Taasisi za afya zitekeleze utunzaji salama wa taarifa za wagonjwa

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Usiri wa Taarifa za Mgonjwa.jpg

Taarifa za matibabu ni miongoni mwa nyaraka nyeti zaidi kwa mtu yeyote. Kuweka salama taarifa za mgonjwa ni sehemu muhimu ya kudumisha uaminifu wa mgonjwa, na pia kulinda utu na heshima yake.

Katika mlolongo wa kupata matibabu wakati fulani mgonjwa analazimika kufichua taarifa zake binafsi, tena wakati mwingine ni zile nyeti zaidi, hivyo ni lazima awe na imani ya juu kabisa na daktari wake ili kutzioa kwa uwazi.

Hebu fikiria ulimshirikisha mtu fulani jambo, kisha mtu huyo akaenda na kumwambia mtu mwingine wakati ulidhani kwamba habari hiyo ingebaki kati yenu wawili tu. Sasa imekuwa ni habari ya mtaa mzima na unahisi kuumizwa, kusalitiwa, na kuaibishwa. Uaminifu wako umevunjika na uhusiano umeharibika.

Sasa fikiria kwamba mtu aliyevunja uaminifu wako alikuwa daktari na kwamba taarifa aliyowashirikisha wengine ni majibu ya uchunguzi wa afya yako. Ni dhahiri lingekuwa jambo la kutia hasira na la kuumiza. Hii ndiyo sababu usiri wa mgonjwa katika huduma ya afya ni muhimu sana—hujenga uaminifu, husaidia mgonjwa kupata huduma bora zaidi, huhifadhi sifa ya daktari na hospitali, na pia ni hitaji la kisheria. Hakuna mtu anayeruhusiwa kusambaza taarifa zako za afya bila ruhusa yako.

Ukweli ni kwamba baadhi ya magonjwa kama vile magonjwa ya zinaa na magonjwa ya afya ya akili, bado yana unyanyapaa unaohusishwa nayo. Hivyo, sifa au ustawi wa mtu katika jamii unaweza kudhurika ikiwa hali zao za kiafya zitawekwa hadharani. Mgonjwa anaweza kuhisi aibu na huenda ikasababisha kujidhuru au kuvunjika moyo wa kutafuta matibabu dhidi ya matatizo yanayomkabili.

Iwe ni kazini au nyumbani, kila mtu anataka kutazamwa kulingana na uwezo wake—si kwa magonjwa au hali za kiafya walizo nazo. Kuweka mambo binafsi kuwa ya faragha huhakikisha kwamba waajiri, shule, wenye nyumba, na jamii kwa ujumla hawamhukumu mtu kulingana na ugonjwa alio nao.

Lakini pia, ujinga unaweza kusababisha watu kuwa na mawazo potofu kuhusu magonjwa fulani, hivyo hofu zao na ubaguzi vinaweza kuleta athari mbaya kwa mtu ambaye ugonjwa wake umewekwa hadharani kwa watu wengine.

HOSPITALI YA KAIRUKI MNAWEZA KUWA BORA ZAIDI YA HIVI
Sasa basi, nije kwenye point yangu. Juzi kati nilifika kwenye moja ya vituo vya Hospitali ya Kairuki kupata huduma kisha nikathibitika kuwa ninahitaji dawa. Nilifungiwa dawa kwenye "bahasha ya mchongo" ila kwa udadisi wangu nikaifungua kujionea maudhui yaliyomo ndani ndipo nikagundua zilikuwa ni taarifa ya vipimo vya Ultrasound vya mtu fulani ambaye baadhi ya taarifa zake zinaonekana.

Ingawa baadhi ya taarifa kama utaifa, wilaya na mkoa atokao mgonjwa havijawekwa bayana, lakini ni dhahiri kuwa yapo majina ya watu fulani ni ya kipekee na ukiliona tu unaweza kujua ni nani - hasa ikiwa na umri wake umewekwa wazi kama hivi.

Kuna nyakati hatuhitaji taarifa lukuki kujua nani ni nani, kwahiyo utunzaji wa taarifa haupaswi kuacha hata chembe ikiwa uchi.

Usiri Kairuki.jpg

Nilipata wasiwasi kuwa huenda hata taarifa za vipimo vya "gonjwa" langu huenda zikawa hadharani siku moja.

Ushauri wangu kwa KH ni kwamba ili kuzuia uvujaji wa taarifa binafsi za wagonjwa kama hivi ni kuwa na mpango wa usalama wa data. Ni vyema kuhakikisha kuwa wafanyakazi muhimu pekee ndio wanaoweza kufikia taarifa fulani, lakini pia kuhakikisha uteketezaji wa nyaraka kama hizi ili zisilete madhara kwa jamii.

Usiri wa taarifa za mgonjwa ni muhimu kwa wagonjwa, madaktari na taasisi za huduma za afya. Usiri huu hudumisha heshima ya jumuiya ya kitabibu.
 
Safi sana hii inapaswa ioewe zawadi kama ingekuwa ipo kwenye Stories of Change. Sijui kwanini hukupata hio idea ya kuandika.
 
Ingekuwa nchi zilizoendelea ndugu mgonjwa ungekuwa ushaenda mahakamani sasa hivi unasubiria tu cheki iive upewe chako. Hapo hospitali imeamua kupunguza gharama za vifungashio kwa kutumia karatasi zenye taarifa za wateja wake.

Ugonjwa ni siri ya mgonjwa na wahudumu wa afya, Kairuki wakumbuke hilo.
 
Umekumbusha jambo la muhimu sana. Hospitali nyingi tu wanafungia dawa karatasi za namna hii, ni hatari taarifa za mgonjwa zikawekwa peupe bila idhini yake.
 
Ingekuwa nchi zilizoendelea ndugu mgonjwa ungekuwa ushaenda mahakamani sasa hivi unasubiria tu cheki iive upewe chako. Hapo hospitali imeamua kupunguza gharama za vifungashio kwa kutumia karatasi zenye taarifa za wateja wake.

Ugonjwa ni siri ya mgonjwa na wahudumu wa afya, Kairuki wakumbuke hilo.
Hili tatizo inabidi limulikwe kwa karibu sana na kuwe na faini kali.
 
Taarifa za matibabu ni miongoni mwa nyaraka nyeti zaidi kwa mtu yeyote. Kuweka salama taarifa za mgonjwa ni sehemu muhimu ya kudumisha uaminifu wa mgonjwa, na pia kulinda utu na heshima yake.

Katika mlolongo wa kupata matibabu wakati fulani mgonjwa analazimika kufichua taarifa zake binafsi, tena wakati mwingine ni zile nyeti zaidi, hivyo ni lazima awe na imani ya juu kabisa na daktari wake ili kutzioa kwa uwazi.

Hebu fikiria ulimshirikisha mtu fulani jambo, kisha mtu huyo akaenda na kumwambia mtu mwingine wakati ulidhani kwamba habari hiyo ingebaki kati yenu wawili tu. Sasa imekuwa ni habari ya mtaa mzima na unahisi kuumizwa, kusalitiwa, na kuaibishwa. Uaminifu wako umevunjika na uhusiano umeharibika.

Sasa fikiria kwamba mtu aliyevunja uaminifu wako alikuwa daktari na kwamba taarifa aliyowashirikisha wengine ni majibu ya uchunguzi wa afya yako. Ni dhahiri lingekuwa jambo la kutia hasira na la kuumiza. Hii ndiyo sababu usiri wa mgonjwa katika huduma ya afya ni muhimu sana—hujenga uaminifu, husaidia mgonjwa kupata huduma bora zaidi, huhifadhi sifa ya daktari na hospitali, na pia ni hitaji la kisheria. Hakuna mtu anayeruhusiwa kusambaza taarifa zako za afya bila ruhusa yako.

Ukweli ni kwamba baadhi ya magonjwa kama vile magonjwa ya zinaa na magonjwa ya afya ya akili, bado yana unyanyapaa unaohusishwa nayo. Hivyo, sifa au ustawi wa mtu katika jamii unaweza kudhurika ikiwa hali zao za kiafya zitawekwa hadharani. Mgonjwa anaweza kuhisi aibu na huenda ikasababisha kujidhuru au kuvunjika moyo wa kutafuta matibabu dhidi ya matatizo yanayomkabili.

Iwe ni kazini au nyumbani, kila mtu anataka kutazamwa kulingana na uwezo wake—si kwa magonjwa au hali za kiafya walizo nazo. Kuweka mambo binafsi kuwa ya faragha huhakikisha kwamba waajiri, shule, wenye nyumba, na jamii kwa ujumla hawamhukumu mtu kulingana na ugonjwa alio nao.

Lakini pia, ujinga unaweza kusababisha watu kuwa na mawazo potofu kuhusu magonjwa fulani, hivyo hofu zao na ubaguzi vinaweza kuleta athari mbaya kwa mtu ambaye ugonjwa wake umewekwa hadharani kwa watu wengine.

HOSPITALI YA KAIRUKI MNAWEZA KUWA BORA ZAIDI YA HIVI
Sasa basi, nije kwenye point yangu. Juzi kati nilifika kwenye moja ya vituo vya Hospitali ya Kairuki kupata huduma kisha nikathibitika kuwa ninahitaji dawa. Nilifungiwa dawa kwenye "bahasha ya mchongo" ila kwa udadisi wangu nikaifungua kujionea maudhui yaliyomo ndani ndipo nikagundua zilikuwa ni taarifa ya vipimo vya Ultrasound vya mtu fulani ambaye baadhi ya taarifa zake zinaonekana.

Ingawa baadhi ya taarifa kama utaifa, wilaya na mkoa atokao mgonjwa havijawekwa bayana, lakini ni dhahiri kuwa yapo majina ya watu fulani ni ya kipekee na ukiliona tu unaweza kujua ni nani - hasa ikiwa na umri wake umewekwa wazi kama hivi.

Kuna nyakati hatuhitaji taarifa lukuki kujua nani ni nani, kwahiyo utunzaji wa taarifa haupaswi kuacha hata chembe ikiwa uchi.

Nilipata wasiwasi kuwa huenda hata taarifa za vipimo vya "gonjwa" langu huenda zikawa hadharani siku moja.

Ushauri wangu kwa KH ni kwamba ili kuzuia uvujaji wa taarifa binafsi za wagonjwa kama hivi ni kuwa na mpango wa usalama wa data. Ni vyema kuhakikisha kuwa wafanyakazi muhimu pekee ndio wanaoweza kufikia taarifa fulani, lakini pia kuhakikisha uteketezaji wa nyaraka kama hizi ili zisilete madhara kwa jamii.

Usiri wa taarifa za mgonjwa ni muhimu kwa wagonjwa, madaktari na taasisi za huduma za afya. Usiri huu hudumisha heshima ya jumuiya ya kitabibu.
Well
 
Back
Top Bottom