nyerere?

Unaweza kuandika historia ya TANU bila ya kumtaja Abdul Sykes?

Watu wanatajwa kwa stahili zao.
Ikiwa unaona nakosea nifahamishe.

Nyerere na BAKWATA historia inawataja kwa stahili zinazowagusa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Au unawezaje kuitaja awamu ya tano bila kumtaja JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom