Allah ampe afya njema mwalimu wetu Prof. Kissinger na azidi kumfurahisha

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
PROF. KISSINGER

Leo mimi, Hamisi Hababi na Sheikh Taufik Kazaliwa tumemtembelea mwalimu wetu Prof. Kissinger.

Kwanza tulikuwa ndani tukapata darsa la Komredi Abdulrahman Babu na Mwana ASP na Memba wa Baraza la mapinduzi Seif Bakari.

Prof. Kissinger akatupitisha kwa ufupi kwa Abdulrahman Mohamed Babu akasema ni sharifu wa aina yake kabisa.

Mzee Kissinger akatukumbusha vijana wawili waliovuma Dar es Salaam ya 1960 Awadh Gesani mchezaji kandanda Yanga na Hussein Shebe.

Awadh katangulia mbele ya haki na alipita kaburini kwake siku za kaburini na Abdallah Tambaza wakafanya dua.

Hussein yu hai anaishi Switzerland kwa miaka mingi lakini hapungui Dar-es-Salaam kila mwaka anakuja kufunga Ramadhani Dar-es-Salaam na Zanzibar.

Kisha akatupeleka kwa Seif Bakari.

Akatuchekesha akasema, "Seif Bakari alikuwa hakukopeshi ukimtukana tusi lako atakurudishia hapo hapo."

Prof. akanyanyua mikono yake akawaombea dua hawa wazalendo - Komredi mmoja na Mwana ASP mmoja.

Tukamuaga.
Tukasimama nje.

Akanyanyua tena mikono kutuombea dua na tulipokuwa nje tunaagana akatuombea tena dua nzito akimuomba Allah asitutwishwe sisi mizigo mizito tusiyoweza kuibeba.

Kama kawaida yake Mzee Kissinger haachi kutuvimbisha vichwa anauliza ati yeye nani hara anatembelewa na Bwana Mkubwa wa Ujiji, Hamisi Hababi.

Hababi ni mmoja wa vipenzi wa Mzee Kissinger kiasi sijui ni nani anampenda mwenzake zaidi.

Hajanitembelea Hamisi Hababi akaacha kumtaja Prof. Kissinger akinieleza nini kaelezwa na Mzee Kissinger yeye hakuwa anakijua.

Katika mazungumzo yetu lazima Mzee Kissinger ataingia kati.

Allah ampe afya njema mwalimu wetu na azidi kumfurahisha kama anavyowafurahisha wote wanaomtembelea nyumbani kwake.

Amin.
 
Back
Top Bottom